Mchanga wa madini kuitwa copper concentrate ilikuwa ni hujuma ya kutuibia

Ndo maana nilikuuliza ulisoma Ripoti ya TMAA au kwavile JPM kasema ndo basi tena?! Sehemu ya ile ripoti hivi ndivyo inavyosema:
View attachment 514292

Hapa tena wanaendelea:
View attachment 514298

Kwahiyo badala ya kudanganya kwamba walikuwa wana-ignore uwepo wa metals zingine, hoja iwe kwanini hizo metals zingine other than gold, silve and copper zilikuwa zinafanywa mali ya smelters owners!!

Hapa chini wanaweka takwimu za major products:

View attachment 514299
Halafu unahoji:Are you seriously asking this question?!

Wewe unadhani ordinary economist anaweza ku-evaluate viability of smelting plants?

Au hufahamu kwamba kuna kitu kinaitwa Mining Economics na hawa Mining Economists ndio wenye uwezo wa kufanya analysis kama hizo na sio ordinary economist ambae probably amebobea kwenye macro- or microeconomics, or Business Economics, or International Trade au hata labda Agricultral Economics!!!!!!

But NOTE, neno viable ukilileta kwenye Kiswahili moja kwa moja lazima utapotosha tu! Kwa mfano unasema: "...smelter haingekuwa na faida kwa uchumi!"

TMAA hawakusema kitu kama hicho kwenye ripoti yao yote! Title of Study ilikuwa: A Study on Viability to Construct a Copper Concentrate Smelter in Tanzania.

Descrption yake inasema: Hakuna popote waliposema NOT PROFITABLE but not economically viable.

Tukichukua mfano huu huu wa copper concentrates tunaweza kuweka 2 alternatives ambapo miner atatakiwa kuchagua mojawapo!

Alternative 1; Miner anajenga smelter hapa hapa Tanzania. Akishafanya smelting na kutoa gharama zote, at the end anapata FAIDA, (say) ya $100 kwa kila tani moja.

Alternative 2 ni pale Miner anapoamua ku-export hiyo concentrates. Akitoa gharama zote through this process, let's anabaki na $105/ton.

Hapo Miner atakuambia it's not ECONOMICALLY VIABLE kujenga smelter Tanzania in exchange of exporting kwa sababu, hatua hiyo itamfanya apoteze $5 lakini sio kwamba atapata hasara!!!!

Remember, huyu ni mwekezaji ambae main goal ni ku-maximize profit! The guy has no interest na ajira ambazo zingepatikana kwa sababu, hizo ajira kwake ni additional COST!!!
Ukakasi wangu uko hapa tu...kwamba maelezo ya TMAA NI KWA HISANI YA MINER....Hahaha hahaha haha ha...na ndio maana nasema huyu miner aliamua kubatiza jina baya ule mchanga wa madini ili autoe kirahisi na akapige hela na kukwepa kodi.
 
Tatizo kubwa sana nchi hii ni kila mtu kujifanya anajua kila kitu....na wanasiasa ndio wanaongoza katika hili. Hebu tuchambue suala moja tu toka kwenye ripoti iliyokabidhiwa jana:
1. Tumeambiwa kuwa katika makontena hayo 277 kunasadikiwa kuwa na tani 7 mpaka 15 za dhahabu. Mimi nimeamua kuchukua hiki kiwango cha juu...yaani tani 15. Dhahabu hupimwa kwa ounces (wakia), na ounce 1 ni sawa na gramu 31.1035.

2. Tani 15 maana yake ni kilo 15,000 ambazo ni gramu 15,000,000. Hizi katika ounces ni 482, 260.

3. Bei ya sasa ya dhahabu ni dola 1,200 kwa ounce. Maana yake kama dhahabu yote hiyo ikifanikiwa kuwa extracted inaleta revenue ya dola 578,712,000 ambazo ni sawa na shilingi 1,273,166,400 (shs trilioni 1.27). Haya yatakuwa ndio mauzo ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa mwezi mmoja tu, tena hii ikiwa ni aslimia 30 tu ya mauzo yao kwa mwezi kwasababu asilimia 70 ya mauzo yao ya dhahabu yanafanyika kwa kuuza mikuo ya dhahabu wanayoibumba straight hapohapo migodini. Kwahiyo mauzo yao ya asilimia 100 kwa mwezi itakuwa kama shs trilioni 4.2.

4. Iwapo ni kweli kuwa tani 15 za dhahabu ziko kwenye hiyo asilimia 30 ya production yao, basi asilimia 100 ya production yao itakuwa ni tani 50 sawa na ounce 1,607,536 kwa mwezi. Kwa mwaka ina maana wana uwezo wa kuzalisha ounces kama milioni 19.

