mchanga (sand)

sky_haf

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
220
23
baadhi ya wakati tunapokula baadhi ya mboga huwa zimechanganyika na mchanga/udongo..hivi ni yepi madhara ya kula huu mchanga katika miili yetu??
 
Ndio maana inapaswa kuosha vizuri hizo mboga, pili labda inaweza kuleta minyoo
 
appendix,a small tissue attached to the end of a large intestine,ikijaa mchanga itabid ufanyiwe opperation.
 
baadhi ya wakati tunapokula baadhi ya mboga huwa zimechanganyika na mchanga/udongo..hivi ni yepi madhara ya kula huu mchanga katika miili yetu??

Mkuu, Mchanga si sehemu(ya chakula/virutubisho) vinavyohitajika mwilini na hivyo basi, uwepo wake katika mwili huweza kusababisha madhara mbali mbali..hii yaweza kuwa kwa wale binadamu wenye kutumia mchanga makusudi kama chakula(mf. watoto, wajawazito, baadhi ya magonjwa kama Pica) au kwa bahati mbaya kama ulivyosema katika baadhi ya vyakula wali, mboga n.k

Madhara hayo ni pamoja na haya;
-Kuharibu meno(hasa katika utafunaji)
-Mchanga unakwaruza/kwangua katika sehemu ya tumbo, utumbo n.k
-Magonjwa(tumbo, minyoo) hasa kutokana na wanyama tunaowafuga na wale wa porini kuweza kuacha vimelea, mayai katika udongo).
-Mwishoni, kuna tatizo linaloitwa Appendicitis, ambapo sehemu ile mchanga ulipokuwa ukihifadhiwa(ingawa hauhitajiki) kujaa/kujiviringa/n k kutokea.

Muhimu ni kuepuka kutumia mchanga/vitu vinavyofanana na hivyo mfano Chaki(Chalk), udongo kina mama wajawazito wanaoutumia wakati wa mimba "pemba", majivu, vipande vidogo vya miti(magome), n.k kwa njia ya

-Kuwachunga(kuwaangalia) watoto wadogo.
-Kusafisha vyakula vizuri na kwa umakini kama mboga za majani, mchele n.k
- Kuwasaidia wajawazito kutotumia udongo kwa mazoea.
-Kutafuta msaada wa kiafya hali inapozidi(kula udongo).
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom