MC alivyoharibu harusi ya jamaa na kuigeuza msiba, ungekuwa bwana harusi ungemfanya nini huyu kiumbe?

Mdukuzii

JF-Expert Member
Jun 27, 2022
2,555
6,381
Kuna MC fulani kitaa ni muongeaji mzuri, kuna siku alikuwa ana kazi mbili. Moja ilikuwa kuongoza ibada ya mazishi makaburini mida ya alasiri kwenye msiba wa mtu wake wa karibu, alipewa kazi hii kutokana na kuwa muongeaji mzuri.

Usiku alikuwa na kazi ya kuongoza sherehe ya harusi na alilipwa kwa kazi hiyo. Sasa basi ikumbukwe mchana kutwa alikuwa akitaja neno marehemu, mfano sawa ni zamu ya watoto wa marehemu kuweka shada la maua, sijui historia fupi ya marehemu n.k.

Kimbembe usiku kwenye harusi mara mbili alikosea, badala ya kusema wazazi wa bwana harusi akatamka wazazi wa marehemu. Mwili ulikuwa ukumbini akili iko makaburini, harusi iligeuzwa msiba.

MC kama huyu unamfanyaje mfano kukuharibia siku yako muhimu?
 
Unasema aligeuza harusi kuwa msiba, em tuambie nani alikufa hapo harusini
 
Back
Top Bottom