Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
2355406_ginger.jpg

Heshima kwenu wakuu.

Ninaambiwa na watu kwamba kilimo cha tangawizi kinalipa sana kwa sababu soko la uhakika lipo na ni zuri. Nimeshaelekezwa sehemu ambayo hili zao linakubali uzuri.

Ombi langu ni kwa wale wenye uzoefu na kilimo hiki wanipe A,B,C zote kuhusu kilimo cha zao hili. Ningependa kujua kuhusu gharama ninazoweza kukumbana nazo mpaka zao hili lifikie hatua ya kuvunwa toka shambani.

Thanks in advance.

MASWALI/ MAHITAJI YA WADAU KUHUSU KILIMO HIKI
Habari wana JF,

Moja kwa moja kwenye hoja. Nina mpango wa kulima tangawizi maana nimesikia kinalipa ingawa sina ABC's za kilimo hicho.

Naomba kuelewa ni jinsi kilimo hiki huendeshwa na soko la tangawizi yenyewe. Nataka kuelewa kama kilimo hiki kinawezekana maeneo ya pwani kama Mkuranga, upatikanaji wa mbegu, gharama za kulima na mapato yatokanayo na kilimo.

Ni wapi naweza kupata taarifa zaidi ya kilimo hiki?

Nikipata contacts nitashukuru.
Habari zenu wana JF,

Naomba kama kuna mwana JF anayejishughulisha na kilimo cha Tangawizi anipatie mawasiliano yake ili niweze kununua tangawizi nitakazo weza kutumia kama mbegu shambani kwangu. Nakaribisha mawazo mbadala kuhusu namna ya kulima na soko la zao hili ndani ya nchi yetu.

Karibuni tubadirishane uzoefu kuhusu kilimo cha zao hili.

Ahsanteni

MREJESHO WA WADAU
Kilimo cha Tangawizi/ Ginger Farming

UTANGULIZI
Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Ambao huonekana kama mizizi ya mmea. Mmea huu kitaalamu huitwa zingiber officinale.

Asili ya mmea huu sehemu za kitropiki za bara la Asia hasa nchi za china za india. Zao hili huzalishwa kwa wingi nchini Jamaica.

Hapa nchini zao hili huweza kustawi katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Ruvuma, kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.

MATUMIZI
Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na changamsha katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, n.k

Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k.

KILIMO CHA TANGAWIZI SONGEA MADABA
Madaba ipo mkoa wa Ruvuma, wilaya ya Songea vijijini, ipo njiani inapotokea Njombe kwenda Songea mjini hivyo kifupi inapatikana katikati ya Njombe na Songea. Iyo huifanya Madaba kuwa na hali ya Hewa mbili ile ya Njombe na Songea. Pia Madaba ina rutuba ya kutosha kuweza kuhimiri mazao mengi ya kibiashara kama kahawa, Tangawizi, Ufuta, Soya, Ulezi n.k na ya chakula kama Mahindi, Maharage, Mpunga n.k hustawi maeneo ya Madaba.

Rejea kichwa cha habari, Tangawizi ilianzwa kulimwa Madaba kama moja ya zao la kibiashara mwaka 2013. Hivyo kuwapatia wakazi wengi wa madaba fursa hii ya kibiashara na kila mkazi asiye lima basi huwa na ndoto hii kuwa ‘’ili nitoke kimaisha basi nijitahidi nilime Tangawizi’’. Basi Tangawizi ni uti wa mgongo kwa mkazi wa Madaba.

Fursa hii pia inakujia wewe pia mwananchi wa Tanzania popote ulipo, kwa kufuata ushauri na utaalamu wa wakazi wa Madaba pia unaweza kuwa na ndoto zile zile za ‘Tangawizi mkombozi’.

Basi nami kama rafiki wa Tangawizi nimekuandalia ‘’ kiarticle’’ hiki basi ili nawe uweze kuwa rafiki ya Tangawizi pia.

TABIA YA MMEA
Kama nilivyodokeza hapo juu, mmea huu huvunwa kama Tunguu hivyo basi; hutambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi.

Ingawa hadi sasa kitaalamu haijasibitishwa kuwa ni aina gani ya tangawizi hulimwa hapa Madaba. Wengine husema ni white Africa (Jamaica) na wengine husema cochin (flint).Ambazo ndio maarufu hapa nchini Tanzania.

Kikubwa sio aina ya mmea bali uwezekano wa kustawi na kutoa matunda mazuri, aina hizi hutofautiana tu katika majani na ukubwa wa tunguu. Ambapo Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati cochin ina tuguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu.

HALI YA HEWA YA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1500 au zaidi. Huitaji mvua kiasi cha mm.1200-1800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigradi 20-25. Hustawi vyema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuwamisha maji.

UPANDAJI
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 800-1000 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekari moja.

Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.

Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 4-8 kwa hekari na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.

Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, na kawaida ni mara nne (4) wakati huo katika palizi ya tatu na ya nne hushauliwa kupandishia udongo kwa kila china la mmea ili kuupa mmea nafasi ya kutoa tunguu kubwa na nene

Pia dawa ya kuuwa wadudu kama simazine hutumika.

MAGONJWA NA WADUDU
Madoa ya majani yanayosababishwa na viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberisna Phyllosticta zingiberi.

Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp.

Mizizi fundo; inasababishwa na viini viitwavyo meloidegyne spp.

UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 8-12 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana.

USINDIKAJI
Tangawizi ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16%-18%.

SOKO LA TANGAWIZI
Soko la Tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, Hapa nchini huuzwa kwa bei ya Tshs. 2000 - 4000/= kutegemea msimu.

GHARAMA ZA UZALISHAJI NA MAPATO
(Gharama ya hekari moja)

Kukodi shamba Tshs.=100,000/=
Mbegu 2,,000, 000/=
Kulima 100,000/=
Kupanda 100,000/=
Kupalilia x 4 @ 90,000/= jumla = 360,000/=
Mbolea / samadi 150,000/=
Jumla 2,810,000/=

Mapato kwa hekari.

Gharama hizi hutegemea sana na msimu zinaweza shuka au kupanda zaidi.
Hatua za kuzingatia

Kwa ujumla tangawizi hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawizi zinastawi.

KUANDAA SHAMBA
Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya April, May au June, ni vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu, Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia November unaweza kuanza kupanda.

KUPANDA
Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia mbolea ya mboji au samadi na usitumie mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz.

Huchukua wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili ya kwenda kupanda. Palilia Mara Majani yanaoota na pandishia udongo kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.

MAGONJWA
Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).

KUVUNA
Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz huwa ya njano na huanza kunyauka.

Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport, wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani. Uzuri tangawizi unaweza kusubiri soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka.

Jamani tusiogope kuwekeza na kujaribu fursa mpya. Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali

Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzàlisha mbegu ambazo utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata uzoefu kupitia hapo na kujua kama eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa kilimo cha tangawizi.

Sokoni tangawizi huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg. Usikatishe tamaa pale tangwizi inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubiri kwa mda mfupi na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa hupanda kwa haraka.
Faida kwenye kilimo cha Tangawizi ipo
Kwa uzoefu wangu kwa eka moja unahitaji si chini ya kg1,000 ya mbegu, afadhali kg 1,300. Na kama umelima vizuri na ardhi yako inakuwa nzuri na umepalilia ipasavyo unaweza kupata kati ka kg 6,000 mpaka 9,000 kawaida.

Ukiacha tena kwa ajili ya mbegu kg 1,300 utauza kg4,700 mpaka kg7,700 ya tangawizi mbichi sokoni. Ila mwaka wa kwanza ni majaribio unaweza kupata chini ya hayo sababu ya kukosa uzoefu wakati wa kupanda au kupalilia au mengineyo. Bei ya Kg moja ya mbegu inategemea lini unapojaribu kuinunua.

