Oloronyo
Member
- Mar 29, 2009
- 80
- 9
Maharusi, wazazi wazama bwawani wakikata keki
na Betty Kangonga
MAHARUSI pamoja na wapambe wao usiku wa kuamkia mwaka mpya, walijikuta wakizama katika bwawa la kuogelea jijini Dar es Salaam katika harusi iliyohudhuriwa na baadhi ya vigogo.
Vyanzo vya habari vimelipasha Tanzania Daima Jumatano kuwa tukio hilo lilitokea dakika kumi kabla ya kutimia saa sita kamili usiku, katika Hoteli ya City Garden iliyopo Gerezani, jijini Dar es Salaam.
Maharusi hao (majina yamehifadhiwa) waliingia katika hoteli hiyo na kuanza sherehe kwenye ukumbi wa hoteli hiyo.
Ilipofika majira ya 5:45 maharusi, wasaidizi wao, wazazi wa pande zote mbili na mshereheshaji (MC) Mkongwe Mdachi, walielekea kwenye bwawa la kuogelea hotelini hapo.
Huku wakizongwa pande zote na mapaparazi wa picha za video na mnato ili wapate picha kabambe za kuuaga mwaka 2009 na kuukaribisha 2010, maharusi hao waliombwa kupanda kwenye daraja lililoandaliwa katikati ya bwawa hilo kwa ajili ya kukata keki ambao walionekana kulizidi nguvu daraja hilo.
MC Mdachi aliwaomba wahusika kulizunguka bwawa hilo wakiwa na glasi zao zilizojaa mvinyo, tayari kwa kugonganisha glasi zao kwa pamoja ifikapo saa sita kamili kuupokea mwaka mpya.
Wakati zoezi la kuhesabu likiendelea na kufika nane, ghafla daraja lilikatika katikati kwa kishindo na maharusi, wasaidizi na wazazi walizama katika bwawa hilo.
Tafrani kubwa ilitokea huku wafanyakazi wa hoteli hiyo wakipiga mbizi kuwaokoa maharusi hao ambao walizama bwawani. Hata hivyo, hawakupata madhara.
Maharusi hao wakiwa wamelowa, waliondolewa kuelekea katika hoteli waliyopangiwa kwa ajili ya kujipumzisha kutokana na dhahama hilo wakiwaacha wageni waliohudhuria sherehe hiyo wakiendelea na muziki huku baadhi yao wakiwa wamelowa. SOURCE: SAUTI YA WATU TANZANIA.