Mchakato wa kumwondolea Mkapa Mafao ya Rais mstaafu

MpigaFilimbi

JF-Expert Member
Apr 30, 2008
1,169
182
Wakuu,
Mkapa kama Rais mstaafu anaishi kwa kodi zetu sisi 'sons and daughters of the soil' bila kujali tunatoka chama gani. Wakati tukitegemea yeye kuwa mshauri wa masuala yanayohusu mustakabali wa kuendesha nchi, yeye anajikita kwenye kudharau wale wote wanaohoji mambo halali juu ya namna hii nchi inavyoendeshwa. Mafao ya viongozi wakuu wastaafu naona yanatumika vibaya. Kwa kuwa Mkapa bado yuko kwenye 'active politics' tena za kutetea uovu, ni wakati mwafaka tuanzishe mchakato wa kisheria wa kumwondolea mafao, kwani anaweza akalipwa kwenye siasa za CCM.

Mwongozo tafadhali...
 
Kuna haja ya kuangalia upya (kisheria) utaratibu wa kuwaangalia viongozi wastaafu na pia kutamka bayana defination ya ustaafu. Mtu hawezi kula mafao ya kustaafu wakati huo huo yuko kwenye active position. Kwa mfano tuna mawaziri wakuu walio kwenye active politics, tunao Speakers (Msekwa na Sitta) wastaafu lakini bado wako kwenye active politics. Je watu hawa wanalipwa mafao yao ya kustaafu wakati huo huo wanachukua mishahara ya nafasi zao mpya?
 
aina gani za soil kuna aina tatu embu wenye kumbukumbu watuelezee pengine we unaendika uko kwenye aina ya nafuu mpwa hukuw wengine kijijini wanateseka anyway ujumbe umefika tutaliangalia hilo kichamaaa

tehteeehhhhteehhh
Hii siyo issue ya chama, ni suala la sisi wenye nchi kuangalia namna gani kodi zetu zinatumika. Hatuwezi kuwalipia watu kama hawa wanaoenda majukwaani kutukana na kutetea uongozi mbovu. Ifike mahali tuangalie ukweli. Rais mstaafu angefaa kuwa mshauri na siyo chanzo cha kibri na kebehi ambazo hazina mpango, hasa kwa wananchi wanaohoji mambo halali. Tuache utani katika hili!!
 
Kuna haja ya kuangalia upya (kisheria) utaratibu wa kuwaangalia viongozi wastaafu na pia kutamka bayana defination ya ustaafu. Mtu hawezi kula mafao ya kustaafu wakati huo huo yuko kwenye active position. Kwa mfano tuna mawaziri wakuu walio kwenye active politics, tunao Speakers (Msekwa na Sitta) wastaafu lakini bado wako kwenye active politics. Je watu hawa wanalipwa mafao yao ya kustaafu wakati huo huo wanachukua mishahara ya nafasi zao mpya?
...usishangae Lowasa na wizi wake wote, analipwa mafao kama PM mstaafu, kama mbunge na bado anakula kutokana na miradi yake yote ya wizi. Mtu akistaafu asibaki kwenye active politics, akitaka kurudi aondolewe mafao.
 
Hii siyo issue ya chama, ni suala la sisi wenye nchi kuangalia namna gani kodi zetu zinatumika. Hatuwezi kuwalipia watu kama hawa wanaoenda majukwaani kutukana na kutetea uongozi mbovu. Ifike mahali tuangalie ukweli. Rais mstaafu angefaa kuwa mshauri na siyo chanzo cha kibri na kebehi ambazo hazina mpango, hasa kwa wananchi wanaohoji mambo halali. Tuache utani katika hili!!
Haya ndiyo mambo ya kuangalia kwenye katiba mpya. Tujiwekee utaratibu wa jinsi wastaafu watakavyokuwa wakitumika kwa manufaa ya nchi.

Pamoja na hayo ni kwamba kilichompata Mr. Ben ni fundisho kwa wazee wetu wastaafu. Nadhani wengi tunakubali kwamba Ben alijitahidi katika uongozi wake pamoja na mapungufu yake lakini hili la kuwa kwenye active politics linamong'onyoa heshima yake mbele ya wale waliokuwa na imani naye.

Pamoja na hayo hili ni fundisho kwa wastaafu wetu. Nina hakika hawa wastaafu wwkiombwa tena na CCM kuifanyia kampeni watakuwa wakijiuliza mara mbilimbili wakirejea yaliyompata Mr. Ben. Sioni wakijihusisha na siasa za majukwaani kwa urahisi tena.
 
