Mch. Gwajima, Watanzania hawapingi miradi ya Rais bali wanahoji manufaa yake. Kuropoka kuwa ni wagonjwa unakosea

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,087
6,568
Kama kuna watu ambao huwa nawaona ni waropokaji hapa Tanzania ni huyu mbunge na mchungaji kondoo aitwaye Gwajima aka askofu Rashid.

Hivi huyu askofu Gwajima anajiona ana akili sana au ndio kujipendekeza kupita kiasi kisa tu shemeji yake kapewa Uwaziri na yeye yupo bungeni akibeba pesa za walipa kodi?

Lini au wapi Watanzania wanapinga miradi mkakati ya rais JPM kama anavyoiita?

Kwa taarifa yako wewe Askofu Gwajima Watanzania sio wajinga. Ndio maana wanahoji manufaa watayopata kutokana na uwepo wa hii miradi mkakati.

Mfano kulikuwa na umuhimu gani wa kujenga reli ya SGR ya umeme wakati tungejenga ya kawaida kwa gharama nafuu ingetufaa na kisha pesa zingine zikaimarisha sekta ya afya na elimu ambayo bado inamapungufu makubwa?

Je, kujenga daraja la bil 700 kuunganisha Sengerema na Mwanza kulikuwa na umuhimu kwa sasa, huku wananchi wanaoishi maeneo hayo hawana shule au maji?

Je, manunuzi ya ndege nane kwa cash yanamnufaisha nini Mtanzania wa kawaida ambae kula yake, vaa yake hata kupata matibabu ni shida?

Wewe askofu Gwajima umevamia siasa unadhani ni sehemu ya kuuza porojo za kisiasa na kujipendekeza. Kwa taarifa yako watanzania hawaumwi Schzophrenia bali wanahoji masuala ya msingi.
 
Kwanza kosa kubwa la kwanza ni kuita miradi ya mtu fulani, Sababu ni Kodi zetu na mikopo ambayo vizazi na vizazi vitalipa hatupaswi kuwa na miradi ya mtu, bali miradi ya watanzania ambayo inafanyika baada ya wadau wote na wataalamu kuona tija yake itakuaje.
 
Kwanza kosa kubwa la kwanza ni kuita miradi ya mtu fulani, Sababu ni Kodi zetu na mikopo ambayo vizazi na vizazi vitalipa hatupaswi kuwa na miradi ya mtu, bali miradi ya watanzania ambayo inafanyika baada ya wadau wote na wataalamu kuona tija yake itakuaje
Upo sawa mkuu, miradi ni yetu wote watanzania lazima tuhoji.
 
Back
Top Bottom