Jehovah Shamah
Member
- Aug 29, 2016
- 18
- 10
Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kupanda miti na kutunza mazingira hatimaye kuifanya Dodoma kuwa Kijani.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Iyumbu wakati wa zoezi la upandaji miti leo tarehe 3 Feb 2018 Makamu Mwangalizi mkuu wa Kanisa la Baptist Tanzania Mch Michael Peter Nhonya, amewataka wana Dodoma na Watanzania kupanda miti kwa nguvu zote kuiepusha dunia na majanga.
Mch Nhonya amesema Biblia inasisitiza upandaji miti na utunzaji wa mazingira. Ni vema watu wakajenga utamaduni huu wenyewe badala ya kusubiri oparesheni za panda miti zinazofanywa na Serikali kila mwaka.