Mchakato wa katiba mpya unakwamishwa na CCM miaka yote

Jul 23, 2018
46
66
Habari wanajukwaa!!

Naona kuna vuguvugu (fukuto) la aina yake hapa Nchini la Madai ya KATIBA MPYA likiongozwa zaidi na kundi la Chama cha Siasa (CHADEMA).

Mimi pia ni muumini wa kuunga mkono upatikanaji wa KATIBA MPYA na iliyo Bora. Madai ya KATIBA MPYA katika Taifa la Tanzania ni madai ya Kihistoria, hayajaanza juzi, jana wala leo.

Ni vyema ifahamike kuwa, tangu Uhuru wa Taifa hili, Watanzania hawajawahi kuandika Katiba yao wanayoihitaji itumike katika kuwaongoza na kutoa dira ya maendeleo yao. Tangu Uhuru mwaka 1961 hadi sasa 2021. Kwahiyo wanaodai Katiba Mpya wapo sahihi kabisa, maana kwa mujibu wa Mwl. Nyerere, Katiba ni sawa na "Vazi" unalomshonea mtoto.

Vazi ulilomshonea akiwa na miaka mitano kamwe hawezi kulivaa akiwa na miaka 30. Lazima atakuwa amekuwa na kuongezeka katika kimo na umbo. Ndivyo ilivyo pia katika Nchi na Katiba.

Mwaka 1998 iliundwa Tume ya Jaji Kisanga ambayo ilipewa mambo 19 ya kwenda nayo kwa Wananchi ili yatolewe maoni juu ya marekebisho ya Katiba. Tume ilipewa kitu kilichoitwa "The Government White Paper No.1 of 1998".

Katika ripoti ya Tume ya Jaji Kisanga, ilipendekezwa na Wananchi kuwepo na mfumo wa Serikali tatu badala ya Serikali mbili uliopo sasa.

Rais Mkapa (kwa wakati ule) alivyopokea ripoti ile alikuwa wa kwanza kujitokeza hadharani kwa vyombo vya Habari na kuipinga ripoti ile. Hakuishia tu kuipinga bali alielekeza kwamba ripoti ile ni lazima ipite kwanza kwenye Kamati Kuu ya CCM ndipo ipelekwe Bungeni.

Mara baada ya hapo, badala ya kuandikwa Katiba Mpya, Serikali ikatangaza marekebisho ya kumi na tatu ya Katiba (13th) ambapo waliingiza mambo makubwa manne.

Tutaendelea na awamu ya Kikwete endelea kufuatilia...
 
Katiba ya mwaka 1977 iliandikwa na wakoloni?

Nasubiri muendelezo nipate madini kwa afya ya akili yangu, maana haitanisaidia chochote zaidi ya hilo, sisi ni wale wale.
 
Katiba ya Mwaka 1977 iliandikwa na wajumbe wa CCM waliokuwa wamepewa jukumu la kuandika Katiba ya CCM baada ya kubadilishwa kutoka TANU.

Kwahiyo hakuna mahala popote ambapo Wananchi walishiriki katika kuandika Katiba ya sasa.
 
Back
Top Bottom