Mch. Peter Msigwa: Wizara ya mali asili na utalii inafuga mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mch. Peter Msigwa: Wizara ya mali asili na utalii inafuga mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by onembuya, Aug 14, 2012.

 1. o

  onembuya Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo Mchungaji Peter Msigwa ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuonesha jinsi uongozi wa Wizara ya Mali asili na utalii unavyowatetea mafisadi na majangili wanaohujumu uchumi wa nchi. Kwa taarifa zaidi soma taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyoambatanishwa.
   

  Attached Files:

 2. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  TAARIFA YA MCH . PETER MSIGWA (MB) KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UFAFANUZI WA MASUALA MUHIMU KATIKA HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KATIKA WIZARA YA MALI ASILI NA UTALII ILIYOSOMWA BUNGENI TAREHE 10 AGOSTI, 2012

  1. Waziri hakujibu hoja za msingi katika hotuba ya Kambi ya Upinzani, na badala yake aliamua kumjadili mleta hoja ambaye ni mimi kuhusu uchungaji wangu kana kwamba ndio ilikua hoja iliyokua inajadiliwa.

  2. Waziri kukana kwamba hakupeana mkono na balozi wa Uingereza wakati wa kukabidhiana faru wakati picha inaonesha hivyo , namwambia kuwa ukiwa muongo usiwe msahaulifu kwani utaumbuka .


  Kielelezo: Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki akipeana mkono na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Dianne Corner mara baada ya kukabidhiwa faru watatu walioletwa nchini kutoka Uingereza kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi

  3. Waziri kutumia muda mrefu na kufanya propaganda kuhusu kosa la uchapaji la jina la kiongozi wa CCM, Mzee Lazaro ambaye anatuhumiwa kwa ujangili wilayani Karatu badala ya kushirikiana na Kambi ya Upinzani katika kuwasaka na kuwatokomeza majangili wa maliasili za taifa.

  4. Kucheleweshwa kwa makusudi marekebisho ya jina husika na kutosambazwa kwa wabunge kwa marekebisho ya hotuba yangu jambo ambalo lilisababisha kuendelea kwa mjadala wa upotoshaji kuhusu hotuba yangu. Huu ulikua mkakati wa viongozi waliokutana hapa bungeni wawili pamoja na afisa mmoja wa serikali na kupanga mpango huo

  5. Maazimio na mapendekezo ya kamati ndogo ya bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu ugawaji wa vitalu vya uwindaji wa kitalii yalipuuzwa na waziri: Mapendekezo ya kamati yalikuwa kwamba vitalu vitangazwe kwa kuzingatia sheria ya manunuzi ya umma kama ilivyorekebishwa mwaka 2011 jambo ambalo halikufanyika.

  MAONI YANGU:
  1. Waziri anaonekana kuwa na kiburi kwa kutojibu hoja za msingi na haoneshi ushirikiano na wabunge na hasa kuhusiana na taarifa muhimu tunazompatia kwa ajili ya maendeleo ya Wizara yake. Jambo hili tasfiri yake kwa jamii ni kwamba Serikali inawalinda majangili na mafisadi wengine katika Sekta hii.

  2. Kauli ya waziri ya kuwatisha watendaji wa wizara yake wanaotoa taarifa za ufisadi kwamba atawachukulia hatua ni silaha ya kibabe ya kuendelea kuwaburuza watendaji wake ili kuficha ufisadi uliopo katika Sekta ya Mali asili na Utalii, nawaambia watendaji wema ndani ya wizara wasikae kimya wakati wanaona ufisadi unaendelea katika wizara.

  3. Kama matatizo ya Vitalu yalisababisha aliyekuwa waziri wa Mali asili na Utalii, Mhe. Maige kujiuzulu, kwa nini huyu waziri wa sasa anaendelea na utaratibu ule ule, tukimuuliza anakasirika? Kulikuwa na haja gani ya kumuondoa Mh. Maige kama utaratibu haubadiliki? Mimi nadhani naye anatakiwa kuwajibika kwa kujiuzulu.

  4. Waziri kuwafukuza kazi watumishi watatu ni kuwahadaa wananchi kwa kuwa amewaacha wale mafisadi waliobobea ambao wako katika nyadhifa za juu walioongoza mchakato mzima wa kusafirisha twiga kwenda nje. Hivi inawezekanaje ndege ya Jeshi la Taifa jingine iingie nchini na kubeba wanyama pori kwenda ratiba ya ndege zinazowasili nchini isioneshe hivyo au hata rada za jeshi letu zisiione?. Hii inaonekana kwamba kuna mtandao mkubwa wa ujangili wa Kimataifa ambao serikali inaujua na inashirikiana nao.

