Mchakato utaanza lini Zanzibar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchakato utaanza lini Zanzibar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 8, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0  Written by Mrfroasty (Ufundi) // 07/02/2011 // Makala/Tahariri // 5 Comments

  [​IMG] Na Ally Saleh,
  Ingawa kilio cha kuwa na mabadiliko ya Katiba ni cha muda mrefu Zanzibar na Tanania, lakini ni kauli ya hivi karibuni ya muda Rais Jakaya Kikwete ndio imetoa muelekeo kuwa mabadiliko hayo yanakuja.
  Ila kuja kwake si lazima kuwe na Katiba Mpya kama wengi wanavyotaka, lakini kwa hila ambazo Watanzania tumezoea kuziona inawezekana kabisa tukawa na mabadiliko ya Katiba bila ya Katiba Mpya.
  Ukosefu wa udhati wa viongozi wetu wa kisiasa na suala la kuweka maslahi ya kujilinda kwao kuwa ni la mbele kuliko kitu chochote chengine, ni mambo ambayo yamekwamisha vitu vingi nchini Tanzania, seuze hiyo Katiba ambayo inavyotakiwa imguse kila mtu hata huyo kiongozi wa siasa.
  Inashangaza jinsi ya viongozi wa Kiafrika wanavyoogopa mabadiliko ya Katiba ingawa wanataka wabaki madarakani. Hufanya kila njia kubakisha Katiba ambayo inafanana na sura zao, kuliko Katiba ambayo itahoji mamlaka yao na kuupa nguvu umma.
  Tanzania inahitaji Katiba Mpya, lakini watu wengi hawajui kuwa Zanzibar inahitaji zaidi Katiba Mpya kama vile ambavyo Zanzibar ilihitaji Zanzibar Mpya, na kwa kiasi fulani imepatikana.
  Kwa miaka Watanzania walijifanya vipofu wakati maovu kupita kimo yalivyokuwa yanaytokea Zanzibar. Kuanzia utawala wa kiimla na fimbo ya Chuma ya Abeid Amani Karume uliopelekea watu kadhaa kukosa haki zao na wengine kuuawa na kukosekana kabisa uhuru wa kujieleza na kujikusanya, lakini kwa kutaka kuuhami Muungano, Watanzania hawakujali kabisa suala la Katiba kwa Zanzibar.
  Kisha ukaja utawala wa utawala wa Aboud Jumbe Mwinyi ambaye ingawa alifungua milango kidogo lakini wengi hawajui, na leo ndio nawaambia kuwa ni yeye aliyeanzisha utaratibu wa kuita serikali ya Zanzibar kuwa ni ya Mapinduzi, na ambayo wengi wa wanasiasa wa Bara wanaitetea bila ya kujua.
  Na Zanzibar hiyo hiyo ikiwa imefanya chaguzi nne za ushindani lakini bado Serikali yake inaitwa ya Mapinduzi na bado salamu kubwa ni ile ya Mapinduzi Daima, na kama ilivyokuwa miaka ya 1960 basi pia hivi sasa Serikali ya Tanzania inafumba macho kwa hili la Zanzibar ili kudumisha Muungano.
  Ingawa Zanzibar ilipata Katiba yake ya 1984 baada y mjadala wa kuimarisha demokrasia uliochapuzwa na CCM, lakini Wazanzibari hawajawahi kushirikishwa katika zoezi lolote lile la maandiko ya Katiba yao, kuanzia ile ya 1979 na hat aile ya 1984.
  Na hayo yanayoitwa mabadiliko makubwa ya 2010 ambayo nayo watu wengi wa Tanzani Bara kwenye kada ya wasomi wanayapigia kelele, basi nayo pia Wazanzibari hawakushirikishwa katika kuyaandaa seuze katika kuyaandika ingawa hivi sasa yametuganda sote.
  Watu hawajui kuwa Zanzibar hadi leo imo kwenye misuguano ya kisiasa, kitabaka na kiitikadi ingawa sasa hivi hali imepozwa kidogo na wengi tukitaraji itaendelea kuwa hivyo baada ya kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
  Watanzania wanajifanya hawaoni kuwa ubaguzi bado ni suala kubwa hapa Zanzibar. Hivi kwa mfano amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Tanzania amewahi kutaka kujua kwa nini ni Waznazibari wa rangi moja tu, huku nchi ikiwa ina rangi nyengine, ambao huingia katika vikosi vilivyo chini yake? Jee ilihitajika kufungua kesi ya ubaguzi ndipo hilo lieleweke?
  Jee rasilmali za nchi zinatumikaje na maamuzi hufanywaje ikiwa mtu naweza kuamua kujenga au kujimegea ardhi ndani ya hifadhi ya taifa ya Maruhubi na bado isiwe lolote lile maana hakuna hatua iliyochukuliwa, jee Serikali ya Muungano hailijui hili kwa athari ya wananchi wa Zanzibar ambao hatimae ni raia wa Tanzania?
