Mchakato wa kuwatoa Masheikh na Waislamu magerezani

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
1,195
590
Asalamaleykum,

Nashauri Waislamu kwa umoja wao na wote wapenda haki dunia nzima kuanza mchakato wa kushinikiza Serikali ya Tanzania na Zanzibar kuwatoa waislamu walioko magerezani. Tunajua masheikh kama wa UAMSHO wako ndani kwa sababu zisizoeleweka/kisiasa zaidi.

Mchakato huu utakuwa na mipango ya hatua ya umoja kama waislamu na kuna mambo mengi yanaweza kufanywa na individuals yaani katika hatua ya mtu binafsi (mifano itafuata hapo chini). Tupange maandamano na kuwasilisha malalamiko yetu kwenye wizara za mambo ya nchi za nje siku ya ramadhan ya mwanzo ya 2021 inshallah kwa njia mtu binafsi kufika ofisini na kuwasilisha kwa barua. Hususan nchi za kiislamu, lakini hata za kimagharibi wanafahamu umuhimu wa haki za binadamu.

Hatua za kuchukuliwa na mtu kibinafsi:
  • Kususa kununua bidhaa yoyote itokayo Tanzania katika hatua ya vyakula kama kahawa, chai, chocolate, korosho n.k
  • Kususa kupanda vyombo vya usafiri vya serikali kama ndege za serikali.
  • Kususa kutumia mawasiliano mitandao ya kiserekali.
  • Kususa kwenda matembezi TZ kwa mapumziko na kuchagua nchi zengine (hususan diaspora)
  • Kususa kutuma pesa kwa njia za benki na badala yake kutumia njia za mashirika mengine kama western union (hususan diaspora)
  • Kususa kwenda hospitali za serekali
  • Kususa kupeleka watoto wapya maskuli ya serikali na kutumia ya watu binafsi
Na mambo mengi ambayo waislamu wataweza kuyafikiria inshallah Iddi-el-fitri masheikh wetu na waislamu wote kwa uwezo wake Allah (SW) watakula na familia zao. Ameen.

Maasalaam.
 
Tunahitaji watu wa kujitolea katika nyanja zifuatazo kwa mfano:
  • Kudraft barua ya kuwasilishwa
  • Volunteers wa kuwasilisha barua katika nchi walizoko pamoja kwa njia ya maandamano. Kwa TZ nashauri kutokufanya maandamano badala yake ni kuwasilisha barua kwenye balozi. Not so sure about this, lakini definately sishauri maandamano yasiyo na kibali.
 
Nadhan ingekua vizuri mkaishinikiza BAKWATA yenyew ndo ikawasiliana Na serikali.am not a moslem ila kumfunga mtu bila hukum sio HAKI.

Kwa waislam,Tumieni njia za amani kuwatoa,mkitumia njia zingine mtaungana nao

Kwa serikali,Masheikh kama wanakesi wahukumiwe kama hawana wawe huru.

Kwa watu wote,hili sio la waislam tu.ni letu sote.HAKI HAINA DINI.
 
Baada ya TL kukwama kuwa Rais....kuna jambo haliko sawa kwa mashekhe hawa. Kwanini wanaendelea kuzuiliwa ndani? Maana tusijidanganye kwamba tunaweza kufanya kitu chochote cha kuvunja sheria na tusiguswe. Hilo halipo popote pale duniani.
Nauliza tena, hawa mashekhe walifanya nini?
 
Kamanda Asiyechoka kabombe
Sitajibu maoni kama hayo yenu maana mchakato kama nilivyoeleza awali si wa kulazimishana ni wa hiari. Huu ni mchakato wa kiislamu, nadhani kiislamu kuwa stuborn kwa serekali haikubaliki. Kwa hio maandamano ambayo polisi na watawala wa TZ hawayataki nasi pia hatutoyafanya. Haina maana kama tunafurahia wanachokifanya, bali tunajaribu kuja na mawazo ambayo tutaweza kuwasilisha maoni yetu kwa njia zengine.
 
Nitaanza na jumuiya za wazanzibari waliko UK/ZAWA na CANADA, tafadhali wataarifu waislamu wote kwa kadiri utakavyoweza.
Wakisusa sie twala.

Mimi ni mkristu ila siungi mkono masheikh kuendelea kukaa jela bila kuhukumiwa. Serikali ya Magufuli iwaachie tu kama ilivyomwachia Babu Seya.

Ila na hao masheikh wajirekebishe tofauti zao za kutaka kutumia nguvu kila sehemu kwa kuhamasisha uasi na kutaka kutugawa.

Kafiri Hapa!
 
Baada ya TL kukwama kuwa Rais....kuna jambo haliko sawa kwa mashekhe hawa. Kwanini wanaendelea kuzuiliwa ndani? Maana tusijidanganye kwamba tunaweza kufanya kitu chochote cha kuvunja sheria na tusiguswe. Hilo halipo popote pale duniani.
Nauliza tena, hawa mashekhe walifanya nini?
Haifahamiki vizuri, masheikh kama wa UAMSHO walikuwa wanafanya mihadhara ya kuelezea muungano. Wakapandikiwa kesi za ugaidi wasipate dhamana na wako jela miaka haipunguwi 7.
 
Nadhan ingekua vizuri mkaishinikiza BAKWATA yenyew ndo ikawasiliana Na serikali.am not a moslem ila kumfunga mtu bila hukum sio HAKI.

Kwa waislam,Tumieni njia za amani kuwatoa,mkitumia njia zingine mtaungana nao

Kwa serikali,Masheikh kama wanakesi wahukumiwe kama hawana wawe huru.

Kwa watu wote,hili sio la waislam tu.ni letu sote.HAKI HAINA DINI.
Wewe hujui kuwa Bakwata ni jumuia ya CCM!
 
Nadhan ingekua vizuri mkaishinikiza BAKWATA yenyew ndo ikawasiliana Na serikali.am not a moslem ila kumfunga mtu bila hukum sio HAKI.

Kwa waislam,Tumieni njia za amani kuwatoa,mkitumia njia zingine mtaungana nao

Kwa serikali,Masheikh kama wanakesi wahukumiwe kama hawana wawe huru.

Kwa watu wote,hili sio la waislam tu.ni letu sote.HAKI HAINA DINI.
Hizo alotaja ni za shari?
 
Bakwata sio wawakilishi wa waislamu, bali ni taasisi ya serikali ya kutawalia waisilamu.
 
Back
Top Bottom