  5. Pia waziri asijisifu kwa kwa kuwafukuza watumishi watatu na kutoa onyo kwa wengine kwani hata waziri aliyemtangulia alifanya hivyo hivyo. Pia Waziri Kagasheki akumbuke wosia wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwamba Serikali inayokimbizana na watu wadogowadogo ni Serikali dhaifu na ni Serikali ‘Corrupt’

  6. Waziri analihujumu bunge haki yake ya kikatiba (ibara ya 63(3) ya kuisimamia na kuishauri Serikali kwa kuwakataza watumishi wasitoe taarifa kwa wabunge. Waziri akumbuke kwamba ufisadi wa Richmond ulifahamika na kukomeshwa kwa kuwa wabunge walikuwa na taarifa mahsusi kuhusu jambo hilo. Kuwakataza watumishi wasitoe taarifa za kifisadi katika wizara yake ni dalili kwamba anatetea ufisadi na kwa maana hiyo hana nia njema na rasilimali za nchi yetu.

  Waziri Kagasheki anaongoza wizara kwa vitisho kama ilivyojidhirisha katika kuwatisha wabunge wasithubutu kutumia nyaraka za Wizara. Huu ni udhaifu mkubwa kwa kiongozi wa kitaifa na vilevile ni dalili ya kuficha maovu na uchafu katika Wizara yake.


  __________________________________________
  MH. PETER MSIGWA (MB)
  WAZIRI KIVULI – MALI ASILI NA UTALII
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo wewe ni katibu muhutasi wa Mchungaji Msigwa?
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  CCM ni Genge la wahuni linalotafuna rasilimali za Watanzania, ni hatari kwa taifa.
   
 5. o

  onembuya Member

  #5
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jadili hoja, usijadili peripheries
   
 6. w

  why JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 203
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiona mtu linamuuma ujue ni miongoni mwa hao mafisadi wengi wa ccm vema tufike mahali tubadilike hapo ni kumuunga mkono mh msigwa mana ameamua kujitoa muhanga katika kuokoa mali za nchi.
  Pia swala kua ni katibu wake sio hoja kwetu hoja ni vip dhuluma iliyopo kwa watanzania
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kagasheki anataka kuongoza wizara kwa kuwatisha watendaji na hilo ndilo litakalokuwa anguko lake kwani wizara hiyo inahistoria ya kufichua ufisadi unaofanywa na viongozi wakuu wa nchi!! Kama unabisha we ngoja uone kama Msekwa ataondoka kama mwenyekiti wa Ngorongoro inspite of all the allegations against him!
   
 8. Josephine

  Josephine Verified User

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante mchungaji.

  Tuliona wengi kwenye taarifa ya habari sijui alikana nini.Not only that amejifanya kuwafukuza watendaji swala si kumfukuza mtendaji tunataka Twiga wetu warudi,
  Japan twiga wetu wametengenezewa zoo watalii wanatoka China,marekani,na Korea kwenda kuangalia Twiga hao.

  Tunataka warudishwe nyumbani.
   
 9. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  sasa Kagasheki analipi la kusema wakati alisema kwenye kukabidhibiwa faru hakuwepo wakati picha inamuonyesha akipeana mkono na balozi mzungu??sijui Vasco anaokoteza wapi hawa watu anaowapa uwaziri??jk mwenyewe ni tatizo!
   
 10. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Kagasheki nae anatengeneza juice ya ndimu...
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Namkumbuka Kagasheki akiwa naibu waziri wa mambo ya ndani, alivyojiapiza kule Nyamongo wakati wa lile SAKATA la binadamu na mifugo kuathiriwa na sumu ya mgodi wa Nyamongo iliyokuwa ina ikitiririka mto Tigit, baada ya kupelekwa sehemu ambayo siyo na uongozi wa Barick kabla ya kutonywa na msamalia mwema kwamba alipopelekwa siko.

  Lakini alivyokuja kunyamaza baada ya kuonana na uongozi wa Barick nikaamini katika CCM hakuna msafi. Msijipe matumaini bure na Kagasheki hapo maliasili hao aliowafukuza ni vidagaa akifika kwa ma-Sangara atanyweya. Hii nchi bila KUONDOA MFUMO CCM, We will Continue to move backwards!
   
 12. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tuvumilie mpaka lini? je sisi ni nani dunia hii tusiwe na kiasi na baadaye kusema inatosha
   
 13. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kaghasheki is like Maige?? watu wale wale.
   
 14. M

  Mlyafinono Senior Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM na Utawala wake hawaminiki
   
 15. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  watanzania wote wenye nia njema na nchi yao ni makatibu muhutasi kwa wapambanaji wa wapora nchi yetu na ushindwe
   
 16. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  inawezekana ni mwananchi wa jimbo lake punguza jazba..
   
Loading...