Adolph Leonard
Member
- Oct 14, 2011
- 49
- 44
Wadau nimeona ku-share na nyie jambo hili huenda ikawa sababu ya kusaidia kuokoa uhai wa watu wanaosumbuliwa na maradhi hayo, ikumbukwe kwa sasa Dunia inapita kwenye taharuki kubwa ya ugonjwa unao sababishwa na virusi vya Corona, na watu wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kujinusuru na janga hilo, siku ya ijumaa nilipata taharuki kidogo nilipo amka asubuhi mwenza wangu alikuwa ana joto kali sana, mafua makali na pia alikuwa analalamika kifua kinambana.
Nilipata khofu sana maana ni miongoni mwa dalili na hili janga la sasa, ukizingatia mwenzangu huyo anafanya kazi hospital kubwa sana hapa nchini, kama mwanaume niliona ngojea nijiongeze ili kuweza kumnusuru mwenzangu, so nilienda duka la dawa nikanunua vicks ya kikopo, pia nikaenda duka la dawa za asili nikanunua dawa inaitwa COGONI, nikarudi home, nikachukua vitunguu Swaumu vya kiasili 2 nikaponda, na mbegu za Habbat sawda (black seed), nikachemshwa mchanganyiko wa vitunguu Swaumu, Habbat sawda na vicks.
Baada ya hapo, nikaweka matone 5 ya COGONI nikampa ajifushe, wadau ndani ya dakika 5, mafua yalikata kifua kikaachia, akawa mzima wa afya, nashauri wadau ambaye atakuwa amepata dalili hizo ajaribu na yeye kutumia njia hii huenda ikawa msaada kwake.
Asanteni.
Sent using Jamii Forums mobile app