Mchaichai, jina la kisayansi

Aluta

Member
Aug 16, 2008
69
3
Wasalaam!

Naomba kama kuna mtu anafahamu jina halisi la mmea kisayansi) mchaichai, kwa wale ambao wamewahi kunywa chai ya mchaichai nadhani mtakuwa mmenielewa na maana gani.

Si maana nataka jina la majani ya chai yanatumika kutengeneza chai ya rangi, hapana bali jina la MCHAICHAI...majani fulani membamba na marefu hutumika kutengeneza chai pia.
 
Wasalaam...naomba kama kuna mtu anafahamu jina halisi la mmea(kisayansi) mchaichai...kwa wale ambao wamewahi kunya chai ya mchaichai nadhani mtakuwa mmenielewa na maana gani (Si maana nataka jina la majani ya chai yanatumika kutengeneza chai ya rangi, hapana bali jina la MCHAICHAI...majani fulani membamba na marefu hutumika kutengeneza chai pia.

Kaka hii umenikumbusha mbali... Mambo ya mchai chai, zaidi ya radha yake muruwa pia ni mmea wenye uwezo mkubwa sana wa kuzuiya mbu na kuzuiya fungus.

Unachotakiwa kufanya ni kuoteza huu mmea kuzunguka nyumba yako, na mbu wote wataishia mita mia kutoka uswa wa nyumba. Mafuta yake (oil) utumika kama Antifungal.

Tukirudi kwenye swali lako, Jina la Kiingereza la mmea huu kiasi una majina mengi kidogo... unaitwa:

Lemongrassor lemon grass (Cymbopogon nardus). Pia unajulikana kama mosquito plant, barbed wire grass, silky heads, citronella grass, fever grass or Hierba Luisa.

lemongrass_citronella_grass-dsc02292.jpg
PB070053.JPG
 
Hata mimi ni mpenzi sana wa mchaichai yaani chai yake ni tamu sana halafu ukiipatia vitumbua na mchuzi mzito wa kuku unaweza ukatafuna vidole kwa utamu :) Swali kwako X-paster miaka yoye chai ya mchaichai niliyokunywa ilikuwa ni ya rangi. Je, huwezi kutengeneza chai ya maziwa ya mchaichai?
 
Hata mimi ni mpenzi sana wa mchaichai yaani chai yake ni tamu sana halafu ukiipatia vitumbua na mchuzi mzito wa kuku unaweza ukatafuna vidole kwa utamu :) Swali kwako X-paster miaka yoye chai ya mchaichai niliyokunywa ilikuwa ni ya rangi. Je, huwezi kutengeneza chai ya maziwa ya mchaichai?
Kaka haya mambo ya michuzi ya kuku (plus mbaazi za tui bubu la nazi) kwa vitumbua unatufanya wengine tuwakumbuke ma'bibi zetu M'Mungu (awarehemu).

Unajuwa bro hata mimi nashangaa sana ni mara chache sana niliwahi kunywa chai ya maziwa iliyochanganywa na mchai chai, tena kwa kulazimisha. Ila mara zote ni chai ya mkandaa. Sihelewi hikma yake hapa.

Labda wazee wanataka wapate ile natural tea flavor, na hakika kabisa walijuwa kuwa chai ya mchai chai ili upate kuburudika na kuchangamsha mwili ni lazima inywewe bila kuchanganywa na maziwa.
 
Ahsante sana X-Paster. Niliutafuta sana mchaichai mara ya mwisho nilipokuwa bongo bila mafanikio yoyote. Naona kuna uwezekano ukapotea maana wengi sasa hivi hawaujui mchaichai. Hao bibi zetu Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi~AMEN.
 
Ahsante sana X-Paster. Niliutafuta sana mchaichai mara ya mwisho nilipokuwa bongo bila mafanikio yoyote. Naona kuna uwezekano ukapotea maana wengi sasa hivi hawaujui mchaichai. Hao bibi zetu Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi~AMEN.

Ukiutaka mchai chai unaweza kuagizia kule Ifakara Morogoro, kwenye mradi wa Mbu (Kama bado upo). Maeneo mengine labda Muheza Tanga.
 
Kweli mdau, mchaichai unatufanya tukumbuke mabibi zetu.
Jina la kisayansi bahati mbaya sijui ningekusaidia.
 