  Hivi sasa mchakato wa Katiba ukiwa umeanza macho ya Watanzania hawaitizami Zanzibar. Ukifuatilia Konogamano la Chama cha Wahadhhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDASA) utaona dhahiri kuwa kwa wengi Katiba ya Tanzania ni kwa maslahi zaidi ya Tanganyika na bila ya Zanzibar.
  Wachache waliozungumzia Zanzibar waliitaja kwa maana ya kuidogosha na kutaka ijisalimishe ndani ya Jamhuri ya Muungano, zaidi ya ambavyo imejikunyata ndani ya Muungano kwa miaka 49 na hawa wakahoji Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka jana.
  Wengi ya Watanzania hawajui au hawataki kujua kuwa kwa makubaliano yetu ni kuwa Zanzibar itaendela kuwepo, hata jina libadilishwe kiharamu kutoka Zanzibar kuwa Tanzania Visiwni au mtawala wao kuitwa Kiongozi wa Zanzibar badala ya Rais wa Zanzibar.
  Kwamba wengi hawawezi kumeza ukweli kuwa Zanzibar ni sehemu moja kamili ya nchi mbili zilizoungana na kwamba kuwa ni Sehemu ya Jamhuri ya Muungano hakumaanishi kuwa Zanzibar haipo kama ambavyo Tanganyika ilivyojikubalisha kuwa haipo.
  Kuwa wengi hawajui kabisa jinsi ambavyo Katiba ya Muungano imechukua mamlaka kadhaa ya Zanzibar hata katika mambo ambayo yamekubaliwa kuwa si ya Muungano, na kwa hivyo mabadiliko ya 10 yaliporudisha badhi ya mambo hayo, hilo halikuwa jambo ambalo ni rahisi kwao kulielewa.
  Kwamba hakuna hadi leo, mabadiliko yoyote yale ya Muungano au sheria ya Muungano iliyotungwa na chanzo chake kikiwa Zanzibar kwa njia moja au nyengine. Kwa maneno mengine Wazanzibari hawajachangia katika uanzishaji wa jambo la Muungano au sheria ya Muungano isipokuwa katika vikao vya Bunge, lakini si kupitia mawazo ya umma au Serikali yao.
  Kwa Wazanzibari wengi tukielekea miaka 50 ya Muungano, basi Muungano huo nikitendawili kikubwa, kama ambavyo pia kuna kundi la Wazanzibari ambalo linaona pia Mapinduzi ni kitendawili kikubwa kwao.
  Kwa hivyo kwa fikra zangu haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa wa Katiba ni kubwa zaidi Zanzibar kuliko hata ilivyo Tanzania Bara. Sitaki kupunguza au kushusha matatizo ya Kikatiba ya Watanzania wanaoishi Bara, lakini hataka kusema kuwa wao ni Watanzania na sisi ni Wazanzibari mwanzo kisha ni Watanzania.
  Tuna mambo mengi ndani yetu kama Wazanzibari ambayo kwa miaka 50 ya Mapinduzi tumeshindwa kuyamaliza na wakati huo huo tuna mambo mengi kama Watanzania ambayo yametuzonga kwa miaka 50. Tunavutwa huku na huku na wenzetu wanavutwa upande mmoja tu.
  Kwa fikra zangu Wazanzibari ndio wanaopaswa kuchangamka au kuchangmkia zaidi hali iliyojitokeza hivi sasa na ndio ambao wameonyesha kuwa wako mbele kifikra kwa kuwa Serikali ya Zanzibr ilianzisha Sheria ya Kura ya Maoni mwaka jana.
  Lakini jee fursa hiyo inaweza kuchukuliwa na Wazanzibari yaani kuijadili Katiba ya Tanzania kama Katiba ya Tanzania lakini pili uhusiano wake na Katiba ya Zanzibar kwa maana nyengine haja za Waznaibari kama Watanzania na lakini pia haja zaWaznzibri kama WAanzibari?
  Hilo linanitia mashaka sana. Kinyume na wenzetu Tanzania Bra fursa za mijdala zinaweza kuwa nyingi sana, lakini hapa siamini kama zitakuwepo kiasi hicho. Matokeo yake upane mmoja utsema sana na mengi kiasi mabachoitaonekana kuwa wanahoja na mantiki na upande mmoja utakaa kimya sana wataonekana hawana kitu wala shida za kikatiba.
  Kwa hivyo wakati najiuliza ni lini mchakato wa Katiba utaanza Zanzibar bila ya shaka najua ni Katiba mbili, lakini najiuliza pia taasisi gani zitazochukua jukumu hilo…sizioni Wazanzibari wenzangu…na kama zipo napenda kuonyeshwa na kuzipa changamoto hii.
  Maana kama Wakristo wnavyosema Kanisani wakati wa ndoa, mwenye la kusema aseme sasa hivi au afumbe mdomo maisha. Naogopa tusije tukafumbwa mdomo maisha.
  –
  Ally Saleh +255 777 4300 22
  Players’ Agent Licenced by
  Tanzania Football Federation (TFF)
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mchakao wa kutenganisha pumba na mahindi... mpaka kiangazi kiishe kwani vichaa ni wengi kipindi hiki
   
Loading...