Mchaga Tajiri Bahili!

Nesindiso Sir

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
379
28
Mzee mmoja wa kichagga tajiri kwa jina la MDAWA alipata ajali mbaya sana ya gari. Alipoteza fahamu na kupelekwa KCMC huku matumaini ya kupona yakiwa yametoweka kabisa. Kutokana na juhudi za madaktari (pengine na Mungu wake) aliweza kupata fahamu baada ya wiki tatu. Muda wote huo familia yake ilikuwa iko
karibu naye kusubiri litakalotokea. Mkewe na watoto wake watatu waliruhusiwa kuwa naye pale ICU (Intensive
Care Unit) kwa zamu. Basi baada ya kupata fahamu nesi aliyekuwa anamhudumia alimwambia;

NESI: Baba pole sana

MZEE MDAWA: Unanipa pole kwani nini kimetokea?

NESI: Baba ulipata ajali mbaya sana ya gari wiki tatu zilizopita.

MZEE MDAWA: Kweli, Kari yangu itakuwa imepona?

NESI: Hapana imeharibika kabisa Baba.

MZEE MDAWA: Hai jamani FII EKIS (VX) yangu. Niliinunua kwa bei kubwa mno. Sasa nitapata wapi
nyingine...aaaiiii aaaaaaiii aaaaaiiii!

NESI: Baba usilie, hilo mbona ni kidogo? Unajua mkono wako wa kushoto umekatika kabisa?

MZEE MDAWA: Mkono wa kushoto? Umekatika? Ule mkono niliovaa ile saa yangu ya bei mbaya? Yaani saa yangu
nayo imekwenda? Aaaiiii....aiiii...aiiiii, jamani saa yangu.

NESI: Baba acha kulia, utaumia zaidi

MZEE MDAWA: Hapana mwanangu, kama kari yangu na saa fyote fimekwenda kwa nini roho isiniume? Hifyo fitu ni
fya bei mbaya sana ati...

NESI: Baba tulia, familia yako iko hapa wanataka kukupa pole.

MZEE MDAWA: Iko hapa ee? Mama Sikola, uko hapa?

MAMA: Ndiyo ! mume wangu, siwesi kukuacha mwenyewe. Pole sana mpenzi. Tunamshukuru mungu sasa unaongea. Yesu asifiwe sana!

MZEE MDAWA: Sawa, Kodilafu uko hapa?

GODLOVE: Ndiyo Mzee, siwezi kukuacha mwenyewe katika hali hii. Pole sana Baba.

MZEE:Sikola, na wewe uko hapa?

SKOLA: Ndiyo Baba, hatuthubutu kukaa mbali na wewe ukiwa katika hali hii baba. Ni hali ya kutisha sana.

MZEE: Na huyu kitinda mimba wangu Ferenaisi, yuko hapa?

Verynice: Niko hapa baba, nyumba yote iko hapa kukupa pole.

MZEE: Basi nyie wote hamna akili hata mmoja. Yaani Mmekuja wote hapa, dukani kabaki nani leo? Yaani
munanona kari yangu ni hiyo imepika msinga tayari na saa yangu ya bei mbaya imepotea badala ya kukaa dukani
wote munaongosana kuja huku KMCC. Nyie ni wajinga wa mwisho kabisa.


Cheers!
 
Yani sijui kwa nini siku zote sikuziona hizi kurasa za udaku. Safi sana. Nimecheka hadi nimefurahi.
 
Back
Top Bottom