Mchakato wa kumkabidhi Magufuli CCM waanza

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatarajiwa kukutana kesho mjini Dodoma,
chanzo cha kuaminika kimelidokeza kuwa pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitajadili maandalizi ya mkutano mkuu maalumu, ambao unatarajiwa kufanyika Juni mjini hapa.

Kwamba katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ataachia ngazi na kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli kama utamaduni wa chama hicho ulivyo katika kukabidhiana kijiti cha uongozi.

Tangu wiki iliyopita vikao kadhaa vya Sekretarieti vimekuwa vikiendelea mjini Dodoma, vikiwahusisha watendaji wa juu wa CCM pamoja na makatibu wa idara husika ambao huteuliwa na mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Kikao hicho cha kesho pia kinatarajiwa kuhudhuriwa na Rais Magufuli, ambaye tayari yupo Dodoma alipokuja kwa ajili ya sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi – Mei Mosi.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa nao wataungana na viongozi wa ngazi za juu wa CCM katika kikao hicho.

Katika kikao cha kesho, Kamati Kuu pia itajadili na kupitisha majina ya wajumbe 10 wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kutoka miongoni mwa wabunge wa CCM.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zilieleza kuwa kikao hicho kitakuwa chini ya Mwenyekiti wake Kikwete, ambapo wabunge walioomba nafasi hizo, majina yao yatapelekwa kwa wabunge wa chama hicho kwa ajili ya kupigiwa kura.

“Wabunge wana nafasi 10 za NEC na unajua waliokuwa wajumbe walishapoteza sifa za kuwa wajumbe, hivyo kwa kawaida kila Bunge jipya linapochaguliwa ni lazima uchaguzi ufanyike.

“Pamoja na kupitia majina ya wabunge waliojaza fomu, pia CC itajadili majina ya wabunge walioomba nafasi ya katibu wa wabunge wa CCM ambapo kuna wajumbe zaidi ya watatu wamejaza fomu,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, miongoni mwa wabunge wanaotajwa kuwania nafasi ya katibu wa wabunge wa CCM yumo Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda, ingawa wapo wabunge wengine ambao kwa pamoja watachujwa na kikao cha kesho.

Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM anayemaliza muda wake ni Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama.

Chanzo: Mtanzania
 
Sasa magufuli anajuta kuwa rais bado wanataka kumbebesha zigo lingine la uenyekiti wa ccm.mhurumieni jamani maana alishasema yeye si mwanasiasa mzuri.
Huko CCM ndipo kuna kisima cha uozo wa hii nchi.

Akikabidhiwa akapashughulikia vizuri, itampa unafuu mkubwa sana wa kuendesha serikali yake
 
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatarajiwa kukutana kesho mjini hapa, MTANZANIA limeelezwa.

Chanzo cha kuaminika kimelidokeza gazeti hili kuwa pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitajadili maandalizi ya mkutano mkuu maalumu, ambao unatarajiwa kufanyika Juni mjini hapa.

Kwamba katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ataachia ngazi na kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli kama utamaduni wa chama hicho ulivyo katika kukabidhiana kijiti cha uongozi.

Tangu wiki iliyopita vikao kadhaa vya Sekretarieti vimekuwa vikiendelea mjini hapa, vikiwahusisha watendaji wa juu wa CCM pamoja na makatibu wa idara husika ambao huteuliwa na mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Kikao hicho cha kesho pia kinatarajiwa kuhudhuriwa na Rais Magufuli, ambaye tayari yupo mjini hapa alipokuja kwa ajili ya sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi – Mei Mosi.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa nao wataungana na viongozi wa ngazi za juu wa CCM katika kikao hicho.

Katika kikao cha kesho, Kamati Kuu pia itajadili na kupitisha majina ya wajumbe 10 wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kutoka miongoni mwa wabunge wa CCM.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zilieleza kuwa kikao hicho kitakuwa chini ya Mwenyekiti wake Kikwete, ambapo wabunge walioomba nafasi hizo, majina yao yatapelekwa kwa wabunge wa chama hicho kwa ajili ya kupigiwa kura.

“Wabunge wana nafasi 10 za NEC na unajua waliokuwa wajumbe walishapoteza sifa za kuwa wajumbe, hivyo kwa kawaida kila Bunge jipya linapochaguliwa ni lazima uchaguzi ufanyike.

“Pamoja na kupitia majina ya wabunge waliojaza fomu, pia CC itajadili majina ya wabunge walioomba nafasi ya katibu wa wabunge wa CCM ambapo kuna wajumbe zaidi ya watatu wamejaza fomu,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, miongoni mwa wabunge wanaotajwa kuwania nafasi ya katibu wa wabunge wa CCM yumo Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda, ingawa wapo wabunge wengine ambao kwa pamoja watachujwa na kikao cha kesho.

Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM anayemaliza muda wake ni Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama.

Waliochaguliwa Bunge la 10

Aprili 15, mwaka 2011, wabunge wa CCM walichagua wajumbe 10 wa NEC akiwamo aliyekuwa Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta, ambaye alichaguliwa kwa kupata kura 104.

Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea walikuwa wanawatumia wabunge wenzao kuwafanyia kampeni, huku wengine wakikodi wapigadebe kutoka Dar es Salaam.

Katiba ya CCM inaruhusu wabunge wa chama hicho kuwachagua wajumbe 10 kuingia NEC kutoka miongoni mwao.

