Mchakato wa kuondoa umiliki wa hisa 51% za UDA kwa kampuni ya Simoni Group waanza

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,694
239,259
Taratibu za kuondoa uhalali wa umiliki wa hisa 51% za kampuni ya Simon Group ilizokuwa ikimiliki katika Shirika la Usafirishaji la Dar es Salaam (UDA) , zimekamilika.

Hayo yamebainishwa na msemaji wa Halmashauri ya Jiji la DSM , Gaston Makwembe , amesema kinachofanyika sasa ni kutoa taarifa rasmi kwa Msajili wa hazina ambaye ni mwanahisa wa shirika hilo, ili arejeshe mali na vifaa vingine vinavyopaswa kuwa mikononi mwa jiji .

Makwembe amesema taarifa iliyopelekwa kwa Msajili wa Hazina inaelezea MAAZIMIO YALIYOFIKIWA NA BARAZA LA MADIWANI YA KUTOTAMBUA MKATABA ULIOINGIWA NA MEYA ALIYEPITA , DIDAS MASABURI KUUZA HISA 51% ZA UDA KWA KAMPUNI YA SIMON GROUP KUTOKANA NA KUTOFUATA TARATIBU.

chanzo - Mwanahalisi.
 
Sasa wajiandae na evidence na mawakili wazuri wenye akili kueteta mali za Umma............Nilitarajia Makonda ajumuike nao lakini kwa vile ni wale wale wanaojidai kumsaidia Rais kumbe wanaagenda zao za siri......................
 
Nawashauri Simon Group wakubali bila mizengwe ili kulinda heshima ndogo sana iliyobaki ya kampuni yao , wakithubutu kwenda mahakamani watadhalilika kwa kiwango cha kutisha mno ! mengine mengi mno yatafumuka na majina kadhaa yatatajwa , hakuna haja .
 
Kama wakikubali kufanya hivyo.............Na hapa Mzee wa Kukurupuka akiiona lazima atainyaka tu
 
mwenyekiti wa CCM na familia yake watapambana hapa
48460-140.jpg

swissme
 
Back
Top Bottom