Mchambuzi Mhando wa Gazeti la Rai yuko wapi? Anajua vema asili na madhara ya IPTL

osokoni8148

Member
Jan 13, 2014
69
46
Wana Jf, kwa wale wenye umri mkubwa kidogo mnaweza kunisaidia ni wapi ilipo mwandishi wa habari na mchambuzi ambaye miaka ya zamani kidogo, yaani mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya 2000 alimuwa akiandika na kufanya uchambuzi kwenye gazeti la Rai ambalo kwa wakati huo likuw limitoka kwa siku moja tu, siku ya alhamisi.

Mwandishi huyu namkumbuka kwa jina moja, Mhando (yawezekana nalo sijalitamka vizuri) na sikumbuki jina lake la pili.

Kilicbonisukuma kuleta ombi hi hapa jf ni kumbukumbu ya makala nzuri alizokuwa anaandika huyu mwandishi katika gazeti la Rai ambalo kwa wakati huo lilikuwa likigombaniwa sana na kuuzika mwa siku zote saba za juma japo lilikuwa linatoka mara moja tu kwa juma.

Mwandishi huyu ambaye mimi namchukulia kama mfano wa kuigwa na waandishi wengine, alikuwa ni researcher, investigative journalists na mtu makini anayeijua kazi yake.

Moja ya makala zake kwenye miaka ya mwanzoni mwa 2000 ni kuhusu jambo ambalo hivi sasa limeiweka Tanzania kuwa tete, IPTL. Mwandishi huyo wakati huo aliwahi kuandika kwa ufasaha na kuelezea mwanzo wa IPTL, mkataba wake ulivyokuwa wa kinyonyaji na kifisadi kwa Taifa, matokeo na athari za mkataba wa IPTL kwa nchi, pamoja na madhara ya mkataba huo kwa uchumi wa Tanzania kwani nakumbuka mwa wakati huo aliweza kuelezea kwamba Taifa kupitia Tanesco, lilikuwa likilipa zaidi ya shilingi milioni mia moja kwa IPTL kila siku iwe imezalisha umeme au haijazalizha kama capacity charges.

Sasa fikiria kwa wakati huo taifa linalipa milioni miamoja kwa siku na tena kwa siku nyingine umeme wa IPTL ulikuwa hautumiki, je ni kiasi gani cha fedha za walipa kodi kilikuwa minapotea bure kwa malipo ya mkataba huu wa kifisadi.

Naamini hili saga la sasa la ESCROW lisingekuwepo kama maandishi, ushauri na maono ya watu kama ndg. Mhando yangekuwa yanachukuliwa kwa umakini, umo wapi Mhando?

Natamani hiyo makara ningeipata iwekwe tena wazi kama rejea, lakini kama Mr. Mhando utanisikia, unaweza kuludia uchambuzi wako ili kukionyesha hiki kizazi kisichosikia asili na madhara ya IPTL.
 
Back
Top Bottom