Mchakato wa uteuzi wagombea ubunge wa EAC kupitia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchakato wa uteuzi wagombea ubunge wa EAC kupitia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Apr 7, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180


  TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA WAJUMBE WATAKAOIWAKILISHA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KUPITIA CHADEMA

  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa taarifa kwa umma kwamba uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kupitia CHADEMA umekamilika tarehe 6 Aprili 2012 saa 10 Jioni.

  Uteuzi wa mwisho wa wagombea utafanyika tarehe 9 Aprili 2012 siku ya jumatatu kuanzia saa 3 asubuhi ambapo wagombea wote waliorudisha fomu wametaarifiwa kufika kwenye mkutano husika.

  Wagombea waliorudisha fomu mpaka sasa ni pamoja na Godfrey Mnubi, Edgar William Chibura, John Simon Malanilo, Patrick Lubango Nkandi, Anna E. Maghwira, Deogratias George Assey, Pasquina Ferdinand Lucas, Deusdedit Jovin Kahangwa, Antony Calist Komu na Mwantum Khamis Mgonja.

  Ikumbukwe kuwa tarehe 12 Machi 2012 Katibu wa Bunge alitoa Taarifa kwa Umma kwamba,Uchaguzi wa wajumbe tisa (9) watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki utafanywa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wakati wa Mkutano wake wa Saba utakaofanyika Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 20 Aprili, 2012.

  Uchaguzi huo wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki unafanyika kwa kuzingatia kuwa maisha ya Bunge hilo lililoingia madarakani mwaka 2006 yatafikia ukomo wake 04 Juni, 2012.


  Taarifa imetolewa kwa vyombo vya habari na:
  John Mnyika
  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
  07/04/2012
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  Asante kwa taarifa, naomba mtoe watu makini.

  Nategemea wa kutusemea EAC kutoka huku wale wengine wamelamba makarasa tu.
   
 3. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  fomu mlianza kutoa lini? mbona mambio kimya kimy aau mimi ndip nilikuwa sina taarifa
   
 4. B

  Bubona JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Last paragraph, tarehe ya ukomo wa Bunge ni sahihi kweli?. I guess something is not right!
   
 5. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Bunge linalozungumziwa hapo si lile la JMT bali la EAC. Ni sahihi.
  @Bubona
   
 6. C

  Chokler Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninachokiamina akilini na nafsini mwangu ni kwamba CHADEMA ni chama makini huwamnafanya maamuzi yasiyo na majuto kwenu na kwa raia pia nawapongeza kwa hilo sasa ni imani yangu mtachagua wabunge wenye nafasi ya kuijua EAC atleast kwa karibu kama sio kwa undani sana "Put the right man at the right place".
   
 7. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Profesa Jumbe Safari hautaki ubunge huu?
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Uamuzi wake wa kuto kugombea ni sawa maana Chadema inahitaji kujengwa sasa mwacheni aendelee
   
 9. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Anne Mgwira hapa ndipo panapomfaa
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kazi nzuri mnyika!
   
 11. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  tuchague watu makini, tuijenge nchi yetu.
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh Mabere Nyaucho Marando hajajitokeza? Naona Komu naye ndani ya nyumba!
   
 13. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,811
  Likes Received: 17,912
  Trophy Points: 280
  wakuu nielewesheni kitu hapa, uchaguzi huu unakuwaje palebungeni, wagombea wote wa CCM&Upinzani hupigiwa kura pamoja?na kivipihakuna biasness kwa CCM dhidi ya candidates wa upinzani, nombeni msaada wakanuni
   
 14. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #14
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Tangu mwanzo mchakato ulikuwa ukiwekwa public kupitia vyombo vya habari. Ndiyo maana wagombea wengine walijitokeza mara baada ya kusoma katika vyombo vya habari.
   
 15. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #15
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Which is not right? Huo ndiyo muda wa ukomo kwa Bunge la EAC.
   
 16. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #16
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Kitu gani hakiko sahihi hapo mkuu? Huo ndiyo muda wa ukomo kwa Bunge la EAC. Usichanganye mambo mkuu.
   
 17. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kaka ni wewe tu haukubahatika kusikia kama uliweza kusikia hii ungeweza kusikia hata ila nyingine
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ungejua usemacho wala usingeandika hivi. Wanaochagua wabunge wa EAC ni bunge zima, sasa jiulize wengi ni wapi ndani ya bunge? Wanao amua hapa nani awe mbunge ni CCM
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mambo ya ajabu kabisa Chadema wanafanya uteuzi halafu CCM ndio wanawachagulia mbunge.
   
 20. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapo ndipo Cdm huwa wanawapigia magoti ccm kuwaonea huruma, si utaona mwenyewe
   
Loading...