Kwa mfano mwaka jana tumenunua kwa Tsh800 kg moja, mwaka huu inawezekana bei ya kg ni tsh1,000 hapo Madaba. Faida ipo sana, lakini unahitaji muda wa kujifunza na pia kutafuta soko. Miaka mengine wanunuzi watakuja mpaka shamba lako mengine inabidi uwatafute sana.

Kwa ufupi mtaji wa kuanzia ni kubwa kidogo lakini faidha ni kubwa sana ukijitahidi kulima vizuri na kuitunza (shamba lako likiwa mbali na bila ulinzi wezi wanaweza kuja na kuiba tangawizi lako). Wengine wamelima eka nyingi na saizi wanakuwa na pesa ya kutosha.

Mimi binafsi silimi, analima mke wangu, lakini baada ya Miaka miwili tangu alipoanza anaweza kujenga nyumba nzuri kijijini na analeta pesa ya kutosha kwa familia Dar es Salaam.
Ni vema kumshirikisha Bwana Shamba/ Mtaalam wa Kilimo

Madaba (sijui sehemu nyingine) unaanza kuandaa shamba Oktoba na unapanda Novemba. Unaweza kuvuna June au unaweza kuiacha mpaka Oktoba Novemba mwaka ujao, inategemea bei unaoikuta June, kama ni bei ya chini sana kama mwaka jana afadhali uiache ardhini kwanza. Lakini hata kwa bei ya chini bado ungepata faida ukifanya hesabu. Ukiuza unauza kwa kilo.

Wakati tangawizi lipo shambani inabidi upambane na kupalilia mara kadhaa walau mara mbili na afadhali mara tatu. Pia tangawizi haipendi Maji ya mvua ikae ardhini sana na majani yake mwanzoni hayapendi jua kali. Ni nzuri daima kushirikiana na bwana shamba wa eneo husika ili apime Ph ya ardhi na akuelekeze wapi ni pazuri kupanda na wapi usipande.

PIA, SOMA:

Kilimo Bora cha Tangawizi

UTANGULIZI:
Jina la kisayansi: Zingiber officinale
Familia: Zingiberaceae

Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k. Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k).

AINA ZA TANGAWIZI
Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo hulimwa Tanzania ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica) na Cochin (flint).

BIOLOGIA YA MMEA WA TANGAWIZI
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni membamba marefu ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.

HALI YA HEWA NA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha mm.1, 200 - 1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20 - 25. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji na wenye pH 5.5 – 6.5.

UPANDAJI
Zao la tangawizi hupandwa Kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 336 - 680 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika ekari moja.

Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita 23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita 5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta, hivyo unaweza tengeneza tuta lenye upatana wa mita 1. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.

MBOLEA
Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 10 - 12 Kwa ekari na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK. N 40 – 48 kg, P2O5 31.2 – 32 kg, na K2O 40 – 48 kg. Mwanzoni tumia nusu ya Nitrogen na kiasi chote cha P na K, kiasi kilichobaki cha Nitrogeni kitumike siku ya 45 na 90 baada ya kupanda. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana. Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua magugu, Kama simazine hutumika.

UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulingana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 8 - 12 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana kwa ekari.

Chanzo: horttechservices.com
 
Attachments

  • ginger.jpg
    ginger.jpg
    122.1 KB · Views: 28
Nataka kulima tangawizi mkoani Mbeya hususani Tunduma.

Swali kwa wataalamu; je, hali ya mkoani mbeya inakubaliana na zao hili?

Kuna jamaa kanambia kuwa zao hili linahitaji misimu miwili ya mvua kwa mwaka kwasababu tangawizi huchukua miezi nane hadi kumi kufikia hatua ya kuvunwa.

Nina hofu kama kweli mkoani mbeya mvua za vuli ni za uhakika.
Naombeni ushauri wenu wataalamu.
 
Je, ni wapi soko la tangawizi linapatikana kwa wingi? je kg 1 inakwenda kwa bei gani? wapi tangawizi soko lake la uhakika? Muhimi please coz nimesikia kuwa kuna viwanda vinanua Tangawizi, ningependa pia kujua bei zao kiwanda wanazonunulia.
 
