Mchakato wa kisheria wa kubadili jina lako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchakato wa kisheria wa kubadili jina lako

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Voice of Wisdom, Oct 23, 2011.

 1. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Heshima zenu wakuu, na poleni na majukumu ya wiki nzima.

  Kuna jambo naomba kujuzwa kuhusu kubadili jina. Hii inatokana na ukweli huu "nilipokuwa std 4 tz nilihamishiwa shule huko kenya ambapo nilisoma miaka miwili ( std 4 &5) kisha nikarudi tz, ile shule niliyokuwa mwanzoni nikakuta jina langu kuna mtu analitumia naye yupo std 7. Nikahamia shule ya jirani mwalimu mkuu akanipa jina la mwanafunzi mwingine ambaye alirudia std 6 nikawa nalitumia hadi sasa nipo chuo mwaka wa 2.

  Kuna tetesi nimepata kwamba mtu unaweza kubadili jina. Wajuzi naomba mnijuze, je ni hatua gani natakiwa kuzifuata na je inagharimu fedha yeyote?

  Nawasilisha.
  =====================
  =====================
  ======================
  =======================
  ==========================
  ==========================

   
 2. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  haiwezekani!,nyie ndio mnatusumbua watoto wa kimaskini..!
   
 3. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  wewe sema tuu ulirudia la saba,ili ufaulu!inawezekana,unaenda kuapa mahakamani,unapata certificate pia ya change of name!ila useme jina ni la kwako unataka kubadili,ukisema ulichukua la mtu utazua soo
   
 4. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  in short mi ni mtoto wa fukara, my parents ni wakulima wadogo wadogo, mazingira ndo yalisababisha mimi kusoma kenya, na by the way nilisoma community day school
   
 5. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  nashukuru mkuu kwa ushauri. Kwa kifupi cjawah kurudia darasa since nimeanza vidudu. Huku nitasema kama ulivyonieleza, hapa nimekuwa mtupu ili nipate msaada
   
 6. baghozed

  baghozed JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 515
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  sasa wataka uwe na jina gani? la kwako asili ama upate jipya?
  na je hilo unalolitumia una cheti chake??
  kama huna cheti cha jina unalolitumia sasa waweza pata cheti cha kuzaliwa kirahisi tu,na ukaendelea kutambuliwa kwa jina hilo,lakini kama wataka kujulikana kwa majina yote basi itabidi uende mahakamani ukaape na kupata kitu kinaitwa DEED POOL ili kukutambua kuwa wa zamani ndo wewe.
  sijui kama umenipata hapo
   
 7. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  mkuu shukrani, lengo langu ni kutaka kutumia jina langu la asili.
  cheti cha kuzaliwa chenye jina ninalotumia sasa ninacho pia
   
 8. baghozed

  baghozed JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 515
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  so una vyeti viwili vya kuzaliwa vyenye majina tafauti?
  Cheti cha asili tena usikitumie nenda kaape tu mahakamani upate DEED POLL ON CHANGE OF NAME coz uta renounce and abandon the use of current name na utataja jina utakalotaka utambulike,
  gharama itategemea coz hilo kwa mahakama ni dili waweza ukakaa kwenye benchi ukaletewa tu ukitoa chchote kitu,bt ukitaka haki utajuta kujaribu coz utasumbuliwa tu.
   
 9. d

  daisy Senior Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwa kiswahili ni sawa kusema kubadili jina.

  Nenda kwa Wakili mueleze hiyo maneno not necessary the whole stori, ila mwambie tu hilo jina ulisomea na sas unahitaji kutumia majina yako uliyopewa either kwa kubatizwa kama wewe ni mtristo au ulipozaliwa.

  atukutengenezea document inaitwa DEED POLL on change of names utaapa utaipeleka kuisajili kwa msajili wa hati then baada yapo peleka kwenye chuo unachosoma, benki, na sehemu zote ambazo una kitambulisho chenye jina la zamani watakubadilishia majina yako utapata kitambulisho kipya na kuanzia hapo document zako zote zitasomeka kwa majina yako mapya.
   
 10. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2013
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nawasalimu Wana Jukwaa La Sheria na Wanachama wote wenzangu wa Jamiiforum!!
  Zaidi Sana,niwape pole na Shughuli za Kujenga Taifa!!

  Naomba nieleze kwa Muhtasari tatizo Langu halafu nisikie kutoka kwenu Kuhusu namna gani Mnaweza Kunishauri maana Peke Yangu nahisi kuishiwa Hekima Kuhusu namna gani niendee Changamoto hii!!

  Mm nilimaliza Elimu ya Msingi katika Shule ya Serikali Mwaka 1997 na nikajiunga na Sekondari ya Serikali Mwaka 1998-2001,Mwaka 2002-2004 nikamaliza Kidato cha Sita,Katika hatua zote hizo nilimaliza kwa Matokeo Mazuri tu!!
  Tatizo Langu ni Jina,Jina Langu La kwanza ni La Kiislamu na La Pili ni La Kikristo(Yaani Jina La Baba Yangu) Hii imetokana na Mama Yangu Kuwa Muislamu ambaye Kimsingi ndiye aliyenilea na Kunisomesha na Baba Yangu ni Mkristo!!
  Sikupenda kuwa na Jina Moja La Imani hii na Lingine La Imani ile na kwa sababu hiyo Mwaka 2005(Mwaka mmoja baada ya Kumaliza kidato cha Sita) nikabadilisha Jina Langu la Kwanza kwa taratibu zote za Kisheria nikapewa Document inayoelezea Kubadilisha kwangu Jina Kisheria inaitwa Deed Poll!!


