Mchakato wa kuajiri watu serikalini unaratibiwa na miongozo yoyote rasmi ya serikali kwa sekretarieti ya ajira?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,471
46,002
Suala la ajira limekuwa changamoto kubwa kwa muda mrefu katika nchi. Kila mwaka maelfu ya vijana wanamaliza vyuo wengi wao wakitegemea kupata ajira serikalini au sekta binafsi jambo linalosababisha mafuriko ya waombaji kwa ajira chache zinazotangazwa popote.

Sio jambo la ajabu kabisa kwa sasa kukuta nafasi 10 za ajira zimeombwa na watu 3000! Jambo la ajabu, la kushangaza na lisilo na mantiki ni utaratibu wa ajira kupitia sekretarieti ya ajira, na taasisi nyingine za serikali kuita maelfu ya watu katika hizo nafasi chache za ajira zisizojaa kiganjani!

Mfano ukiita watu elfu 3000 kwenye usahili kwa nafasi 100 za ajira lengo ni nini? Nini hasa faida ya kuhangaisha watu, kuwapotezea muda na kuwafanya waingie gharama za ziada juu ya matatizo yao ya kukosa ajira?!

Hakuna muongozo wowote rasmi unaolekeza nafasi moja ya ajira ifanyiwe usahili wa kuandika na kisha wa mahojiano na watu wangapi?! Kama hakuna huo muongozo mimi niwasaidie; Nafasi moja ya ajira wasiitwe watu wanaozidi 5 katika usahili wa mchujo wa kuandika na waitwe watu watatu tu katika usahili wa mahojiano.

Kama mnazo nafasi 100 za ajira iteni watu 500 au 600 tu katika usahili wa awali. Vijana waliomaliza vyuo wana mahangaiko makubwa katika kupata ajira, wengi wanaishi maisha ya kubangaiza, nyie mlio na ajira za kudumu tayari msiwaongezee adha, udhia na mahangaiko kwa kutofanya kazi yenu ya uchambuzi wa maombi ya kazi sawasawa.
Mnaweza kufanya vizuri zaidi ya sasa.
 
Nasikitika ili jambo umeliona kwa side moja tu unasahau Panelist inavuta Posho kwa kukaa muda mrefu kwenye saili
 
Ndio maana serikali kupitia wizara ya kazi inatakiwa iweke miongozo na udhibiti katika mchakato mzima wa usahili serikalini.
 
Ni kweli unachosema yaani hivyo ndivyo mambo yalivyotakiwa kuwa.
Na bila shaka katika nafasi za ajira 100 zilizofanyiwa usahili na watu 3000, lazima watapatikana waliokidhi vigezo zaidi ya 100.
Swali ni je, ni njia gani inatumika kuwapata hao 100 pasi upendeleo/maghumashi yoyote?

Tukubali kuwa hapa ndipo hali ilipofikia waombaji ni wengi na ajira ni chache.

Sasa mimi ninachokiomba ni mchakato wa kuwapata hao 100 uwe ni wakiadilifu pasi na upendeleo wowote na Wala sio kuwafanyisha watu usahili halafu kumbe nafasi zenyewe walishapewa watu wengine kinyemela.

Tunajua kuna watakaokosa, lakini hakuna atakayepata kama kinachofanyiwa usahili chenyewe hakipo hata kama wanaokitaka ni wachache.
 
Wabongo bwana kila kitu wanalalamika lengo la utumishi ni kumpa nafasi kila mtu kujaribu bahati yake na wapo waliobahatika bila connection wala nn.
 
Suala la ajira limekuwa changamoto kubwa kwa muda mrefu katika nchi. Kila mwaka maelfu ya vijana wanamaliza vyuo wengi wao wakitegemea kupata ajira serikalini au sekta binafsi jambo linalosababisha mafuriko ya waombaji kwa ajira chache zinazotangazwa popote.

Sio jambo la ajabu kabisa kwa sasa kukuta nafasi 10 za ajira zimeombwa na watu 3000! Jambo la ajabu, la kushangaza na lisilo na mantiki ni utaratibu wa ajira kupitia sekretarieti ya ajira, na taasisi nyingine za serikali kuita maelfu ya watu katika hizo nafasi chache za ajira zisizojaa kiganjani!

Mfano ukiita watu elfu 3000 kwenye usahili kwa nafasi 100 za ajira lengo ni nini? Nini hasa faida ya kuhangaisha watu, kuwapotezea muda na kuwafanya waingie gharama za ziada juu ya matatizo yao ya kukosa ajira?!

Hakuna muongozo wowote rasmi unaolekeza nafasi moja ya ajira ifanyiwe usahili wa kuandika na kisha wa mahojiano na watu wangapi?! Kama hakuna huo muongozo mimi niwasaidie; Nafasi moja ya ajira wasiitwe watu wanaozidi 5 katika usahili wa mchujo wa kuandika na waitwe watu watatu tu katika usahili wa mahojiano.

Kama mnazo nafasi 100 za ajira iteni watu 500 au 600 tu katika usahili wa awali. Vijana waliomaliza vyuo wana mahangaiko makubwa katika kupata ajira, wengi wanaishi maisha ya kubangaiza, nyie mlio na ajira za kudumu tayari msiwaongezee adha, udhia na mahangaiko kwa kutofanya kazi yenu ya uchambuzi wa maombi ya kazi sawasawa.
Mnaweza kufanya vizuri zaidi ya sasa.
Kaka habariii kwemaaa
 
Back
Top Bottom