Mchanga wa madini kuitwa copper concentrate ilikuwa ni hujuma ya kutuibia

Conclusion yao kwa nini ili-ignore fact kwamba kuna uwepo wa metals nyingine ...kwa nini haikueleza mustakabali wa metals nyingine??

Je TMAA walikuwa na utaalamu wa kiuchumi kuwa kwenye nafasi ya kuconclude kuwa na smelter haingekuwa na faida kwa uchumi ??
Kwa taarifa yako hata marekani mchanga wao wa copper concentrate unaenda kuchenjuliwa china. Rais anaamsha madude yenye utata ili msiwaze ahadi alizowahaidi. Endelea kusubiri smelter wakati bei za vitu zinapanda, dawa zinaadimika na thamani ya shilingi inashuka.
 
Kwa hiyo marekani ikiruhusu ushoga na Tanzania iruhusu ushoga...hii ni argument ya kitoto sana.

By the way hoja hapa hiko kinachotoka marekani kinaweza kuwa copper concentrate ya ukweli tofauti na hiki tunachoambiwa hapa kwetu kuwa ni copper concentrate.

Swali ambalo unatakiwa kulijibu ni kwa nini ACACIA anaignore uwepo wa hayo madini mengine eti kwa kiasi hayahusishwi kwenye biashara??
 
Tatizo hatupendi kusoma na kujielimisha na tunabaki kucomment kama vile sisi ndo wataalamu wabobezi. Wanaposema sio commercial valuable hawana maana kwamba hayana thamani sokoni, but kiasi kilichopo kwenye makinika (concentrate) ni kidogo sana kulinganisha na gharama za smelting cost. Naomba upitie hii attachment na uone kuwa TMAA, TRA na wizara wanahusishwa kwa kila hatua. So unataka kuwashtaki kwa kigezo gani? Sampuli zinachukuliwa na TMAA na ACACIA/SGS na kupimwa na matokeo hupewa kwa wadau wote wanaohusika (TMAA, TRA, ACACIA na smelter) ili kodi ilipwe kabla ya kusafirishwa. Kontena zinakuwa sealed mbele ya TMAA/Wizara, ACACIA, TRA na msafirishaji. Sasa wenyewe kwa kupenda rushwa tunawapa ACACIA mianya ya kuiba then leo tunakurupuka kama tumetoka dunia nyingine. Pole yetu
 
Attachments

  • mining-to-smelting-gold-copper-concentrates-detail-english_v2.pdf
    619.6 KB · Views: 34
Mkuu hapa tunajadili kilichopo kwenye mchanga.....sio mkataba wa kuuondosha nchini.Hapa tunajadili kama kilichopo kwenye mchanga hakina thamani ya kuuzwa au la...yaani ukiondoa copper,gold na silver.

Sasa si utuletee mkataba tujue nini kimo ndani yake? Vipi ikija kuthibitika kuwa kwenye mkataba tuliwakubalia haya yote wayafanye? Kumbuka uhusiano wetu na wao uko kimkataba na sio kwa mdomo tu.
 
Ni kweli kuna madini mengi katika viwango vidogovidogo, na ni hasara kununua mtambo wa kuyachenjua.
Tumsubiri magu anunue mtambo utakaogharimu bilioni kumi kwa mwezi ili kupata madini ya bilioni 2, maana sidhani kama tuna umeme utakaokidhi mahitaji ya smelter na treni ya sgr. Ameshakuwa na bashite brain huyu rais wetu.

Kwahiyo unahisi akili ya Magufuli na watu wake imeishia hapo ilipoishia yakwako?..Ila mzungu akikwambia nunueni smelter umeme utatosha utakubali tu..
 
Hii michezo inachezwa na watu wa serikali ya ccm sio kwamba hawajui na wahusika wanafahamika ni wakuu wa nchi, hivi haya mahotel makampuni ya simu yanayobadili majina kila siku simply wasilipe kodi kweli serikali ya magamba hajui, hata hii acacia yenyewe imecheza mchezo huohuo na kipindi chote hicho sizonje yupo kwenye hizi serikali.

Sasa acheni kufanya maigizo kwa kutoa watu kafara tu lakini mzizi wa tatizo liko palepale na hamligusi.