Kweli mdau, mchaichai unatufanya tukumbuke mabibi zetu.
Jina la kisayansi bahati mbaya sijui ningekusaidia.


Wadau michaichai Bongo bado ipo,lazima uende pembezoni ya mji utaipata mingi,tatizo iko ktk viunga vya watu. Na bongo siku hizi kila kitu pesa.
 
Kweli mdau, mchaichai unatufanya tukumbuke mabibi zetu.
Jina la kisayansi bahati mbaya sijui ningekusaidia.
Mmea huu kiasi una majina mengi kidogo... unaitwa:

Lemongrass or lemon grass (Cymbopogon nardus). Pia unajulikana kama mosquito plant, barbed wire grass, silky heads, citronella grass, fever grass or Hierba Luisa.
 
Asanteni sana wakuu...basi naona mbegu nilizonunua obviously ndio zitakuwa hizo...maana nilinunua kutokana na picha ya cover na si jina...Niliona picha inafanana na mchaichai hasa. Jina la packet linasomeka kama CITRONGRÄS; SITRUSHEINÄ, INTIAN (citroen grass which is the same as Lemon grass maybe).
 
Jamani mchaichai hata kwa chai ya maziwa ni mruua sana. Nakumbuka enzi zile bibi anakamua maziwa ya ng'ombe, na lita mbili zinapikia chai wajukuu wote tunajipanga kuzunguka jiko la mafiga kila mmoja ananyoosha kikombe kile cha uhuru (kilikuwa na plastic rangi ya kijani) unawekewa chai na kiporo kwani kila jioni chakula kikipikwa ni lazima kiachwe kingine kwa ajili ya kifungua kinywa asubuhi. Nilikuwa nikiamka tu kwa wazazi break ya kwanza ni kwa bibi na kikombe changu mkononi!!!!!

Ninafurahi bibi yangu yu hai ana zaidi ya miaka 95, ana nguvu, anatembea mwenyewe kwenda kanisani jirani na tunaongea kwenye simu akiwa na akili zake timamu na kuendelea kunitemea cheche za baraka!! Mungu aendelee kumweka hai aone hadi Vilembwekeze!!! Kwa babu yangu, pumzika kwa amani, tumekosa upendo wako kwa miaka 10 sasa.

Sasa basi, bibi yangu huyu ni mpenzi wa mchaimchai sana na hadi naongea hajawahi hata kuugua ugonjwa mkubwa zaidi ya homa za kawaida, hasa unaposema ukizoea kunywa mchaichai utapata ugonjwa wa ini. Pengine ugonjwa unaweza patikana kutokana na kuwa pengine ulipigwa dawa fulani, vinginevyo madaktari wa JF watuambie mmea huu una nini cha asili ambacho kinasababisha ugonjwa wa ini. Mimi nimeupanda kila piece of land I have na ninatumia!!!!
 
Ila msiuzoee sana kwani unasababisha ugonjwa wa inni na mwishowe unaweza kupata kansa ya inni hii iliripotiwa na WHO


Hawa wanasayansi nao, kila kitu kina ubaya wake. Ukiwasikiliza sana hauli chochote. Kuna wakati nimetafuta sana mchaichai sikupata, nilitaka nipande hata katika beseni niweke katika ile corridor ya katikati ya nyumba yetu ya kupanga (hope hawataumwagia chai ya moto).
 
Ila msiuzoee sana kwani unasababisha ugonjwa wa inni na mwishowe unaweza kupata kansa ya inni hii iliripotiwa na WHO

Mkuu ungetuma source ya hii. Sina hakika juu ya hili. Lakini ninachojua hata mama waja wqazito wakitumia ni mzuri sana mtoto anatoka akiwa VERY CLEAN.
 
mchaichai kisayansi ni mchaichai. kingeereza, kijerumani na kifaransa ndio sijui wanauitaje.
 
Ila msiuzoee sana kwani unasababisha ugonjwa wa inni na mwishowe unaweza kupata kansa ya inni hii iliripotiwa na WHO

Mhhhh! Kuna mwanaJF yeyote anaweza kuthibitisha habari hii toka WHO kuhusiana na mchaichai!?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
..mchaichai ..napenda hiki kikombe cha kijani ni kile kilikuwa kimechorwa mwenge au ? unanikumbusha mbali
 
Back
Top Bottom