Naunga mkono hii hoja. Iangaliwe namna bora ya kuiwasilisha katika channel sahihi halafu isonge mbele.
 
watoto wa wezi utajua tu jibu anavyojibu hoja kwa kukatisha tamaa watu wenye points, lakini hii haishangazi kwani aitukane CCM akale wapi? na hapa wamejaa weka mbelembele kutoa maoni upuuzi. sijui kwanini asianzishe blog ya kusuport CCM? anyway majority wanaanza kuona mwanga mpaka tuwe huru tena na nyang'au hawa weusi. mapambano yanaendelea.
 
Mkapa si wa kukatiwa hiyo pension na hayo malupulupu tu bali ni wa kupelekwa Segerea kunyea debe. Ufisadi mkubwa na wa waziwazi umechipuka katika awamu yake.
 
aina gani za soil kuna aina tatu embu wenye kumbukumbu watuelezee pengine we unaendika uko kwenye aina ya nafuu mpwa hukuw wengine kijijini wanateseka anyway ujumbe umefika tutaliangalia hilo kichamaaa

tehteeehhhhteehhh

tofautisha jukwaa la chit-chat na hili. Soil ina maana zaidi ya moja; hapa jamaa ana maanisha a 'country'.
 
Ukweli hili suala lazima liwekwe kwenye katiba mpya. Ndio maana juzi juzi CFD mstaafu Jenerali Mboma alitaka kuingia kwenye siasa kugombea Ubunge, ni aibu hii. Viongozi wakuu wakistaafu wanatakiwa watulie wakila mafao yao ya ustaafu na kazi yao kuu iwe ni ushauri tu kwa serikali na nchi kwa ujumla. Mkapa kajiabisha sana, hana tofauti na Lucy Nde... Kudadadekii
 
Naomba kwahili tuwadharau hawa watu (Magamba) muda si mrefu mwana wa Adam atakapokuja kuteua watu wake kutoka mikononi mwa hawa mafisadi ndipo wengine watalia na kusaga Meno
 
Pelekeni hoja ya dharula bungeni kuhusu mafao ya viongozi wastaafu ili mambo haya yajadiliwe kwa kina, kungoja mpaka katiba mpya iandikwe ni muda mrefu sana!
 
Nilikuwa ninamuheshimu sana Mkapa. Hasa kutokana na mafanikio yake ya kiuchumi; kwenye kufufua sekta ya migodi na kuiondoa serikali kwenye kufanya biashara.

Hauwezi amini kuwa nilimsifu hata hatua yake ya kuuza nyumba za serikali zilizokuwa zinakula kodi kuzitunza huku zikiozea chini. Kumbuka kuwa ukarabati wa nyumba kwa bei za serikali si mchezo - mfano 2Billion kurekebisha nyumba ya gavana wa BOT.

Lakini baada ya 2010, Igunga na sasa Arumeru, ninasikitika kuwa nimempunguza thamani huyu Rais wetu mstaafu.
 
Si ndio maana hata katiba wanaiwekea mizengwe? Wanajua ikiiachiwa iandikwe upya kabisa kwa mtazamo wananchi wanaoutaka kikwelikweli itakula kwao. Ndio maana mtu akimaliza uwaziri mkuu, urais, unaibu rais, wanakuwa wakali kweli ukigusa maeneo yao. Hawajui umasikini unafananaje.

Wao walizaliwa kwa ajili ya kula nchi tu. Matusi yote na kiburi majukwaani ni kwa sababu wanajua sheria walizozichakachua zinawalinda milele.

Kweli mchakato bora ni kuchomekea kwenye katiba mpya na halafu ccm na mbegu zao chafu waondoke kwenye hatamu wakati katiba hiyo inaanza kufanya kazi.

Wakirudi baadaye potelea mbali watakuwa wameonyeshwa namna ya kuendesha nchi. Tanzania tajiri sana bwana. Wanafaidi wachache. Kutokuwa na mafuta sio tija. Mungu alichotupatia mbona tunawafaidisha wahuni wa nje na ndani na sio wenye haki?
 
Alipoapa, aliapa kuwatumikia Watanz wote, ametumikia na amestaafu huku akiendelea kulipwa na watz wote. Hivyo basi, akubali kuendelea kutumika kwa wote kama anapenda alipwe na wote otherwise iwekwe wazi kwamba viongozi wakuu wakitaka kuendelea kutumika basi vyama vyao vibebe jukumu la ustaafu wao. Mbona akina Warioba, Sumaye, Mwinyi wametulia? Mkapa Ben is doing what a stupid mind is expected to do. Katiba mpya kwa ukombozi.
 
naunga hoja mkono. Hawa wastaafu sijajua kwa nn wanakuwa na viherehere.
 
Hoja ni nzuri,naomba waheshimiwa waichukulie hii kama hoja binafsi ili tuwajue wastaafu halali wanaokula mafao yetu huku wakiendelea kujihusisha na vyama vyao hata kwenye campaign
Naunga mkono hoja asilimia mia
 
Back
Top Bottom