Kama sizonje ni mzalendo kweli alete katiba ya wananchi, maana katiba iliyopo watu wa aina sizonje wanajiona wako juu wa katiba na sheria.
Vinginevyo haya yanayofanyika ni maigizo ya kutafuta kiki na wakati huo mnaendelea na maandalizi ya kuiba kura, na sema hivi ni wajinga tu ndio mtawapata.
 
Ni kweli kuna madini mengi katika viwango vidogovidogo, na ni hasara kununua mtambo wa kuyachenjua.
Tumsubiri magu anunue mtambo utakaogharimu bilioni kumi kwa mwezi ili kupata madini ya bilioni 2, maana sidhani kama tuna umeme utakaokidhi mahitaji ya smelter na treni ya sgr. Ameshakuwa na bashite brain huyu rais wetu.
Kwa hyo wakipeleka huko wanapata hasara?
 
Mawe yote, mchanga na udongo ni madini. Jiwe, mchanga na udongo vimetengenezwa na madini. Madini hayo yanaweza kuwa na thamani au yasiwe na thamani. Uthamani unategemea unit price na kiasi. Dhahabu ina thamani lakini siyo kila dhahabu ni commercially viable.

Kuna parameters nyingi zinazoweza kufanya mineral kuwa commercially viable or not. Baadhi ni kama unit price, average grade, recovery which is subject to metallurgical peoperties, style of mineralization, tonnage, n.k.

Watu wasibishe bila hata ya kuelewa hata kile kinachoongelewa. Hata mawe tunayojengea yana chuma, sulphur, silica, Magnesium, manganese, calcium and some REE lakini quantities zake haziwezeshi kufanya extraction kwa faida.

Report ile ya Prof. Mruma is too good to be true. Kwa sababu inaonekana walifanya multielement analysis na baadaye kuifanya kila element ni extractable at a profit. Proffessionally I can urgue it did not meet professional standards, na hilo litatugharimu, ikiwa ni pamoja na kushusha professional credibility yao kwa Rais na nchi.

Unapofanya kazi ya kuaminiwa kama hiyo yenye maslahi kwa Taifa, inalazimu kuwa real professional kiasi kwamba una uhakika yeyote ambaye ni real professional akija kufanya hatapata matokeo tofauti kwa kiasi kikubwa.
 
Conclusion yao kwa nini ili-ignore fact kwamba kuna uwepo wa metals nyingine ...kwa nini haikueleza mustakabali wa metals nyingine??

Je TMAA walikuwa na utaalamu wa kiuchumi kuwa kwenye nafasi ya kuconclude kuwa na smelter haingekuwa na faida kwa uchumi ??
Ndo maana nilikuuliza ulisoma Ripoti ya TMAA au kwavile JPM kasema ndo basi tena?! Sehemu ya ile ripoti hivi ndivyo inavyosema:
Copper 01.png

Hapa tena wanaendelea:
Copper02.png

Kwahiyo badala ya kudanganya kwamba walikuwa wana-ignore uwepo wa metals zingine, hoja iwe kwanini hizo metals zingine other than gold, silve and copper zilikuwa zinafanywa mali ya smelters owners!!

Hapa chini wanaweka takwimu za major products:

Copper03.png

Halafu unahoji:
Je TMAA walikuwa na utaalamu wa kiuchumi kuwa kwenye nafasi ya kuconclude kuwa na smelter haingekuwa na faida kwa uchumi ??
Are you seriously asking this question?!

Wewe unadhani ordinary economist anaweza ku-evaluate viability of smelting plants?

Au hufahamu kwamba kuna kitu kinaitwa Mining Economics na hawa Mining Economists ndio wenye uwezo wa kufanya analysis kama hizo na sio ordinary economist ambae probably amebobea kwenye macro- or microeconomics, or Business Economics, or International Trade au hata labda Agricultral Economics!!!!!!

But NOTE, neno viable ukilileta kwenye Kiswahili moja kwa moja lazima utapotosha tu! Kwa mfano unasema: "...smelter haingekuwa na faida kwa uchumi!"

TMAA hawakusema kitu kama hicho kwenye ripoti yao yote! Title of Study ilikuwa: A Study on Viability to Construct a Copper Concentrate Smelter in Tanzania.