5. Migodi mingi inayofanya vizuri duniani kote kuweza kuzalisha ounce kati ya 75,000 na 100,000 kwa mwaka. Tulawaka Gold Mine katika uhai wake chini ya African Barrick Gold wa miaka 9 ulizalisha ounce 900,000 tu. Na huu unaingia kwenye historia kama moja ya migodi ya dhahabu Africa uliokuwa na deposit kubwa....ounce laki 9 zilizovunwa kwa miaka 9...yaani wastani wa ounce laki moja kwa mwaka.

Conclusion: Kuna walakini katika figures zilizotolewa kwenye ripoti. Hizo tani 15 ambazo ni ounce 482,260 ni production ya dhahabu ya miaka minne mpaka mitano kwa mgodi wenye gold concentration nzuri....unahitaji kuwa na grade ya 3 grams per tonne na uprocess tani kama 3,000 za kifusi madini ili upate walau ounce 8,000 kwa mwezi...sawa na kama ounce laki moja kwa mwaka. Hizo tani 15 yaani ounce 482,260 utazipata baada ya miaka minne. Na migodi yenye uwezo huo kwa sasa Tanzania ni mitatu tu...Geita, North Mara na Chunya.
Tupewe ripoti yote tuijadili.

NB: Kuhusu kwanini inaitwa copper concentrate...ni kwasababu copper ndio inakuwepo kwa wingi zaidi ya madini mengine yote. Acacia wao wameshatoa estimates zao kuwa kwa kila container kuna dhahabu around kilo 3 (yaani ounce kama 96), silver nayo 3kg na copper kama copper 3,000kg...hivyo copper ipo mara 500 as compared to other minerals. Kwa maneno mengine yale makontena yote 277 yana kama kilo 831 tu za dhahabu, haifiki hata tani moja...wakati ripoti inasema ni tani 15...yani zaidi kwa mara kumi.
Ungechukua kiwango cha wastani ingetosha kufikidha ujumbe.

Hivi hiyo report ya Tulawaka ni report ya mchimbaji mwenyewe au wataalamu wengine pia?

Halafu hapa utatufanya turejee kwenye swali la wakati mgodi unaanza...estimates za kiasi cha gold kilikuwaje?...swali ambalo haliwezi kujibiwa kwa wasaa na wachimbaji wakwepa kodi au watendaji wala rushwa....
 
Ukakasi wangu uko hapa tu...kwamba maelezo ya TMAA NI KWA HISANI YA MINER....Hahaha hahaha haha ha...na ndio maana nasema huyu miner aliamua kubatiza jina baya ule mchanga wa madini ili autoe kirahisi na akapige hela na kukwepa kodi.
Mbona unabadilisha magoli?! Mijadala haiendi hivyo!! Hoja yako ilikuwa ni suala la viability of smelter construction na madini ya aina nyingine!!!

Kuhusu suala la jina la copper concentrates, hata kwa Ripoti ile ya JPM bado inaswihi kuitwa copper concentrates!! According to ripoti ya JPM, wakati kontena moja lilikuwa na wastani wa 28kg za Gold, ndani yake kulikuwa na wastani wa kilo 6000 za copper!!

Sasa kama gold ni 28kg na copper ni 6000kg, kumbe kama si copper concentrates ulitarajia iitwe vipi?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Conclusion yao kwa nini ili-ignore fact kwamba kuna uwepo wa metals nyingine ...kwa nini haikueleza mustakabali wa metals nyingine??

Je TMAA walikuwa na utaalamu wa kiuchumi kuwa kwenye nafasi ya kuconclude kuwa na smelter haingekuwa na faida kwa uchumi ??
Serikali ya chama unacho shinda ukikitetea humu ndo mama wa hasara zote. Serikali ina kila kitu kinacho takiwa kufanya mambo yatokee, lakini hawafanyi, bungeni wamejazana wao, mamlaka yote yapo mikinoni mwao lakini wanacho kifanya ni aibu tupu....
 
Sijahamisha goli mkuu...hoja yangu ni kutaka kupinga kuwa yale madini mengine sio lolote na hivyo hayana maana kupigiwa hesabu za kodi...
my observation hawa jamaa walificha hapo awali na sasa wanatuambia si kitu....meaning hawataki kuyalipia kodi.
 
