Mchaga akesha mataa ya Kamata Kariakoo akiangalia TV ya barabarani

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,939
517
Jamani, watu wanasema ushamba ni mzigo. Leo pale Kariakoo Kamata kwenye mataa, nimemkuta jamaa mmoja anaitwa Massawe wa Ushirombo akiwa na suti yake maridadi amekaa chini akiangalia screen kubwa ya matangazo ya biashara pale kwenye mataa Kamata.

Huyu Massawe alikua katulia tuli na soda yake ya pepsi na chips mayai anaangalia ile TV, nilipomuuliza inakuaje Massawe uko hapa?, Akajibu kwa kujihamini "hallow chalii yangu, nipo hapa nasubiria tamthilia ya Isidingo na 24 maana home sina kideo yelewiiii "

Lakini baada ya muda traffic walimuondoa yule Massawe pale barabarani. Ama kweli mjini kuna mambo!

Wakuu mnasemaje kuhusu hili? Karibuni.
 
Hata kama ni uongo basi usipitilize. Ushirombo na wachagga wapi na wapi. Au lengo ni kuwataja Wachagga tu uridhike?

Sawa huyo katokea Rombo, UMERIDHIKA?
 
kua mbunifu kidogo hata kwa kwastori za ku tungaa mkuu daily wachagaa tuu...
 
Ushirombo? Ingawa anaweza kuwa wa huko lakin Ushirombo sio makaz ya wachaga
Exactly ndugu! Mleta mada hajazingatia kanuni moja muhimu ya utani ambayo ni:

Mtu/Watu unaowatania lazima uwajue vizuri eg kufahamu vizuri wanapoishi.

Kwa hiyo kwangu thread hii imebuma vibaya sana kwa sababu anayetaniwa ni mchagga na wachagga asili yao si ushirombo. Tena cha kuchekesha sana hapa ni kwamba mleta mada kapotezwa na neno 'rombo' kwenye Ushirombo.

Tafadhali mleta mada weka jiografia yako vizuri!
 
Hata haichekeshi hata kidogo, kazi kuwadhalilisha Wachaga wa watu tu, Ushirombo yenyewe ipo Geita...!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom