Salaam Wanajanvi,
Tupo katika mapambano na malaria, hasa kuwatokomeza mbu wanaoeneza hayo malaria.
Mwenye kujua hebu tujuze kama mchai chai (Lemon Grass) unaweza kufukuza mbu pamoja na wadudu wengine kama nzi?
Kama ni kweli hufukuza mbu (insect reppellent-citronella), haya majani yanatumikaje? Pamoja na kwamba watu wengi wanatumia kama kinywaji moto badala ya chai.
Kama utafukuza mbu, je unapatikana sehemu gani?
Nawasilisha
Tupo katika mapambano na malaria, hasa kuwatokomeza mbu wanaoeneza hayo malaria.
Mwenye kujua hebu tujuze kama mchai chai (Lemon Grass) unaweza kufukuza mbu pamoja na wadudu wengine kama nzi?
Kama ni kweli hufukuza mbu (insect reppellent-citronella), haya majani yanatumikaje? Pamoja na kwamba watu wengi wanatumia kama kinywaji moto badala ya chai.
Kama utafukuza mbu, je unapatikana sehemu gani?
Nawasilisha
1.KUSAFISHA FIGO NA MKOJO
Mchaichai una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu katika mwili, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali za viwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali.Figo inapokuwa safi na imara,hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika
kirahisi
2.HUSAIDIA UMENGENYWAJI WA CHAKULA MWILINI
Mchaichai husifika kusaidia urahisishaji wa mmengenyo wa chakula mwilini na kutibu maumivu ya tumbo kama vile hali ya tumbo kujaa gesi.
3.KUZUIA HALI YA KUHARISHA MARA KWA MARA
Mchaichai pia ni dawa nzuri kwa wale wanaosumbuliwa na hali ya kuarisha mara kwa mara,kwani inauwezo wa kupambana na mdudu aina ya protozoa anayesababisha ugonjwa huu.
4.HUSAIDIA KUSAFISHA DAMU
Faida nyingine ya mchaichai ni kusafisha damu mwilini hasa kwa watu ambao wamekuwa na tabia ya kupata magonjwa ya ngozi kama mapele na kutoka majipu.
5.HUUPA MWILI KINGA DHIDI YA UGONJWA WA SARATANI.
Mchaichai umegundulika pia unauwezo wa kuua seli zinazoweza kusababisha ugonjwa wa saratani.Kwani kwenye gila gram 100 ya mchaichai kuna virutumbisho ambayo vinaweza kuondoa na kuukinga mwili dhidi ya sumu ambayo inasababisha ugonjwa wa saratani.
6.KUONDOA MLUNDIKANO WA MAFUTA KATIKA MISHIPA YA DAMU
Mchaichai husaidia kuondoa mafuta katika mishipa ya damu hivyo kuruhusu damu kupita vizuri katika sehemu mbalimbali za mwili na kuifanya mishipa hiyo kuwa na afya njema.Pia kusaidia mapigo ya moyo kuwa katika hali nzuri wakati wote.
JINSI YA KUTUMIA MCHAICHAI
Kupata faida hizi unashauriwa majani ya mchaichai yalowekwe katika maji ya moto kiasi cha vikombe vitatu vya chai, weka majani ya mchaichai kisha kunywa maji hayo kiasi cha kikombe kimoja cha chai kabla ya kula chochote asubuhi, mchana, nusu saa kabla ya mlo, na jioni kabla ya chakula cha jioni.Pia unaweza kutia sukari kwa kiasi kidogo mno. Unaweza fanya jambo hili kuwa endelevu kwa kutumia chai ambayo imepikwa kwa majani ya mchaichai mara kwa mara.
[https://4]
Kumbuka faida zilizo tajwa hapo juu ni chache tu ambazo nimekuletea siku ya leo na ni matumaini yangu utanza kutumia mchaichai kuwa sehemu ya lishe yako ili kupata virutubisho mbalimbali na kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Sent using Jamii Forums mobile app