Serikali ya chama unacho shinda ukikitetea humu ndo mama wa hasara zote. Serikali ina kila kitu kinacho takiwa kufanya mambo yatokee, lakini hawafanyi, bungeni wamejazana wao, mamlaka yote yapo mikinoni mwao lakini wanacho kifanya ni aibu tupu....
Serikali ya CCM ni mama wa hasara zote lakini pia ni mama wa maendeleo yote....Hata wewe kuna faida na hasara ulizoleta kwenye familia yako.
 
Conclusion yao kwa nini ili-ignore fact kwamba kuna uwepo wa metals nyingine ...kwa nini haikueleza mustakabali wa metals nyingine??

Je TMAA walikuwa na utaalamu wa kiuchumi kuwa kwenye nafasi ya kuconclude kuwa na smelter haingekuwa na faida kwa uchumi ??
Sasa kama hawakua na utaalam,na waliambiwa waandike Ripoti kwa utafiti wao,ulitaka wasiandike chochote? Hujaona tunapeleka watu nje kutibiwa kwa sababu bado vifaa vyetu haviwez kufanya in depth analysis? Je vifaa walivyotumia Tume ni vile walivyo navyo TMAA?
 
Kama serikali inaamini mchanga huo una value kubwa kuliko hiyo waliosema accacia, kwa nini isiuuuze mchanga huo kwa mnada ili tupate hela tunayostahili?

Maana kama accacia wansema mchanga una value ya shilingi kumi na serikali inasema una value ya shilingi mia moja, njia nzuri ni kupiga mnada tupate hiyo mia na tuwagawie accacia hiyo kumi yao. Simple and fair.
 
In order to construct a viable smelter in Tanzania, it would require importing 60% of Copper Concentrate to feed the smelter, or Tanzania would have to increase its own production of Copper Concentrate through the development of more mines, and of similar production technology. However, there are currently no known copper sulphide deposits in Tanzania, which would add significantly to the Copper Concentrate requirements to feed the smelter to be constructed.

The study concludes that it is currently not feasible for a Copper Concentrate smelter to be constructed in the country to smelt and refine Copper Concentrate produced by BGM and BZGM. However, investors are encouraged to explore more on possibilities of discovering copper deposits which will warrant for installation of a Copper Concentrate smelter in the Country.

Source:
http://www.tmaa.go.tz/uploads/A_Stu...a_Copper_Concentrate_Smelter_in_Tanzania1.pdf
we dont need smelter... tunataka haki kwanza.. Na hata wao wakiwa na terms nzuri na uwazi wanaweza kuendelea kubeba mchanga...................... msitumwe kuwapumbaza watz na kuwatia hofu...... tunaibiwa... tunaibiwa
 
Kwa vile ripoti ya kamati ya kwanza ya rais inaonyesha kuna dhahabu mara kumi zaidi ya ile ambayo wanatangaza acacia mimi namshauri acacia ampe makontena yote yalimpa majibu rais na alete hizo dhahabu na madini mengine kama walivyopata kwenye uchunguzi

hapo ndo tutachujua acacia mwizi au maprofesa wetu wametudanganya
Na zaidi,ni vema kama ACACIA wako fair,wagharamie Kontena moja lile lenye uziko tani 20, na lingine lenye tani23 likachakatwe kwenye smelter ya nchi neutral kabisa ili kupata distribution ya madini yaliyopo,under Witness ya Mamlaka za Tanzania, ACACIA Representative na Mtu ambaye ni Msuluhishi.
 
In order to construct a viable smelter in Tanzania, it would require importing 60% of Copper Concentrate to feed the smelter, or Tanzania would have to increase its own production of Copper Concentrate through the development of more mines, and of similar production technology. However, there are currently no known copper sulphide deposits in Tanzania, which would add significantly to the Copper Concentrate requirements to feed the smelter to be constructed.

The study concludes that it is currently not feasible for a Copper Concentrate smelter to be constructed in the country to smelt and refine Copper Concentrate produced by BGM and BZGM. However, investors are encouraged to explore more on possibilities of discovering copper deposits which will warrant for installation of a Copper Concentrate smelter in the Country.

Source:
http://www.tmaa.go.tz/uploads/A_Stu...a_Copper_Concentrate_Smelter_in_Tanzania1.pdf
Tovuti ya hawa TMAA wala siyo source nzuri ya kufahamu ukweli kuhusu smelter. Maana nao hawa TMAA ni madalali wa hao mabepari
 
Hiyo ndio ile study iliyotudanganya.???
Ukipigia mahesabu ya smelter kwa ajili ya copper concentrate utakuja na majibu hayo ....Je ukipigia mahesabu kwa smelter ya "metal" smelter utakuja na conclusion gani?
Hivi katika ulimwengu wa leo hatuwezi kutengenezewa smelter ya kiwango cha 60000 tons za copper concentrate?

ndio maana hata TMAA ni sehemu ya tatizo ...kwa kukosa weledi na kwa kuhongwa.

