Mc Mdachi awaangusha Maharusi katika Swimming pool

Oloronyo

Member
Mar 29, 2009
80
9
Maharusi, wazazi wazama bwawani wakikata keki

na Betty Kangonga



MAHARUSI pamoja na wapambe wao usiku wa kuamkia mwaka mpya, walijikuta wakizama katika bwawa la kuogelea jijini Dar es Salaam katika harusi iliyohudhuriwa na baadhi ya vigogo.
Vyanzo vya habari vimelipasha Tanzania Daima Jumatano kuwa tukio hilo lilitokea dakika kumi kabla ya kutimia saa sita kamili usiku, katika Hoteli ya City Garden iliyopo Gerezani, jijini Dar es Salaam.
Maharusi hao (majina yamehifadhiwa) waliingia katika hoteli hiyo na kuanza sherehe kwenye ukumbi wa hoteli hiyo.
Ilipofika majira ya 5:45 maharusi, wasaidizi wao, wazazi wa pande zote mbili na mshereheshaji (MC) Mkongwe Mdachi, walielekea kwenye bwawa la kuogelea hotelini hapo.
Huku wakizongwa pande zote na mapaparazi wa picha za video na mnato ili wapate picha kabambe za kuuaga mwaka 2009 na kuukaribisha 2010, maharusi hao waliombwa kupanda kwenye daraja lililoandaliwa katikati ya bwawa hilo kwa ajili ya kukata keki ambao walionekana kulizidi nguvu daraja hilo.
MC Mdachi aliwaomba wahusika kulizunguka bwawa hilo wakiwa na glasi zao zilizojaa mvinyo, tayari kwa kugonganisha glasi zao kwa pamoja ifikapo saa sita kamili kuupokea mwaka mpya.
Wakati zoezi la kuhesabu likiendelea na kufika nane, ghafla daraja lilikatika katikati kwa kishindo na maharusi, wasaidizi na wazazi walizama katika bwawa hilo.
Tafrani kubwa ilitokea huku wafanyakazi wa hoteli hiyo wakipiga mbizi kuwaokoa maharusi hao ambao walizama bwawani. Hata hivyo, hawakupata madhara.
Maharusi hao wakiwa wamelowa, waliondolewa kuelekea katika hoteli waliyopangiwa kwa ajili ya kujipumzisha kutokana na dhahama hilo wakiwaacha wageni waliohudhuria sherehe hiyo wakiendelea na muziki huku baadhi yao wakiwa wamelowa. SOURCE: SAUTI YA WATU TANZANIA.
 
hahaaaa mambo mengine bwana!!! walitaka kuwa unique katika sherehe yao, and it happened to a wedding reception of its own!!!
 
kuna dada nafanya naye kazi alihudhuria huko namdadisi km kuna mtu alipiga picha wakati maharusi na baba wakwe wakiogelea kwenye pool tuziweke hapa jf
 
...labda Sijaelewa? Mdachi anahusikaje hapo sasa katika kuwazamisha maharusi ndani ya Swimming Pool??
 
Jamani Jamani, KAMATI ZA MAANDALIZI, ...muwe makini na mipango yenu, kwa nini mlipanga kuwazamisha maharusi? ama mnataka kusema kuwa hela ya kumpa contractor wa daraja hilo haikuwepo?
Mnaooa angalieni kamati zenu vizuri
 
Ngoja niwaambieni yale ninayoyajua. Hiyo ilikuwa ni send off ya binti wa Meja General mstaafu ambaye kwao ni Tanga lakini hivi sasa ni mfanya biashara akimiliki kiwanda cha kushona nguo kule mwenge. Pia ni board member wa First Middle East Bank iliyopo Dar. Huyo siku za nyuma aliwahi kuwa mwambata wa jeshi huko Misri. Ni mzee mmoja ambaye ana nyodo sana na kupenda kuonekana na kusifiwa sifiwa. Alitaka send off hiyo iwe ya kipekee na kwa kweli palipambwa haswa.

Awali alietakiwa kuwa MC hakuwa Mdachi bali alikuwa dada mmoja naye maarufu sana. Dada mmoja wa Kitanga. Siku chache kabla ya siku ya shughuli kufika mawasiliano kati ya Meja General na huyo dada yakapotea. Basi General kumbe alikuwa kakerwa akaamua kumchukua MDachi ambaye pia ni mgosi wa kaya. Yule dada hana habari. Ikawa siku ya shughuli ilipofika yule dada kapeleka vyombo vyake na DJ wake pale city garden (zamani Gerezani Club). Jioni anafika kwenye ukumbi kamkuta Mdachi yuko kazini. Yule dada kuepuka aibu na shari kaondoka kimya kimya kaacha vyombo vyake na Dj wake wanatumiwa na Mdachi.