Mbali na Sitta, wabunge wangine walioshinda ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, Nimrod Mkono (Butiama), aliyekuwa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia.

Wengine waliochaguliwa ni wabunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki, Munde Tambwe, Faida Mohamed Bakari, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim.

Wengine ni aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye kwa sasa anawakisha Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba.

Wabunge walioanguka katika uchaguzi huo ni waliokuwa wabunge katika Bunge la 10, Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan Ngwilizi (Mlalo), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini), aliyekuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Athman Mfutakamba, Dk. Charles Tizeba (Buchosa) na Christopher Ole Sendeka (Simanjiro).

Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile, Ahmed Salum Ali (Solwa), Yahya Kassim Issa (Chwaka), Mwanahamisi Kassim Saidi (Viti Maalumu), Martha Mlata (Viti Maalumu) na Saidi Mussa Zubeir (Fuoni).
 
Ngoja wampe kofia zote 2 tuone jeuri yake na dharau zake maana chama na dola zote zake! Tuon akiwafukuza aliowaita mamluki , kuziba mianya yote ya upigaji ndani ya chama! Anataka wanachama wakiwezeshe chama kujitegemea sio waishi kwa kutegemea chama! Sijui anakuja na sera gani za kuchangia chama! Vipi atapata pesa za mikutano ya chama toka wapi? Wafanya biashara au? Maana wenzake waliopita walikumbatia wafanya biashara wakubwa! Vipi yeye? Tunasubiri CCM mpya ya JPM
 
Pagumu sana hapo.

Yawezekana akawa na njia mbadala, au akaminya vyanzo vyao vingi akawaachia kimoja kikubwa mfano kamgodi kamoja.

Hili linawezekana kabisa
 
Mahafidhina na majizi ndani ya CCM hawapendi kusikia habari hii.Joto la 'HAPA KAZI TU' linachoma vibaya sana Serikalini,sasa hofu yao joto hili likihamia kwenye Chama,halitawaacha salama.
 
Ngoja wampe kofia zote 2 tuone jeuri yake na dharau zake maana chama na dola zote zake! Tuon akiwafukuza aliowaita mamluki , kuziba mianya yote ya upigaji ndani ya chama! Anataka wanachama wakiwezeshe chama kujitegemea sio waishi kwa kutegemea chama! Sijui anakuja na sera gani za kuchangia chama! Vipi atapata pesa za mikutano ya chama toka wapi? Wafanya biashara au? Maana wenzake waliopita walikumbatia wafanya biashara wakubwa! Vipi yeye? Tunasubiri CCM mpya ya JPM

uandishi wako mh. mara ulize swali mara ujibu mwenyewe taabu tupu.
kwa taarifa yako hamna aliyechangia chama kwenye kampen ,hata kwenye mkutano na wawekezaji wa ndani alilisema hilo bila kupepesa macho watu walipe kodi , mbowe ndo anafanya biashara na chama , na hata kwenye campen 9 , 10. 2015 alisema kuna matajiri wanye mapenz mema na chama. wamejitolea kuchangia chama ikiwemo akina Sinare , kitilya, Sioye na co. lakini kwa sasa CCM itaendeshwa kisayansi zaidi chini ya jemaderi JPMmaana tayari ina vitegauchumi vyake ni kiasi tu cha kuviimarisha na kuvisimamia
 
Bahati nzuri magufuli hashindwi na jambo lolote kote huko atapasua na kukipanga vizuri chama viva magufuli.
 
Hahaha na zile walizochukua toka kwa wafanyabiashara wakubwa ajili ya uchaguzi na chama? Na hazikufika kwa walengwa wamepiga watu wasiozidi 10...mbona hilo wazi na JPM anajua mchezo mzima usije ukajitoa akili kwa michezo michafu! JPM aliwatega kuwauliza kama mtu alimchangia yeye kama JPM anyoshe mkono! Sio chama.....maana kwenye chama walivuta na wanajua walipoweka! Hazikufika!!!!
uandishi wako mh. mara ulize swali mara ujibu mwenyewe taabu tupu.
kwa taarifa yako hamna aliyechangia chama kwenye kampen ,hata kwenye mkutano na wawekezaji wa ndani alilisema hilo bila kupepesa macho watu walipe kodi , mbowe ndo anafanya biashara na chama , na hata kwenye campen 9 , 10. 2015 alisema kuna matajiri wanye mapenz mema na chama. wamejitolea kuchangia chama ikiwemo akina Sinare , kitilya, Sioye na co. lakini kwa sasa CCM itaendeshwa kisayansi zaidi chini ya jemaderi JPMmaana tayari ina vitegauchumi vyake ni kiasi tu cha kuviimarisha na kuvisimamia
 
Mwenyezi Mungu jaalia amtumbue Kinana ampe Bulembo kurahisisha kazi 2020
 
iFIKE mda kua sio lazima rais wa tanzania awe lazima awe mwenyekiti wa chama na pia ifike mda Zanzibar inufaike na huo uenyekiti
 
Bahati nzuri magufuli hashindwi na jambo lolote kote huko atapasua na kukipanga vizuri chama viva magufuli.

JPJM namba nyingine yule, sina shaka amekwisha jipanga jinsi ya kusafisha CHAMA hatangalia mtu usoni, kama nakumbuka vizuri alikwisha wapa onyo mapema kwamba utumbuzi wa majipu utahamia kwenye CHAMA kwa muda mpaka mambo yakae sawa.
 
Back
Top Bottom