Kwenye hiyo link uliyoiweka utaona rejea ya TMAA ni hao hao waongo wa BZG....What do you expect???
You are very right. TMAA walishakuwa maYuda (wasaliti) kitambo. Walianza kwenye kujenga hoja kwa kuweka ugumu wa sisi kuconstruct smelter ili ulaji huu uweze kuendelea.

Wanasema Smelter ni almost 1.2Trilion. Wkt Mali ya Jana tu ni zaid ya hiyo 1.2 Trillion Sasa kuna ugumu gani hapo wa kuwa na yetu?

Wanasema tutahitaji 1.53 megawatt kurun hiyo smelter kuchenjua cubic ton moja. Hii ni ngumu kumeza. Yani nguvu inayohtajika kwenye hiyo smelting ni zaid ya nguvu inayotumika pale Bulyanhulu? TMAA ni wezi tusirely on their information.
 
Mkuu na wewe unataka tuamini kuwa Uchenjuaji unafanyika ni kwa ajili ya 0•02 ya gold??au kwa ajili ya faida "nyeusi"??

Je wewe kama msomi wa nyanja hiyo uko tayari kuhoji huo mchanga unapoenda kuchenjuliwa kinachotoka mwishoni kina thamani gani??

Acacia na ninyi mna guts za kuonesha umma step by step and the final destination ya makanikia?

By the way who were the first proffesionals who performed the initial analysis and declered that it was just a copper concentrate with other cormecially invaluable metals???
0.02% gold ni kiasi kingi sana maana hiyo ni 200ppm (200g/ton). Bila kufanya concentration, hakuna mgodi hata mmoja nchini ambao una average grade ya kiasi hicho. Hicho ni kiwango ambacho kinakupa justification ya kusafirisha kama concentrate.

Kwa usahihi kabisa kinachosafirishwa ni gold- copper-silver concentrate. Kinachoenda kuwa recovered ni gold, copper and silver.

Makosa ni kuanza kutoa thamani ya elements zote zilizopo kwenye concentrate hata zile ambazo haziwezi kuwa recovered profitably. Sijawahi kusikia kampuni hata moja katika Dunia hii inayosafirisha concentrate kwaajili ya recovery ya chuma au sulphur. Chuma na sulphur vina very low unit price.

Kamati ilikuwa na uwezo wa kufuatilia hata huko Japan ili kujiridhisha na nini kinakuwa recovered kutoka kwenye concentrate.

Kuunda kamati ulikuwa ni uamuzi sahihi lakini kamati imeshindwa kufanya kazi kwa weledi.

Ingekuwa inawezekana, hiyo concentrate tusafirishe hata container moja tu sisi wenyewe kwa usimamizi wa wataalam wanakamati, ipelekwe mahali popote penye smelter, tukafanye recovery ya vyote vilivyotajwa. Halafu tuje tuelezwe ni nini kimepatikana.

Mpaka sasa katika ulimwengu huu, hakuna mgodi hata mmoja Duniani ambao umewahi au unatoa madini ya aina nyingi tena kwa faida, kama hiyo ripoti ilivyoonesha. Huenda huu utakuwa ugunduzi mpya uliofanywa na wataaam wa Tanzania.

Tunaotilia mashaka ripoti tunaonekana siyo wazalendo au tumehongwa lakini kuna siku moja tutaonekana kinyume chake. Nafarijika ninapotoa maoni yangu kwa uelewa wangu kwa kitu ambacho nina utaalam nacho kuliko kunyamaza au kubebwa na mkumbo hata pale ambapo hata ule uelewa wa kawaida unakataa.

Ningekuwa katika nafasi ya kushauri, ningemshauri Rais aitake kamati kufanya presentation ya findings zao kwa jopo la wataalam wa madini (mineral industrialists). Hawa watakuwa na uwezo wa kuhoji kila eneo lenye mashaka na kujiridhisha kama kweli utafiti unakidhi vigezo vya kufika tamati iliyofikiwa.
 
Una hoja lakini kuna kitu unakikwepa kama walivyofanya acacia na TMAA...Tume iliyataja baadhi ya madini iliyoyaita strategic na kusisitiza kuwa yamo kwenye hiyo copper concentrate na yamo katika kiasi murua kabisa cha kuweza kuingiza faida na kodi .kwenye post yangu ya kwanza nimetoa mfano wa rhodium(kama sijakosea jina) nikijaribu kukuonesha nayo ni sehemu significant ya metals inayopatikana kwenye hiyo concentrate.

Hoja ya mada hii ni kwamba acacia na TMAA waliamua tu kwa makusudi kuibatiza jina baya hiyo copper concentrate kumbe kuna madini ya ukweli yanayowapa faida pengine kubwa kuliko hiyo 0.02 ya gold.

Jibia hoja yangu mkuu...be honest ba uwe mzalendo....
 
Sina mashaka kabisa na uzalendo wangu. Sina maslahi ya namna yoyote na Acacia. Madini uliyoyataja ni PGEs (platinum group elements). Sielewi kwa nini kamati iliyataja kama strategic minerals. Katika hiyo group waliyataja rhodium na iridium. Hizi elements zina thamani lakini siyo kuizidi dhahabu. Hizi elements unaweza kufanya extraction zinapokuwa zimefikia ore grade. Hizi elements kwa hapa kwetu hakuna mgodi ambao zimefikia ore

Kitu kinacholeta mashaka ni kuwa hatujaona QAQC report ya analysis yao ambayo kwa kupitia hiyo report unaweza kuthibitisha perfection and accuracy ya lab (instruments and people). Instruments ili zitoe majibu sahihi, zinahitaji kufanyiwa configuration kwa kutumia control samples ambazo kwa kawaida huwa zimefanyiwa analysis na maabara siyo chini ya tatu zinazoaminika Duniani. Usipotumia hizi samples vifaa vyako vinaweza kusoma consistently high or low.

Zile values walizozisoma, kama ni za kweli basi migodi yetu hiyo ni World Class kwa kila aina ya madini waliyoyasoma, kitu ambacho siyo kweli.

Nashawishika sana kuamini kamati imepotoshwa na vipimo vya maabara na ndiyo maana ACACIA wanaonekana kuwa very confident. Wana uhakika samples hizo zikipelekwa maabara nyingine zitatoa majibu tofauti.
 
Sina mashaka kabisa na uzalendo wangu. Sina maslahi ya namna yoyote na Acacia. Madini uliyoyataja ni PGEs (platinum group elements). Sielewi kwa nini kamati iliyataja kama strategic minerals. Katika hiyo group waliyataja rhodium na iridium. Hizi elements zina thamani lakini siyo kuizidi dhahabu. Hizi elements unaweza kufanya extraction zinapokuwa zimefikia ore grade. Hizi elements kwa hapa kwetu hakuna mgodi ambao zimefikia ore

Kitu kinacholeta mashaka ni kuwa hatujaona QAQC report ya analysis yao ambayo kwa kupitia hiyo report unaweza kuthibitisha perfection and accuracy ya lab (instruments and people). Instruments ili zitoe majibu sahihi, zinahitaji kufanyiwa configuration kwa kutumia control samples ambazo kwa kawaida huwa zimefanyiwa analysis na maabara siyo chini ya tatu zinazoaminika Duniani. Usipotumia hizi samples vifaa vyako vinaweza kusoma consistently high or low.

Zile values walizozisoma, kama ni za kweli basi migodi yetu hiyo ni World Class kwa kila aina ya madini waliyoyasoma, kitu ambacho siyo kweli.

Nashawishika sana kuamini kamati imepotosha na vipimo vya maabara na ndiyo maana ACACIA wanaonekana kuwa very confident. Wana uhakika samples hizo zikipelekwa maabara nyingine zitatoa majibu tofauti.
Anayesema kwamba hizi element zimefikia kiwango cha ore grade ni nani?
kiwango cha ore grade ni kipi?
Hizo maabara za kimataifa unazoziamini zina sifa gani...na je sifa ya ufisadi unaicontrol vipi?
Je acacia hajafaidika na kiwango hiki ambacho umekiita sio ore grade??kama amefaidika je kodi yetu ililipwa?kama hajalipa kwa nini?

Uwepo wa hizo elements kwa kiwango ore grade ni kiasi gani kimataifa?

Mkuu karibu ufunguke.
 
Mkuu hapa tunajadili kilichopo kwenye mchanga.....sio mkataba wa kuuondosha nchini.

Hapa tunajadili kama kilichopo kwenye mchanga hakina thamani ya kuuzwa au la...yaani ukiondoa copper,gold na silver.
Mkuu mkataba ndio una majibu yote.Na ndio maana ACACIA kwenye taarifa yao wamesema wamekuwa wakilipa kiasi chote cha "commercial value" ya madini hayo.Sasa mkataba unasema "commercial value" ni kiasi gani?
 
Acacia wamesema...this reference is disgraceful!
 
Back
Top Bottom