Mch. Msigwa: Kuna uwezekano baadhi ya mawaziri wetu akili zao zimedumaa

tumemuondoa ngereja wamemleta ngereja umeme bado wa mgao, tumemuondoa waziri maige na kuja kagasheki ni yale yale.
Umeme hauwezi kupatikana kwa kubadilisha mawaziri bila kuwekeza kwenye miundo mbinu ya kisasa ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme. Hapa kwetu tumekuwa hatufanyi uwekezaji wowote wa maana kwenye sekta ya umeme tunabaki kudanganyana kuwa mgawo utakuwa historia! Mgawo hauwezi kuisha kwa mbinu za dharula zenye sura ya Richmond and Dowans na ni uendawazimu kudhani kuwa hizi mbinu ni endelevu. Yawezekana kabisa huku ndio kudumaa akili anakoongelea huyu mchungaji.
 
Nimemshangaa Lukuvi kuchanganya lugha.Msigwa amesema ccm ni chama chakavu,Lukuvi akafikiri amesema ccm ni chama cha CUF,huyu jamaa ni kilaza kweli.

Akili za Lukuvi zimedumaa hawezi kufikiri zaidi ya hapo
 
Magamba ni chama chakavu teh teh teh teh....akili ndogo kuongoza akili kubwa teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh mchungaji msigwa ni noumer!
 
Ili kuondoa uchakavu wa CCM kudumaa kiakili kwa mawaziri mizigo ni kuachana na ufisadi, ujangili, ahadi hewa, utekelezaji mbovu wa mipango ya maendeleo...

wapewe dawa za minyoo na kupunguza vitambi .......vya bia na nyama nyingi......
 
Nilimwona na kumsikiliza. Kuna ukweli katika mtazamo wake. Hali ya nchi yetu sio nzuri hata kidogo, kasi ya kusukuma maendeleo haitoshi kulinganisha na idadi ya mawaziri wetu lukuki waliosambazwa kwenye wizara mbalimbali. Ni kweli pia kuwa tunasubiri miujiza tu kwani hata wakibadilishwa hakuna matarajio kama watakuja wengine wenye kasi tofauti na tuliyo nayo sasa.
Huwa nashangazwa zaidi ninaposhuhudia wanapoteuliwa kuwa mawaziri, eti wanafanya tafrija kubwa wao, familia zao na marafiki zao kuwapongeza kwa kuteuliwa. Na mara zote najiuliza, kwa nini wanafanya sherehe? Jawabu ni kuwa wanafurahia kupata nafasi ya kutumbua rasilimali zetu na kuboresha maisha yao na ya familia zao kwa njia haramu ya wizi, ufisadi na rushwa!! Mungu ibariki Tanzania!!!!
 
Inayotuletea viongozi wachakavu ni CCM yenyewe ambayo imechakaa tayari na tusitegemee kupata viongozi bora kutoka ndani ya CCM iliyo chakaa.Ili tuweze kupata viongozi wasiyo chakaa dawa ni kuiweka CCM pembeni kiwekwe chama kipya ambacho kitakuja na uongozi mpya kabisaa.
 
Wabunge wanaokula ela za safari wote ni wezi, km anajua hataweza kwenda arushe hela(cash retirement)
 
Tatizo la Lukuvi ni akili ndogo. Hapo alipofika ni kwa kujikomba (boot leaking), na fitna na majungu kwa sana.
Huyu jamaa ni sawa na kobe. Ukimwona kobe juu ya mti, ujue kapandishwa.
 
Back
Top Bottom