Descrption yake inasema:
This study was mainly focused on the determination of the viability of constructing a copper smelter in Tanzania so as to be used to process Copper Concentrate produced by BGM, BZGM and that to be produced by other mines in future.
Hakuna popote waliposema NOT PROFITABLE but not economically viable.

Tukichukua mfano huu huu wa copper concentrates tunaweza kuweka 2 alternatives ambapo miner atatakiwa kuchagua mojawapo!

Alternative 1; Miner anajenga smelter hapa hapa Tanzania. Akishafanya smelting na kutoa gharama zote, at the end anapata FAIDA, (say) ya $100 kwa kila tani moja.

Alternative 2 ni pale Miner anapoamua ku-export hiyo concentrates. Akitoa gharama zote through this process, let's anabaki na $105/ton.

Hapo Miner atakuambia it's not ECONOMICALLY VIABLE kujenga smelter Tanzania in exchange of exporting kwa sababu, hatua hiyo itamfanya apoteze $5 lakini sio kwamba atapata hasara!!!!

Remember, huyu ni mwekezaji ambae main goal ni ku-maximize profit! The guy has no interest na ajira ambazo zingepatikana kwa sababu, hizo ajira kwake ni additional COST!!!
 
Tatizo hatupendi kusoma na kujielimisha na tunabaki kucomment kama vile sisi ndo wataalamu wabobezi. Wanaposema sio commercial valuable hawana maana kwamba hayana thamani sokoni, but kiasi kilichopo kwenye makinika (concentrate) ni kidogo sana kulinganisha na gharama za smelting cost. Naomba upitie hii attachment na uone kuwa TMAA, TRA na wizara wanahusishwa kwa kila hatua. So unataka kuwashtaki kwa kigezo gani? Sampuli zinachukuliwa na TMAA na ACACIA/SGS na kupimwa na matokeo hupewa kwa wadau wote wanaohusika (TMAA, TRA, ACACIA na smelter) ili kodi ilipwe kabla ya kusafirishwa. Kontena zinakuwa sealed mbele ya TMAA/Wizara, ACACIA, TRA na msafirishaji. Sasa wenyewe kwa kupenda rushwa tunawapa ACACIA mianya ya kuiba then leo tunakurupuka kama tumetoka dunia nyingine. Pole yetu
Mkuu hebu rudia kusoma andiko la TMAA....kiufupi TMAA hawakufanya utafiti wowote lakini wakaja na taatifa kutoka chanzo kinachoitwa "WAMILIKI WA MGODI" Kama wewe unavyofanya.

Yaani wamiliki wa mgodi ndio walisema hiyo ni coppet concentrate na wamiliki hawa hawa wanatuambia metals nyingine zilizopo sio cormecially viable...

Pili ripoti ya prof Mruma inaonesha wazi uzembe au rushwa katika usimamizi wa TMAA ambayo inatoa ripoti tofauti na uhalisia yet unataka tukubaliane na hao wezi wa kitanzania na kigeni.!!

My point hebu jaribu kuingia kwa undani na kusaka articles mbalimbali kuhusu haya makanikia na uachane na ripoti ya TMAA ambayo ni echo ya ACACia ...tafuta ukweli. na hapo tutakuwa tumetendeana haki.
 
Huyu mkulu wetu hawezi kuunda tume halafu ikamwambia asichotaka kusikia. Baada ya uhakiki kwisha alikuwa anatafuta sababu nyingine ya kufanya tusimlaumu kwa kushindwa kutimiza ahadi. Anataka tumlaumu Prof. Muhongo. Mchanga "uliibiwa" miaka mingi na pesa za huduma za jamii zilikuwepo. Hakuna kitu kitafanyika kuhusu huo mchanga bali siasa tu apate makiki huku maisha yetu yakizidi kuwa duni mpaka 2020.
Bei ndogo ya smelter ni dola mil. 370,000. Nani atamkopesha pesa zote hizo wakati amewapa watu hasara soko la hisa la London? Madini ya kwenye makinikia ni machache kwa kuchenjulia nchini. Ni sawa na kununua photocopy machine kwa ajili ya kutoa kopi 20 kwa siku, bora ku-outsource.
 
