Mchanganuo na ushauri kuhusu biashara ya nguo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchanganuo na ushauri kuhusu biashara ya nguo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Qsm, Mar 26, 2010.

 1. Q

  Qsm JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 400
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Naomba msaada wenu nina duka la nguo la kawaida tu na lipo eneo zuri la biashara kinachonishangaza sipati faida kabisa je kuna yeyote kwenye biashara hiyo ambaye anaweza kunishauri jinsi ya kulisimamia? Mimi ni mfanyakazi kwa hiyo si mara kwa mara nakuwa dukani hapo.

  Naombeni ushauri tafadhali.


  ===========================================

   
 2. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nataka kukushauri ila kwanza naomba unijibu hili swali/maswali kwani sikuona kokote ulipoeleza kwenye post yako.

  Je,unapata hasara na biashara/duka lako ina muda gani?
   
 3. Pilato2006

  Pilato2006 Senior Member

  #3
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nenda Bagamoyo!!
   
 4. J

  Jafar JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nikuulize: Hela ya kula inatoka hapo hapo?
   
 5. Q

  Qsm JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 400
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  lina miaka mitatu sasa
   
 6. Q

  Qsm JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 400
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Hapana huwa sichukui kabisa
   
 7. Arsenal

  Arsenal Senior Member

  #7
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 191
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hela yako inarudi?(break even)
   
 8. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ikiwa hakuna faida kwa miaka mitatu yote na labda pia huna hasara inawezekana ni usimamizi mbay

  hakikisha unajitahd baada ya muda wa kazi pita dukani angalia mauzo ya siku hiyo, weka kumbukumbu ya kila bidhaa inayoingia na kutoka dukani kuwa na daftari lenye kumbukumbu za vitu vyote naamni kama nguo zinatoka na unaingiza nyingine lazima kuwe na faida.
   
 9. Q

  Qsm JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 400
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  nimewahi kuhesabu fedha za mauzo pamoja na stock iliyopo naona kuwa mtaji hauongezeki
   
 10. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Acha kuuza nguo zilizotoka uchina, Dubai etc zisizo na ubora, usifuate mkumbo, uza vitu bora, unique vitanunuliwa
   
 11. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwani kasema anauza za kichina? lakini pia sioni shida iwe ya kichina ama inatoka uk mradi ipate mteja, ni kuchagua tu zile zilizopo kwenye fashion kulingana na wakati uliopo
   
 12. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Miaka mitatu,ni mingi kwa biashara kama hiyo yako ya nguo.Nadhani kuna mambo machache tu unahitaji kufanya ili uweze kuiona faida hiyo ya hicho unacho kifanya.
  Kama biashara/Duka linajiendesha lenyewe kwa maana lina lipa kodi zote za nyumba,Tra na Mishahara au mshahara kwa kipindi chote cha miaka mitatu,basi hilo duka lako lina faida sana,tena sana.

  Kama mchangiaji mmoja hapo juu alivyo shauri,Fanya uwe unaangalia ana uwe na muda na biashara na hesabu zake zote,usiache kila kitu kwa mtu/watu bila ya uangalizi wako mwenye.
   
 13. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  pia angalia upande wa choice....labda hukidhi mahitaji ya wateja,
   
 14. Q

  Qsm JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 400
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  sawa ila nguo hizo ndizo zinanunuliwa sana maeneo hayo. lakini nitalifanyia kazi wazo lako.
   
 15. n

  newazz JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Dada huyu hajasema anauza nguo za China au Dubai, sasa kwanini ufikiri hivyo? Halafu JF ni The home of Great Thinkers?

  Dada ni hivi..

  1. Nenda kwenye mipango ya awali uliyopanga kwa ajili ya duka hili.
  2. Je mipango inafuatwa?
  3.Kwanini mipango inafuatwa na bado kuna hasara?
  4. Je kuna tofauti yoyote ya mauzo ya mwanzo na sasa.
  5. Je mtaji wako umeongezeka au umepungua tangu ulivyofungua?

  Ninachoona hapa ni usimamizi hafifu, unajua unapoanza biashara changa ni kama mtoto mdogo anatakiwa atunzwe kwa karibu na usimamizi makini ndipo aweze kukua na kujisimamia mwenyewe.

  Kwa biashara mpya unabidi usimamie kwa karibu ujue maendeleo ya mwanao ( duka hili).

  Usitumie pesa ya mtaji na ukumbuke kurudisha mtaji ( kureinvest )

  Mambo mengine je kuna ushindani mkubwa kutoka biashara za karibu,lazima zipo! Je duka au biashara yako inakidhi mahitaji ya wateja uliowalenga ?, ubora wa bidhaa, bei nk.

  Je huduma kwa wateja inaridhisha? Au msimamizi ndiyo amekuwa kama ndiye mfalme wakati wafalme ni wateja!!!

  Kwa ufupi unahitaji kwenda kwenye biashara yako na kuchunguza mambo madogo na ya msingi kama hayo juu ndipo utakapogundua pesa inaungulia wapi.

  Yapo mengi ya kufanyia kazi lakini hayo hapo juu ni ya msingi ya kukuonyesha muelekeo.
   
 16. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  biashara ya nguo imekuwa ngumu sana kwa sasa kutokana na watu wengi kuivamia.upinzani umekuwa mkubwa sana na ukiangalia kodi za flame zilivyokuwa juu ndio kabisaa.

  hii biashara nina experience nayo toka miaka ya 94 mpaka leo.miaka ya 94 na sasa tofauti ni kubwa sana kutokana na sababu hizo juu.kutokana na ugumu huo wengi tunategemea wateja wetu wa siku zote miaka nenda rudi huku wao wakileta wenzao na wengine wachache. wapya.

  ningekushauri vitu viwili vitatu kama unataka kuendelea nayo manake sasa hivi kutokana na ugumu wake watu wengi wamekimbilia kwenye ukulima.

  cha kufanya unapoleta mzigo jaribu kutafuta soko mikoani.unaweza kutafuta watu wa mikoani ukawauzia kwa jumla wao kama unaleta mzigo mwingi.

  kitu kingine jaribu kuleta mzigo mkubwa karibu na sikukuu kubwa zote,lazima hujue kutime hizi sikukuu kwnai hapo ndio biashara huwa kubwa na watu wanapenda mzigo mpya wakati huo.

  kitu cha mwisho wajue wateja wako,nikimaanisha jaribu kuangalia nguo zipi zinatoka zaidi ya nyingine,nguo za watoto ndio zaidi sijui kwako wewe kwahio unatakiwa kununua mzigo mkubwa wa nguo ambazo zinatoka sana.

  endelea na hizo hizo nguo za china kwani unalenga watu wenye kipato cha chini sio kila mtu anaweza kununua nguo kutoka marekani.

  nakutakia kila kheri kwenye biashara yako.
   
 17. Q

  Qsm JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 400
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  newazz na Arsenal Wenger nawashukuru mno mno kwa mchango wenu nitafanyia kazi maoni hayo kwani nina uzembe mkubwa wa kusimamia na kufuatilia kwa karibu duka langu.
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  wajua sasa biashara ya nguo imesambaa kila kona
  kama unaweza kubadrisha bidhaa katika duka lako au uwe unaenda na catalogue mpya mpya
  kuwa up todate kila siku
   
 19. N

  Nanu JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hebu pata likizo halafu simamia mwenyewe kwa muda ili uone mwelekeo!!!
   
 20. T

  Tall JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  kama huwezi kukaa mwenyewe kwa muda mpe muuzaji likizo.inawezekana anauza na kununua tana bidhaa bila wewe kujua ,faida anachukua
   
Loading...