Mchakato wa kuwania urais ndani ya CCM mwaka 1995 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchakato wa kuwania urais ndani ya CCM mwaka 1995

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungi, Oct 10, 2009.

 1. Sungi

  Sungi Senior Member

  #1
  Oct 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakubwa - hivi wangapi mnakumbuka majina ya wagombea wa urais kupitia CCM mwaka 1995 kwenye round ya kwanza? Nakumbuka walikuwa wanne, Msuya, Mkapa, Kikwete na nimesahau wanne, kabla ya mchujo walipobaki Kikwete, Mkapa na Msuya. Ninaandika paper fulani hapa na ningependa kukumbushwa.

  Asanteni
   
 2. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mkuu heshima mbele kwa kujaribu kutoa mchango wako kwa kuweka historia mahali pake. Lakini nina wasi wasi na kitu unachotaka kuandika kuwa kinaweza kikapindisha hiyo historia kutokana na lugha ilivyokaa kwenye hili bandiko lako.

  kwanza sio kweli kuwa round ya kwanza ilikuwa na wagombea wanne, sijui unaposema round ya kwanza unamaanisha katika hatua/kikao kipi.

  kwasababu waliochukua form na kizirejesha walikuwa wana CCM 17 hapo mimi ndio napaona ndio pa kupaita round ya kwanza, kati ya hao alikuwepo mwanamke 1, baada ya kikao cha kamati kuu wagombea wawili majina yao yaliondolewa kwa kukosa kutimiza msharti, yakabaki majina 15 ambayo hayo yalipelekwa NEC. Na baada ya hapo mchujo uliendela hatimaye ngazi ya Mkutano mkuu wa Taifa.

  Ninachojua round zilikuwa kama ifuatavyo. 17 -15-10-5-3-2-1
  Kwa hiyo katika 3 bora walikuwepo Msuya, Ben na JK round ya kwanza ya tatu Bora aliongoza JK na msuya alikuwa wa mwisho, kwa vile JK hakupata zaidi ya 50% ya kura zote ilibidi uchaguzi urudiwe kwa kumuondoa mjumbe liyekuwa ameshika nafasi ya 3 Mzee Msuya. JK alikuwa akiungwa mkono na kundi kubwa la vijana (ambao awali walikuwa wamegawanyika kambi 2 moja ya JK na nyingine ya EL lakini baada ya jina la EL kuondolewa kwenye NEC vijana waliomuunga mkono EL walihamia kwa JK) EL ndiye aliyempa Lift ya ndege ya kukodi JK kukusanya sahihi 1000 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani ya wanachama wa kumdhamini kugombea Urais, na Msuya alikuwa chaguo la wazee, kwa kumuondoa Msuya wazee waliokuwa wanamuunga mkono walihamia kwa Ben ambaye alionekana anaendana na sera zao kiasi ukilinganisha na JK na pia walimuona amekomaa na inaonekana KNM wa kivinje alishawanong'oneza wanakamati kuwa JKN anamtaka BWM.
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huo mchakato siwezi kuusahau hasa pale watanzania tulpoona na kushuhudia role ya mwalimu katika siasa za nchi hii, big up mwalimu!
   
 4. p

  p53 JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nalikumbuka jina la John Samuel Malecela aka Tingatinga ambaye this time Mwalimu mwenyewe alipiga chini!
  Wakuu hivi ile ya Kikwete kutofikisha asilimia zaidi ya 50 ya kura ilikuwepo kwenye katiba ya CCM au lilikuwa ni zengwe tu la Nyerere?
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nyerere alifanya janja moja ambayo baadhi ya watu wanaamini ilimsaidia Mkapa kupita. Baada ya kupigwa kwa kura, Nyerere alikataa kutaja kura za kila mtu na badala walitaja tu Msuya kushika nafasi ya tatu na hivyo kutolewa.

