Mch. Fernandez amlaumu Nyerere kwa kutaifisha mali za wahindi!

I had the very similar opinions.

Umaskini tunaoupata nchini ni laana juu ya ukwapuaji wa mali za watu. Alichokifanya Nyerere ni wizi tu. Huwezi kuchukua mali za watu kwa dhulma halafu utegemee neema.

Mchungaji umenena kweli na kwa hili mimi nakuunga mkoni 100%. Utaacha nihamie kwenye channel station yako.

Kikwebo.
Na hao wahindi si kwamba walikwapua mali zetu hapa? Walikuja nazo toka India? Si kwamba walitumikisha mababu zetu utumwa na kuwadhalilisha ambayo ni dhambi mbaya kuliko walivyonyang'anywa hizo mali zetu? Hawa wachungaji njaa wanaoota kila siku kwenye jamii zetu kama uyoga taabu. Hawa si wachungaji ni wawajasiriamali.
 
Mch Fernandez wa Agape Ministries kupitia ATN anasema mambo yanayoendelea hapa Tanzania hasa wezi unaofanywa na wawekezaji inatokana na dhambi aliyoifanya Nyerere ya kutaifisha mali za wahindi na watu wengine miaka iliyopita. anasema walichukua mali za watu bila bila ridhaa yao na bila ya kuvuja jasho, ndio maana laana ya alichofanya nyerere ndiyo inayorudi sasa kwa watu kuja kuiba raslimali zetu.

anaunganisha na maneno ya kwenye bible kuwa kama mkuu mmoja wa familia akifanya kosa, laana hiyo inaweza kusambaa na kuwafuata wazaliwa wa mbeleni.

Source ni ATN live boadcasting!
Wapendwa neno la Mungu linasema ukinyanganywa shati mpe na joho, mtu akimupeleka mita 50 nenda nae kilometre moja. Zakayo alipogundua utajiri wake ulitokana na kuonea wanyonge alirejesha mali zote kwa aliowaibia.

Anyway,Hivi tangu amekuwa mchungaji amefungisha ndoa ngapi kati ya muhindi na mswahili? Je kuna mwenye statistics? Je kuna ubaguzi kwenye ndoa? Je ni kweli muhindi akioa mswahili anatengwa?

Dalili wa Upanga kwenye mambo ya nyumba awaambie, mswahili kupanga apartment ni ngapi na muhindi ni ngapi? Nyie mnaoshabikia hili jambo mnashabikia hatari kubwa kwa mustakabali wa Taifa letu. Kwa ufupi, Taifa letu halijalaaniwa hata kidogo, Mungu amelibariki kwa kulipa baraka zote, mito, maziwa, madini etc. tunachohitaji ni kujikomboa kifikra, kumtegemea Mungu na uongozi bora(integrity).

Mimi nadhani yeye aendelee kujikita na kuhubiri injili watu wa okoke, wamjue na kumfuata Yesu kuwa Bwana na mwokozi wao. Agizo kuu "enendeni ulimwenguni mkawafanye watu wote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza ktk Jina la Baba, mwana na Roho Mtakatifu".

WaTZ hawawachukii wahindi na wasichokozwe na maneno Kama hayo! Mbegu hiyo ni mbaya kwa mustakabali wa nchi yetu. Wapendwa na tuliombee jambo hili. Narudia HATUJALAANIWA Bali TUMEBARIKIWA, TUINGIAPO NA NA TUTOKAPO, BWANA AMEBARIKI KAZI ZA MIKONO YETU, TANGU SASA NA HATA MILELE. Amen

Queen Esther
 
mbona hamnijibu swali langu kuwa kwa nini Nyerere aliwanyang'anya nyumba ambazo hakuzijenga yeye
 
Miji mingi tz hadi leo imepambwa nna hizi nyumba, hao jamaa wasingezijenga sjui tungekuwa na miji inayofananaje
 
Back
Top Bottom