Mchakato wa katiba: Kwa hapa tulipofikia tuangalie tulikoanzia

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Wote tunafahamu kwamba, Katika kipindi cha miaka zaidi ya ishirini iliyopita chama cha Mapinduzi hakikuwahi kuwa na agenda ya kutengeneza katiba Mpya.

Lakini mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, hasa baada ya kuwa wazi na dhahiri kwamba DR SLAA kaibiwa kura zake kihuni kabisa kwa ushirikiano wa CCM,TISS na tume ya uchaguzi na alipoanzisha sekeseke za maandamano kila kona ya nchi ambayo yaliungwa mkono na wananchi kila alikokwenda ukiongezea na matukio yaliyokuwa yakiendelea katika nchi za Kiarabu ndo ikalazimika Kikwete atangaze mchaakato wa kutengeneza Katiba Mpya, Hili alilifanya Kikwete Mwenyewe bila kushirikisha viongozi wowote wale wa serikali wala chama chake zaidi ya mwandishi wa hotuba zake katika hatua za kuhakikisha kwamba maandamano yasijemkumba na kumchomoa Ikulu.

Kutokea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, wananchi waliitikia maandamano ya CHADEMA kama ishara ya kukubaliana na mahitaji yafuatayo.
1. Tuwe na tume huru ya uchaguzi ili kuepuka uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi.
2. Matokeo ya Urais yaweze kupingwa mahakamani ili itakapotokea hata katikati ya uwepo wa tume huru ya uchaguzi uchakachuaji ukafanyika basi haki itafutwe mahakamani.

Mahitaji haya ndiyo yaliyokuwa hitaji la msingi la wananchi, na mijadala mingi ilijikita katika hili na sio haya mambo ya serikali tatu na viti maalumu.

JE. Rasimu hii ya katiba imekidhi mahitaji haya?
 
Back
Top Bottom