Ni kweli kuna madini mengi katika viwango vidogovidogo, na ni hasara kununua mtambo wa kuyachenjua.
Tumsubiri magu anunue mtambo utakaogharimu bilioni kumi kwa mwezi ili kupata madini ya bilioni 2, maana sidhani kama tuna umeme utakaokidhi mahitaji ya smelter na treni ya sgr. Ameshakuwa na bashite brain huyu rais wetu.

Akili zakufuata mkumbo!!
Rais anajua nini anafanya
 
Hatuwezi kuwaamini ACACIA tena. Kila uchunguzi wanaoufanya lzm wataalamu wetu wa ndani wawepo. Naona kama tunajitoshereza sana ,angalau kutambua nini kipo kwenye Mchanga. Ni aibu kutegemea ripoti ya Uchungizi wao. Akili ya kawaida inasema lzm wataficha ili wafaidike zaidi na kukwepa kodi.
 
Mawe yote, mchanga na udongo ni madini. Jiwe, mchanga na udongo vimetengenezwa na madini. Madini hayo yanaweza kuwa na thamani au yasiwe na thamani. Uthamani unategemea unit price na kiasi. Dhahabu ina thamani lakini siyo kila dhahabu ni commercially viable.

Kuna parameters nyingi zinazoweza kufanya mineral kuwa commercially viable or not. Baadhi ni kama unit price, average grade, recovery which is subject to metallurgical peoperties, style of mineralization, tonnage, n.k.

Watu wasibishe bila hata ya kuelewa hata kile kinachoongelewa. Hata mawe tunayojengea yana chuma, sulphur, silica, Magnesium, manganese, calcium and some REE lakini quantities zake haziwezeshi kufanya extraction kwa faida.

Report ile ya Prof. Mruma is too good to be true. Kwa sababu inaonekana walifanya multielement analysis na baadaye kuifanya kila element ni extractable at a profit. Proffessionally I can urgue it did not meet professional standards, na hilo litatugharimu, ikiwa ni pamoja na kushusha professional credibility yao kwa Rais na nchi.

Unapofanya kazi ya kuaminiwa kama hiyo yenye maslahi kwa Taifa, inalazimu kuwa real professional kiasi kwamba una uhakika yeyote ambaye ni real professional akija kufanya hatapata matokeo tofauti kwa kiasi kikubwa.
Mkuu na wewe unataka tuamini kuwa Uchenjuaji unafanyika ni kwa ajili ya 0•02 ya gold??au kwa ajili ya faida "nyeusi"??

Je wewe kama msomi wa nyanja hiyo uko tayari kuhoji huo mchanga unapoenda kuchenjuliwa kinachotoka mwishoni kina thamani gani??

Acacia na ninyi mna guts za kuonesha umma step by step and the final destination ya makanikia?

By the way who were the first proffesionals who performed the initial analysis and declered that it was just a copper concentrate with other cormecially invaluable metals???
 
Hawa jamaa ni wajanja sana ingawa ni waongo na njia ya muongo ni fupi sana.

Nina uhakika kuwa kwa asilimia zaidi ya 100 kwamba wamiliki na wachimbaji tuliowakabidhi migodi yetu walijuwa fika kuwa hapo chini ya ardhi kuna aina gani za madini hata kabla ya kuanza kuchimba pia nina uhakika wakati wa mchakato wa uchimbaji makampuni haya yaliweza kugundua uwepo wa madini mengine ambayo ni wazi yanauzika kibiashara.

Ni aibu kwa Mchanga huu kuitwa copper concentrate na kuignore the fact kwamba kuna madini mengine muhimu na yenye uhitaji na bei nzuri tu huko duniani.

Mbaya zaidi hata sasa ACACIA wanataka kutuhadaa kuwa kilichopo kwenye hiyo copper concentrate hakina thamani ukiondoa copper, silver na gold.

Yaani ACACIA wanatufanya watoto wasiojielewa na wapuuzi wa hali ya juu.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa hata TMAA walishawahi kuufahamu uwepo wa madini hayo mengine ingawa walibakia kwenye kuamini ripoti za wenye makampuni kuwa mchanga huu ni copper concentrate tu.

