Mchakato wa katiba ya Muungano hauna nchi kubwa na ndogo,Tanganyika na Z.bar ziwe sawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchakato wa katiba ya Muungano hauna nchi kubwa na ndogo,Tanganyika na Z.bar ziwe sawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Nov 14, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1]Wabunge wetu wanao iwakilisha Z,bar tokeni kwenye Bunge pindipo ukisomwa mswada wa katiba ya Muungano.[/h]Written by amini // 14/11/2011 // Habari // No comments

  [​IMG]Munakumbuka wabunge wa chadema walivyotoka kwenye bunge ili kuonyeshwa hawakuridhishwa na uchaguzi?.

  Mukifanya hivyo italeta faraja zaidi kwetu Wzanzibar na itakuwa mumefanya kitendo cha ujasiri na uzalendo wan chi yenu, ikiwa wabunge wa ccm Zanzibar watabakia kwa woga wao basi washeni tokeni japo nyiyi tu wa cuf itaonyesha kuwa hamukupendezewa na murudipo Zanzibar wazanzibar tutawapokea kiheshima.
  Na hili lakutoka hamukulianza nyiyi hata chadema walitoka walivyo chukizwa na Kikwete kufuja uchaguzi kwa hio sio gani na hata inchi zilizo endelea kama vile Marekani nan chi za Eu hutoka ktk Baraza la Umoja wa Mataifa UN mara nyingi tu na hususani mzozo wa wao na Iran.
  Hii nikuonyesha kuwa mumekerwa na mchakacho wa kuchakachuliwa katiba ya Muungano na Zanzibar kuto kupewa haki sawa za kujadili katiba kama ni sehemu ilio unda huo Muungano wenyewe.
  Hivi sasa ubabaishaji umekuwa mwingi kuhusu Muungano wenyewe tokea kufa kwa Tanganyika imekuwa Muungano na makubaliano yamezidi kuwa fake na yenye utata kutatua.
  Tukiachana kuwa Muungano hauna ridhaa ya watu wote wa pande mbili lakini kwa upande wa Zanzibar hatari nikubwa zaidi yakuyayuka power ya Zanzibar na nguvu ya Zanzibar kuwa ni sehemu moja ya Muungano .
  Tunawaomba Wabunge wetu mutoke vipi suala kubwa kama hili linalohusu nchi mbili zilizo unda huo Muungano Zanzibar Watanganyika wai-Treaty kama mkoa? Madaraka yote na power yote yakupanga na kupangua yaweko upande moja tu.
  Ikiwa viongozi wetu watalifanya lipite hili basi zitaibuka kero nyingi tu za Muungano kwa vile tayari upande moja umeshajifanya jabari na kujiona super power, hili suala sio laKikwete kushauriana na Shein , hili linahusu Baraza la Uwakilishi kushauriana na japo baraza la muda la Tanganyika kuhusu hatma ya nchi mbili husika.
  Kama watashindwa kuwashirikisha wananchi kuanzie a-b basi mabaraza mawili yakae kujadiliana kwanza nikuhusu huu Muungano wenyewe ndio mama halafu ndio wazae hio katiba sio leo kero za Muungano zinazidi na kushindwa kupatiwa ufumbuzi halafu turukie katiba ambayo hio katiba yenyewe wazanzibar tumefanywa niwapambe wapempeni tu.
  Viongozi wetu wa smz ihurumieni Zanzibar musiwe kimya kesho na keshokutwa katiba hii hii ndio kitanzi shetu cha kuambiwa tulipo andika watu wenu walikuwepo na nilazima muitii na ndio itatufunga ktk mabano yake.
  Cuf ccm/smz you have to do same thing kwa Zanzibar
   
Loading...