Mchakato mwingine wa katiba mpya

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,163
787
Katiba mpya inamichakato miingi, huu nao wa kila chama kwenda mafichoni kuuchakato nina wasiwasi na kuuchakachua,

Hii katiba ni wananchi sio ya chama chochote, lkn ninamashaka makubwa na namna vyama vinapokwenda kuujadili ili iweje

Hivi ni nani atatakiwa mawazo yake yachukuliwe ni hawa wanaokaa na kujadili tena mawazo ya wananchi?

Ninaimani na ripoti ya warioba kwamba mawazo mengi ni ya wananchi, lakini kiongozi mmoja anatoa wapi haki ya kukataa

maoni ya wengi?

KATIBA HII MAONI HAYA LAZIMA YALINDWE KAMA WIZI ULE WA KURA,
 
Mimi nashangaa sana, wakati makundi yote yalipewa nafasi ya kutoa maoni. Sasa wameanza CCM na vyama vingine vitafuatia na mwisho wake sijui utakuwaje. Ngoja tuone
 
Wanasiasa wetu wanajiona wao ndio wenye Tanzania na sisi wengine ni vijakazi wao,hii katiba itafinyangwa mwisho siku mwananchi hana chake na tunarudi kule kule.......
 
Kama hawa viongozi huomba kura kutoka kwetu, basi wakae chini na wasikilize kila wananchi wanachotaka, zaidi ya hapo ni huchu wa utawala. tumechoka kuburuzwa na chama cha kifisadi
 
Back
Top Bottom