Sasa yule mjeshi kutokana na uzoefu wake wa kujenga madaraja wakati wa vita akabuni daraja ambalo lilikuwa linapita juu ya hiyo swimming pool. Kumbe hakufanya mahesabu ya kujua ni kiasi gani cha watu wangehimili kusimama juu ya lile daraja. Miongoni mwa waalikwa walikuwemo wahandisi. Wakawa wanajiuliza na kunongona kuwa jamani hili daraja litaweza kubeba watu wote wale.

Nirudi kwa dada MC. Yule dada ni mlokole wa kufanya maombi sana. Akiwa nyumbani kwake akamlilia sana Mola wake. Matokeo ndiyo hicho kituko cha kufungia mwaka cha maharusi na General mwenyewe kutumbukia kwenye pool. Simu zao mahela yao, ATM Cards zao zote zililowa. Hayo yaliyoandikwa kwenye gazeti si uwongo ni ukweli mtupu.

Kuchamba kwingi kushika mavi. Jamani wa kulaumiwa siyo kamati ya maandalizi wala si Mdachi bali ni General mwenyewe.
 
...labda Sijaelewa? Mdachi anahusikaje hapo sasa katika kuwazamisha maharusi ndani ya Swimming Pool

MC Mdachi aliwaomba wahusika kulizunguka bwawa hilo wakiwa na glasi zao zilizojaa mvinyo, tayari kwa kugonganisha glasi zao kwa pamoja ifikapo saa sita kamili kuupokea mwaka mpya.
 
mkuu marigwe
kwa mtazamo na maelezo yako nahisi haina uhusiano na yule dada

1)Huyu general smjui lakini alikuwa ana haki ya kumchukua mdachi;
sababu
kama unawasiliana na mtu na mwishoni mwishoni mwa shuguli mawasiliano yanakatika ualafu unakuja kuleta vyombo;general si mungu kujua kama yule dada angekuja ama lah akaamua kujihami;kama maelezo yako ninavyonukuu

""' Dada mmoja wa Kitanga. Siku chache kabla ya siku ya shughuli kufika mawasiliano kati ya Meja General na huyo dada yakapotea"""

2.)Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
kama unapafahamu hapo walipomwagikia hata wewe uwezi kaa na watu 4
ilikuwa ni maarifa na ufahamu uliowapotoka ndicho walichovuna;pengine kama kulikuwa na""" kamvinyo"" nacho katakuwa kalicontributi

3)Else nielewe yule genera aliktaa mawasilliano yeye bila kumjulisha yule dada
kama ni hivyo basi hapo alikuwa ana shuguli best;unajua watu awajui umuhimu wa watu wa mungu;mi nawaambia watu kabisa chezeeni kila sehemu msinichezee;;biblia inasema msiwaguse masihi wangu""na yoyote atakaeonja lazima azame kama walivyozama maharusi

polen dada MUNGU ni mwema na fadhili zake ni za milele;wanasema shukuruni kwa kila jambo,yawezekana ungekuwepo ungezama wewe,mungu akaona na alishasema ataaangamiza watu wake kwa maji tena tangu nuhu,so endelea na maombi mshike mungu tumia silaha zote ulizonazo kuwaangamiza maadui,yawezekana pesa zilizotumika hapo za mafisadi mungu akupenda ujumuike nazo

kila la kheri
 
Ha ha ha ha ha ha
tuache utani,hii ni kali na imechekeshasha mno...
Yaani ....
 
Hii ingefaa kule kwenye Jokes,na picha za hiyo kadhia kama zipo ziwekwe.

MC Mdachi sioni uhusika wake katika hiyo aibu ya funga mwaka labda kama nia ni kumwaribia umaarufu wake. Yote haya ni ma mbwebwe ya maharusi wa karne hizi. Kutaka kila kitu "westerned". Gharama nyingi, kisha aibu kubwa!.


Sie zamani sherehe za harusi hazikuwepo, wazazi wa mke wanakuletea binti wao wenyewe akiambatana na barua kwenye bahasha iliyogandikwa kwa gundi ya ulimbo au uji wa muhogo kukushukuru kwa uamuzi wako wa kumchukua binti yao kama mkeo kwani waliamini ukioa binti yao na unafanya kazi mjini, ipo siku watakunywa chai ya "sukari" ambayo ilikuwa ni nadra sana kule vijijini.

Ukiwa mjini binti anatumwa kama "parcel" toka kijijini , unampokea binti kituo cha TTCO akiwa amebeba furushi la unga wa muhogo na amekumbatia kuku wake kwa ajili ya mlo wa siku ya kwanza mkikutana ni kama dada yako vile (no kiss, no kukumbatiana).

Haya yenu ya sasa ya makeki juu ya daraja yana umuhimu gani kwenye maisha ya ndoa????
 
honestly hao waliamua kufanya maonesho kwakweli, mi nngekuwa huyo bwa_harusi ningemtwanga m2 mangumi!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom