Mchakato wa Sensa 2012 Tanzania waanza, Kaa tayari kuhesaniwa kwa manufaa ya nchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchakato wa Sensa 2012 Tanzania waanza, Kaa tayari kuhesaniwa kwa manufaa ya nchi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mathias Byabato, Jan 28, 2011.

 1. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 908
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Na Mwandishi wetu,Bukoba
  Mchakato wa kazi ya sense ya watu na makazi nchini umeanza rasmi katika ngazi ya mkoa wa Kagera ambapo wananchi wanaombwa kushiriki kikamilifu katika hatua zote za mchakato huo.
  Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw Mohamed Babu wakati wa kikao cha kwanza cha kamati ya Sensa ngazi ya Mkoa,ambapo sensa ya watu na makazi itafanyika nchi nzima mwezi August mwaka 2012.

  Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwamba zoezi hilo lina umhimu wa kipekee kwa wananchi kwani takwimu zitakazo patikana zitasaidia katika kutengeneza sera na mipango mbalimbali ya maendeleo na kutathimini uboreshaji wa maisha ya wananchi.

  Kuwa iwapo wananchi watashiriki kikamilifu katika sense hiyo taarifa zitakazotokana na sense hiyo ndizo zitakazotumika kutathimini na kubanisha hatua iliyofikiwa na Tanzania katika kutekeleza malengo ya mileninia ya mwaka 2015 na dira ya Taifa ya Mwaka 2025.

  Kwa upande wake Mratibu wa Sensa ngazi ya Mkoa Bw Peter Milinga amewaeleza wjumbe wa kamati hiyo kuwa maandalizi ya sense ya kitaifa yapo katika hatua za mwanzo za kutenga maeneo hivyo wananchi watoe ushirikiano kwa watendaji wa zoezi hilo na muda ukifika wawe tayari kuhesabiwa.

  Sensa ya watu wa makazi kwa nchini Tanzania hufanyika kila baada ya miaka kumi na kwa mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2002 na kuwa gharama zilizotengwa na Serikali katika zoezi hilo kitaifa katika awamu hii ni shilingi bilioni 113.7.


  Chanzo:Blog
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Haya...pa kuchota pesa pengine hapooo!
  Sensa yenyewe tunahesabiwa kama default system, lakini sijaona impact yake!
  Mi nashauri ifanyike sensa ya Dar-Es-Salaam peke yake ili waweze kupanua miundombinu ya pale!
  Barabara ni kifo
  Sewerage systems ni balaa
  Shule za aina zote ni kimbembe..
  Je wakuu hawa wanajua inflow-rate ya watu kuingia Dar?

  Huku mikoani watapoteza muda bure, maana hakuna jipya linalofanyika.
  Viwanja vya Arusha wanagawiwa akina RIZ1 na akina Nyalandu..this is fukcin!
   
 3. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 908
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45

  Mkuu pj
  Mbona kuna mahitaji mengi ya kufanyika kwa sensa tofauti na uliyotaja? Kikubwa ni kuwa utaratibu unaotumika unaweza kuwa siyo mzuri lakini hii ni ka sababu ya sera iliyopo
   
Loading...