Inakuwaje ACACIA waseme madini kama Rhodium (mtanisahihisha) yaliyokutwa kwenye mchanga wanaouita copper concentrate sio comercially valuable?

Kwa wenye kuchimba zaidi tufuatilie uhitaji na thamani ya haya madini kwa jina la madini ya kundi la platinum ambayo ACACIA walificha kuyataja na mpaka sasa hawataki kukubali kwamba yana thamani na yanatakiwa kulipiwa kodi.

Facts About Rhodium
Tatizo kubwa sana nchi hii ni kila mtu kujifanya anajua kila kitu....na wanasiasa ndio wanaongoza katika hili. Hebu tuchambue suala moja tu toka kwenye ripoti iliyokabidhiwa jana:
1. Tumeambiwa kuwa katika makontena hayo 277 kunasadikiwa kuwa na tani 7 mpaka 15 za dhahabu. Mimi nimeamua kuchukua hiki kiwango cha juu...yaani tani 15. Dhahabu hupimwa kwa ounces (wakia), na ounce 1 ni sawa na gramu 31.1035.

2. Tani 15 maana yake ni kilo 15,000 ambazo ni gramu 15,000,000. Hizi katika ounces ni 482, 260.

3. Bei ya sasa ya dhahabu ni dola 1,200 kwa ounce. Maana yake kama dhahabu yote hiyo ikifanikiwa kuwa extracted inaleta revenue ya dola 578,712,000 ambazo ni sawa na shilingi 1,273,166,400 (shs trilioni 1.27). Haya yatakuwa ndio mauzo ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa mwezi mmoja tu, tena hii ikiwa ni aslimia 30 tu ya mauzo yao kwa mwezi kwasababu asilimia 70 ya mauzo yao ya dhahabu yanafanyika kwa kuuza mikuo ya dhahabu wanayoibumba straight hapohapo migodini. Kwahiyo mauzo yao ya asilimia 100 kwa mwezi itakuwa kama shs trilioni 4.2.

4. Iwapo ni kweli kuwa tani 15 za dhahabu ziko kwenye hiyo asilimia 30 ya production yao, basi asilimia 100 ya production yao itakuwa ni tani 50 sawa na ounce 1,607,536 kwa mwezi. Kwa mwaka ina maana wana uwezo wa kuzalisha ounces kama milioni 19.

5. Migodi mingi inayofanya vizuri duniani kote kuweza kuzalisha ounce kati ya 75,000 na 100,000 kwa mwaka. Tulawaka Gold Mine katika uhai wake chini ya African Barrick Gold wa miaka 9 ulizalisha ounce 900,000 tu. Na huu unaingia kwenye historia kama moja ya migodi ya dhahabu Africa uliokuwa na deposit kubwa....ounce laki 9 zilizovunwa kwa miaka 9...yaani wastani wa ounce laki moja kwa mwaka.

Conclusion: Kuna walakini katika figures zilizotolewa kwenye ripoti. Hizo tani 15 ambazo ni ounce 482,260 ni production ya dhahabu ya miaka minne mpaka mitano kwa mgodi wenye gold concentration nzuri....unahitaji kuwa na grade ya 3 grams per tonne na uprocess tani kama 3,000 za kifusi madini ili upate walau ounce 8,000 kwa mwezi...sawa na kama ounce laki moja kwa mwaka. Hizo tani 15 yaani ounce 482,260 utazipata baada ya miaka minne. Na migodi yenye uwezo huo kwa sasa Tanzania ni mitatu tu...Geita, North Mara na Chunya.
Tupewe ripoti yote tuijadili.

NB: Kuhusu kwanini inaitwa copper concentrate...ni kwasababu copper ndio inakuwepo kwa wingi zaidi ya madini mengine yote. Acacia wao wameshatoa estimates zao kuwa kwa kila container kuna dhahabu around kilo 3 (yaani ounce kama 96), silver nayo 3kg na copper kama copper 3,000kg...hivyo copper ipo mara 500 as compared to other minerals. Kwa maneno mengine yale makontena yote 277 yana kama kilo 831 tu za dhahabu, haifiki hata tani moja...wakati ripoti inasema ni tani 15...yani zaidi kwa mara kumi.
 
Back
Top Bottom