  Kwa Kutumia Deed Poll nikaweza Kubadilisha Jina hadi kwenye Pasi yangu ya Kusafiria,kwenye Mchakato wa Kitambulisho cha Kupigia Kura nikaweka Jina Langu Jipya na hata Kwenye Mchakato wa Kitambulisho cha Taifa.

  Shida ni kwamba Mwaka Huu nimeazimia Kuingia Chuo Kikuu na nilipokwenda Mlimani Kuulizia nilipata wakati Mgumu sana,Academic Certificate ni Msaafu hapa Tanzania,hauwezi Kubadilishwa asilani!!
  Chuo kimesema kama nikitaka Kusoma nitatumia Majina yaleyale yanayo-appear kwenye Vyeti vyangu Vya O'level na A'level vinginevyo imekula kwangu,Sasa nikawauliza Kwa nini Sheria Mama iruhusu kubadili Jina Halafu taratibu za Chuo tu zikatae? Kwamba Taratibu za Chuo ni Kuu Kuliko Sheria za Nchi maana Deed Poll ni Nyaraka ya Kisheria na Utaratibu wote wa Kisheria Umefuatwa,Pamoja na Hoja zote nilizojaribu Kuzijenga Dean of Students wa Shule ya Biashara hakunielewa,Akasema HAIWEZEKANI!!

  Nina Imani kubwa na Jf,Najua Wadau wengi hapa Wana Fikra Pevu,nitafanyaje kujinasua kwenye kadhia hii,Ninawezaje kwenda Chuo kwa Jina Langu Jipya maana hata NECTA niwapigia Simu Majibu ni hayohayo,hawawezi Kubadili Jina kwenye Cheti!!

  Neno hili Limekuwa Kubwa kwangu nami kwa Unyenyekevu Mkubwa ninalileta kwenu!!
  Ninatanguliza Shukrani!!
   
 11. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2013
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  Dah mkuu hii ishu yako kwa TANZANIA hii ni nzito sana...Huwezi kubadili majina ya vyeti vya elimu na hata kupata vyeti vya pili ni kazi vile vile... Chuoni hawana kosa kwani wanatakiwa wafuate majina yaliyomo kwenye vyeti na wana operate between nationa and international laws.... Sidhani kama suala lako linawzekana kwani hata kwenye ajira ni tabu tupu......
   
 12. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2013
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Asante Asigwa,Nimekusikia Mkuu wangu,Asante kwa Kuchukua Muda wako na Kuniandikia!!
   
 13. Root

  Root JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2013
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,285
  Likes Received: 12,997
  Trophy Points: 280
  Sababu wengi wangeweza nunua vyeti na kubadili majina ndio maana iko hivyo
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2013
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Mbona vyeti vinanunuliwa kama kawaida? huna hoja.
   
 15. mossad007

  mossad007 JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 1,169
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Usiwalaumu chuo cz uli apply kw vyeti vyenye majina tofauti na admission zao zinafuata application names. Deed poll itabaki kuonyesha ulibadili majina lakini academic certificate haziwez kubadilishwa na hii ni salama kw future yko utapoenda kuomba kaz na vyet vyenye majina manne matano tofauti matter una deed poll na affidavit bdo kw mwajiri itamjengea hali ya was was na hawa watu hawana mda wa kuanza kukuchunguza in detail while kuna watu wengne mamia waeomba kaz hyo hyo na wanavigezo. Endelea na majina yko ya zaman kwenye vyeti ila deed poll itengenezee affidavit
   
 16. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2013
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Peleka mahakamani huyo mkuu wa chuo akafundishwe sheria.
   
 17. O

  Oby One Member

  #17
  Feb 7, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana mkuu, ulipaswa kufanya hivyo mapema kabla ujajisajili kwajili ya mitihani ya kidato cha pili. Tatizo la sheria za nchi yetu ni kama zinapingana. Umenikumbusha mbali sana nilisha teseka sana kwa tatizo kama lako kipindi cha nyuma. POLE MKUU
   
 18. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2013
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,128
  Likes Received: 1,726
  Trophy Points: 280
  Mkuu,msaidie sasa,wakati ndio huu,ulilitatua vipi hilo tatizo lako ili naye apate mwangaza,ndiyo uzuri wa JF kaka,kusaidiana na kufaana hata kama hatufahamiani
   
 19. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2013
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  pole sana mkuu,
  ila kubadilsha jina kisa dini mimi kwangu naona haina faida! kwani kama ulkua unaitwa Mohamed John na sasa unaitwa Mohamed Hassan inakuongezea nini? Jina ni jna tu hata waweza itwa Dunia, Meza, Ngengemkeni, Bahari n.k na likawa jina lako!
  Ushauri - Rudia jina lako la awali halafu acha udini
   
 20. K

  KITWANGAUTAM Member

  #20
  Feb 8, 2013
  Joined: Jan 19, 2013
  Messages: 80
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Kaka nakushauri hivi, usiangaike na majina ya kwenye vyeti vyako, ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu,endelea kutumia majina hayohayo kazn , alafu uchague mwenyewe kati ya hizo din 2 ni ip itakufaa ndipo uende kwenye din husika ubadilishe jina kulingana na inavyopaswa, hivyo kazn utatumia majna yale2 ya mwanzo lkn katka imani unakuwa tayar unamajina yako, lengo c ni kwenda ahela tu...eee kaka nawasilisha
   
Loading...