Mchaga na Pilau! duh!

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,217
Kuna jamaa mmoja kutoka kilimanjaro, alitembelea zenji. Katika pilikapilika zake za siku nzima, njaa ilimshika na akaamua kwendi hotelini kupata menyu.

Kwa bahati mbaya alikuwa vyakula vimeisha isipokuwa pilau tu. Kwa vile aliwaona watu wakila na yeye alikuwa hajawahi kula akaamua kuagiza pilau. Kwa kweli ilikuwa tamu sana. Aliporudi Moshi akawahadithia wenzake..
''aisee baba'ngu, nilikwenda zanzibar na kuingia kwenye hoteli moja, nilikuta fyakula fyote fyimekwisha, ila kumebakia wali mshafu(mchafu), wali ulikuwa mshafu lakini mtamu kweli baba'ngu. Nilipopiga kijiko cha kwansa nikakutana na vipande fya mbao(amdalasini) kupiga kya pili nikakutana na mbegu za mpapai (pilipili manga) kupiga fya tatu nikakutana na fimbegu fya bangi(iliki). Baba angu japo wali ulikuwa mshafu lakini ulikuwa mtamuuu, kiruuu''

~Pilau lamtoa ushamba~
 
Mifano mingi au topic nying mchaga asipotajwa nahsi server ya JF inaweza kuzimika! Mwe!
 
ila kwa uzoefu wangu mdogo nimegundua watu wa pwani wanajua sana kupika pilau. Na ukitaka kula pilau basi wewe nenda pwani iwe Zanzibar au Tanga yaani ni raha tupu. Moshi kule pilau sio tamu kivile,labda ukutane na mpishi haswa. Na hii ni sababu uwa Pilau la Moshi halina Nazi,na viungo.
Wachaga ni wataalamu wa kupika ndizi na Kitimoto a.ka Noah. Siku hizi gari za noah wanazihita kitimoto.
 
wachaga tuko juu ndio maana haiishi siku hatujatatwa hapa, kichwa kinakuwa kikubwa wewe!!!
 
itabidi wajitenge sasa, jamhuri ya wachaga

makabila mengi yana hofu nao, wivu
 
hapo kwenye wachagga ungebadili kabila, ukaweka kabila lengine ungevutia zaidi mdau!

nyinyi asili yenu ndizi hivyo ukiweka utani wa kutolifahamu pilau vizuri kwa makabila ya watu wa pwani inakuwa hainogi. Si unaona mlivyo-mind? Kwa mtaniaji inakuwa raha!
 
Back
Top Bottom