Je ni wapi soko la tangawizi linapatikana kwa wingi? je kg 1 inakwenda kwa bei gani? wapi tangawizi soko lake la uhakika? Muhimi please coz nimesikia kuwa kuna viwanda vinanua Tangawizi, ningependa pia kujua bei zao kiwanda wanazonunulia.
Yeah,
Ngoja werevu wa hii issue waje.
 
Habari wandugu,

Natafuta mbegu ya tangawizi, nahitaji kupanda mwenye nayo au pia msaada wa maeneo zinapopatikana anisaidie tafadhali.
 
Habari ndugu zangu?

Kwanza mniwie radhi kwan kifaa changu kilizma chaji kabla sijapost. Nahitaji kupata maarifa juu ya kilimo cha tangawizi , je mbegu nzuri ni aina gan? Zinapatikana wap? Je huchukua muda gan mpaka kuvuna? Kama nikiweza kupata gharama Zake na faida. Nitafurahi pia kupata uzoefu mwingne juu ya kilimo hiki.

Asanteni sana
 
Kwa ujumla tangawizi hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawizi zinastawi.

KUANDAA SHAMBA
Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya
April, may au June, ni vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu, Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia November unaweza kuanza kupanda.
.
KUPANDA

Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia mbolea ya mboji au samadi na usitumie mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz.

Huchukua wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili ya kwenda kupanda. Palilia Mara Majani yanaoota na pandishia udongo kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.

MAGONJWA
Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).

KUVUNA
Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz huwa ya njano na huanza kunyauka

Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport, wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani. Uzuri tangawizi unaweza kusubiri soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka.

Jamani tusiogope kuwekeza, na kujaribu fursa mpya, Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali

Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzàlisha mbegu ambazo utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata uzoefu kupitia hapo na kujua kama eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa kilimo cha tangawizi.

Sokoni tangawizi huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg. Usikatishe tamaa pale tangwiz inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubir kwa mda mfupi na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa hupanda kwa haraka.
 
Kwa ujumla tangawiz hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawiz zinastawi.

Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia mbolea ya mboji au samadi na usitumie mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz. Huchukua wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili ya kwenda kupanda. Palilia Mara Majani yanaoota na pandishia udongo kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.

MAGONJWA
Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).

KUVUNA
Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz huwa ya njano na huanza kunyauka

Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport, wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani. Uzuri tangawizi unaweza kusubiri soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka.

Jamani tusiogope kuwekeza, na kujaribu fursa mpya, Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali

Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzàlisha mbegu ambazo utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata uzoefu kupitia hapo na kujua kama eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa kilimo cha tangawizi.

Sokoni tangawizi huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg. Usikatishe tamaa pale tangwiz inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubir kwa mda mfupi na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa hupanda kwa haraka.
Hizo mbegu kwa hekta moja hugharimu shilingi ngapi?
 
Kwa ujumla tangawiz hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawiz zinastawi.

KUANDAA SHAMBA
Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya April, May au June, ni vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu, Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia November unaweza kuanza kupanda.
.
KUPANDA

Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia mbolea ya mboji au samadi na usitumie mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz.

Huchukua wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili ya kwenda kupanda. Palilia Mara Majani yanaoota na pandishia udongo kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.

MAGONJWA
Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).

KUVUNA
Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz huwa ya njano na huanza kunyauka

Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport, wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani. Uzuri tangawizi unaweza kusubiri soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka.

Jamani tusiogope kuwekeza, na kujaribu fursa mpya, Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali

Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzàlisha mbegu ambazo utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata uzoefu kupitia hapo na kujua kama eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa kilimo cha tangawizi.

Sokoni tangawizi huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg. Usikatishe tamaa pale tangwiz inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubir kwa mda mfupi na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa hupanda kwa haraka.
Costs za kulima na kupanda mpaka unapovuna ni sh.ngapi mkuu, maana umeweka tu bei yake sokoni
 
Back
Top Bottom