Mch. Msigwa: I am not that cheap. Polepole na Gerson Msigwa siyo wasemaji wa familia

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,459
40,959
Mchungaji Msigwa ameeleza kwamba kulikuwa na njama zilizokuwa zimepangwa na CCM kuhusiana na Rais Magufuli kumlipia faini ya Mahakama.

Alipokuwa anatoka, tofauti na wakati Halima Mdee na wenzake wanatolewa, ambapo hakukuwa na waandishi wa habari, yeye alipotolewa alishangaa kuwaona CCM na wanahabari na makamera yao. Akawaambia, nirudisheni haraka gerezani. Mimi siyo wa bei rahisi kiasi hicho. Nina msimamo, kuna mambo ya msingi ninayoyasimamia.

Ameeleza kuwa yeye na Rais Magufuli, wana uhusiano wa kifamilia lakini Taifa ni kubwa kuliko familia. Kama Rais Magufuli alimchangia kwa kuzingatia uhusiano wa kifamilia, Polepole anahusikaje? Polepole siyo mwanafamilia. Polepole siyo Msigwa, siyo ndugu. Gerson Msigwa ni ndugu lakini siyo msemaji wa familia, yeye ni msemaje wa Ikulu.

Jambo la kujiuliza: Is Polepole that low, kiasi cha kushindwa kufikiria haya aliyoyahoji Mch. Msigwa?

Kwa maelezo yake, sikiliza video hiyo.
 
Naona hili swala Chadema mmelivalia njuga.

Baada ya bunge kuvunjwa sitashangaa Mchungaji Msigwa akihamia CCM na kuwa mgombea ubunge Iringa Mjini akipigiwa kampeni na Happi plus Kasesela!
 
Polepole na mwenzie Msigwa wa Ikulu,mnatakiwa muitishe wanahabari kwa mbwembwe zilezile mlizozifanya wakati mnamfuata mfungwa Mch.Msigwa kule gelezani mmujibu huyu mtu.vinginevyo hii aibu aitawaisha.
 
Akishajamia huko uchumi utakuwa asee watu wa cccm vichwa vyenu vimejaa kamasi tupu! mpaka sasa wangapi wamwunga juhudi na bado wanafunzi wanakalia matofali darasani badala ya madawati
Naona hili swala Chadema mmelivalia njuga.

Baada ya bunge kuvunjwa sitashangaa Mchungaji Msigwa akihamia CCM na kuwa mgombea ubunge Iringa mjini akipigiwa kampeni na Happi plus Kasesera!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utasubiri sana. Msigwa ana akili, na pia ni msomi mzuri.

CCM ina watu wenye elimu ndogo na wazee (TWAWEZA).
Unatakiwa ujue jinsi ya kuchambua utafiti!

Huu ndio utafiti wa TWAWEZA

CCM na CHADEMA kukubalika.png

CCM kukubalika.png
 
Heshima adabu kwa mtu huyu, ila pia lazima awe ni mtu wa shukrani kwa ndugu yake John Pombe Joseph Magufuli kumlipia.
P
 
Ana undugu na Rais na huwa wana zungumza kifamilia.. sasa wee endelea kutiwa ujinga wa kumchukia rais tu wakati mwenzako akikwama anaweza kusaidiwa na huyo huyo anayekuambia hafai.. ndugu changanya na zako!!☆
 
Back
Top Bottom