Mchanganyiko wa FDLR na CNDP unaweza kuunganishwa na Meremeta?

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
8,755
Likes
5,146
Points
280

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
8,755 5,146 280
Makao makuu FDLR na CNDP yapo katika jimbo la Kivu lililopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Tokea nilifahamu jimbo hili la Kivu nimekuwa nafuatilia kujua hasa kwanini pale pana mzozo.

FDLR iliundwa na wanamgambo wa kihutu waloitwa Intarahamwe ambao walikuwa wakiwasaka na kuwauwa wale wote walokuwa wakishikiri kwenye mauaji dhidi wa watu wa kabila la Watusi mwaka 1994.

Lakini wengi wa wanamgambo hawa walikimbilia nchini DRC katika jimbo hili la Kivu baada ya raisi wa sasa wa Rwanda Paul Kagame kushika madaraka nchini Rwanda.

Katika miaka ya hivi karibuni serikali ya DRC ikisaidiwa na vikosi vya umoja wa mataifa wamekuwa wakifanya kampeni ya kuwaondoa kama si kuwatokomeza wanamgambo hawa wa FDLR. Hiyo pia ikiwa ni katika kudumisha ushirikiano wake na serikali ya Rwanda ambayo nayo imekuwa na kazi ya kutokomeza kikundi cha wanamgambo wa CNDP ambao kiongozi wake Laurent Nkunda alikamatwa na majeshi ya Rwanda na mpaka sasa yupo chini ya ulinzi akisubiri kujibu mashitaka kwenye mahakama ya kimataifa.

Vikosi vya CNDP vyote vimeungwanishwa na jeshi la DRC na vilikuwa vimeundwa na wale watusi wa DRC na kwa kuwa ni kabila moja na raisi Kagame walikuwa wakisema wanapigana kulinda maslahi ya watusi dhidi ya mashambulizi ya FDLR. Lakini mpaka sasa vikosi vya Laurent Nkunda vya CDNP vina nguvu kutokana na vita inayoendeshwa dhidi ya vikosi vya FDLR ambavyo vinaonekana kutosaidia kumaliza tatizo na pia ikumbukwe kwamba FDLR na CNDP wote ni wa kabila la Watusi.

Ingawa wanamgambo wa FDLR walionekana kama wameondolewa katika maeneo yote yenye migodi ya dhahabu, inaonekana kwamba wameyakamata tena maeneo hayo ya mashariki mwa Kongo na wamekuwa pia sasa wakisajili watu wa Kongo na Wahutu wa kutoka Rwanda. Pia inasemekana idadi ya wapiganaji ni kubwa kuliko inavyofikirika.

Kiini cha yote haya ni utajiri wa dhahabu ambao umeikumba DRC tokea itawaliwe na wabelgiji. Katika mkutano wa Berlin 1984-1985 uloitishwa na Chancellor Bismark , wakoloni wengi walikutana na ulikuwa ni mkutano wa kuigawa Afrika.

Mfalme Leopold wa pili aliitaka Congo na akapewa kuimiliki kama mali yake binafsi. Aliita ‘Cede Congo' kama jimbo kule Ubelgiji. Mfalme Leopold wa pili alishutumiwa sana kwamba alikuwa anauwa watu hovyohovyo na kuchukua dhahabu yote kupeleka kwao Ubelgiji.

Leo hii 2010 Ubelgiji ni makao makuu ya Umoja wa nchi za Ulaya, makao makuu ya umoja wa nchi za ujihami- NATO na mashirika mengine ya kiulayaulaya.

Congo kama Congo imebaki ikiwa nchi isio na dira, wanajeshi wake wanawasaidia wanamhambo wa FDLR kwa kuwapa silaha na vifaa vingine. Hali hii inawasaidia FDLR kuendelea kuchimba dhahabu na madini mengine adimu kama yale yaitayo Tin duniani na kuyavusha nje ya Kongo kwa msaada mkubwa wa baadhi ya viongozi wa nchi za maziwa makuu.

Jambo moja ambalo ni muhimu kufahamu ni kwamba FDLR ina watu wengi wanaoiunga mkono wakiwa nje ya Kongo na Afrika kwa ujumla. Kuna mtandao ambao unashughulika na upangaji wa shughuli za kijeshi nchini humo, usafirishaji wa silaha na masuala yoote ya fedha.

Ilikuwa ikiaminika kwamba chanzo cha mapato kwenda FDLR ni hao walioko nje na kwa kufuatilia mawasiliano ya simu inaonesha makamanda wakipiga simu kwenda kwa viongozi wa serikali za Afrika, vyama vya kujitolea na kwingine.

Maswali nnayojiuliza ni kwamba vikosi vya umoja wa mataifa MONUC vipo nchini DRC kwa muda sasa kazi yao ni ipi hasa?

Kwa nini mpaka leo Jenerali Bosco Ntaganda hajakamwatwa kujibu mashtaka ambapo anatuhumiwa kuamrisha mauaji, mateso, ubakaji, kulazimisha watoto wajiunge na jeshi. kwa sababu inajulikana Jean Piere Bemba tayari yupo ndani.


Na mwisho je FDRLna CNDP ndio waendeshao Kongo na nje ya mipaka yake hasa maziwa makuu?
 

Forum statistics

Threads 1,190,287
Members 451,082
Posts 27,666,623