  Ni kawaida kwa mwanadamu kwenda upande wa mshindi, kuna watu wanaamini laiti kura zote zingetajwa kama ilivyo kawaida, huenda watu wengi kutoka kambi ya Msuya wangemuunga mkono JK kwenye round ya mwisho.

  Pia kulikuwa na kundi la Wazanzibar ambalo lilimwunga mkono Msuya na kuwa na makubaliano kwamba Omar Juma angelikuwa makamu wa rais. Baada ya Msuya kutolewa, kundi la Mkapa liliwafuata Wazanzibari na kuahidi kumteua Omar Juma kuwa makamu wa rais. Kundi zima la Zanzibar likahamia kwa Mkapa.

  JK kutokufikisha asilimia 50 ilikuwepo kwenye katiba na bado ipo. Mwaka 2005 JK alipita 50% kwenye round ya kwanza hivyo hakukuwa na haja ya kubakiza wagombea wawili.
   
 6. p

  p53 JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35


  asante sana mkuu.umeniondolea dukuduku nililokuwa nalo kwa muda mrefu
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,070
  Trophy Points: 280
  Mtanzania,

  ..kambi ya JK na ile ya Msuya zilikuwa haziivi.

  ..JK alikuwa na malalamiko kwamba, Dr.Lawrence Gama, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, alikuwa akipiga kampeni kwa ajili ya Msuya.

  ..kilifanyika kikao cha "usuluhishi" ambacho habari zake nakumbuka ziliandikwa na gazeti la Rai. sina hakika kikao hicho kiliongozwa na nani lakini nadhani Dr.Gama hakuwa na wakati mzuri.

  ..kuna wanaodai kwamba Mkapa alifaidika na ugomvi kati ya kambi ya JK na ile ya Msuya. ukiangalia mgawanyo wa kura za raundi ya kwanza na ya pili, utaona karibia kura zote alizopata Cleopa Msuya ktk raundi ya kwanza zilihamia kwa Mkapa ktk raundi ya pili alipobakia na JK.

  ..kwa upande mwingine hotuba za Mzee Mwinyi na Mwalimu Nyerere zilikuwa ni kama maelekezo kwamba kura ziende kwa JK na Mkapa na siyo Cleopa Msuya.

  ..Mwinyi aliwaasa wajumbe wampigie kura mgombea anayetajwa vizuri Watanzania wenzao walioko nje ya mkutano. sasa hiyo ilikuwa ni kama maelekezo kwamba wampigie kura JK ambaye alikuwa akiandikwa vizuri na magazeti.

  ..Mwalimu aliwaasa wajumbe wampigie kura mgombea ambaye wana uhakika atapiga vita rushwa, ukabila, na udini. hotuba ya Mwalimu ilikuwa kama maelekezo kwamba wajumbe wasimpigie kura Cleopa Msuya ambaye wakati wote amekuwa akituhumiwa kwa rushwa na ukabila. suala la udini sina uhakika kama lilikuwa ni dongo dhidi ya JK kwasababu wakati huo alikuwa hana tuhuma zozote zile za udini.
   
 8. p

  p53 JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hawa makatibu wakuu wawili wa CCM wamepata dhahma baada ya mchujo wa wagombea urais katika chama chao kwavile washindi wamekuwa wale ambao hawakuwa chaguo lao
  Mangula nasikia nae alikuwa na mtu wake ndiyo maana alimuandikia ripoti mbovu Kikwete.Huyo mtu wake alikuwa nani?
   
 9. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Asante na vile nimepata mwanga juu ya hilo . Nilikuwa gizani juu ya hilo . honger a wana Jk.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni hatua hiyo hiyo imefuatwa mwaka 2005.. Waliochukua form na kuondolewa ktk hatua ya kwanza inaonyesha hawahesabiki ila wale waliobakia na kupigiwa kura.. Malecela aliondolewa mapema lakini waulize wenyewe watasema ati alipigwa chini ktk kura wakati Mkapa alimwengua kiroho mbaya kabla hata ya upigaji kura!
   
Loading...