MC afariki akifanya mapenzi na mke wa mtu

Che Guevara

JF-Expert Member
May 22, 2009
1,236
346
Date: 1/5/2010
Daniel Mjema,Moshi

MSHEREHESHAJI maarufu katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, Willy Lema alifariki akiwa anafanya mapenzi na mwanamke ambaye ni mke wa mkazi mmoja wa Nzega mkoani Tabora, Mwananchi imebaini.

Lema, ambaye alifariki akiwa kwenye chumba cha Hoteli ya Newcastle mjini Moshi, ana mke mwenye watoto na familia yao inaishi jijini Arusha.

Uchunguzi wa Mwananchi wa tukio hilo ambalo limekuwa gumzo katika miji hii miwili, umebaini kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano baada ya tukio hilo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinadai kuwa marehemu na mwanamke huyo walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya siri tangu mwaka 2001.

Vyanzo mbalimbali vilivyomkariri mwanamke huyo akitoa maelezo polisi, vimedai kuwa baada ya kufanya awamu ya kwanza ya tendo la ndoa, Lema alimuomba mwanamke huyo wafanye tendo hilo kwa ‘staili’ nyingine, jambo ambalo alilitekeleza.

‘Baada ya marehemu kufanya tendo hilo kwa staili na kumaliza aliishiwa nguvu’, amedokeza mpashaji wa Mwananchi ambaye pia alieleza kuwa kabla ya kufika hotelini, mshereheshaji huyo alichanganya pombe kali ili kupata ‘nguvu’ ya kufanya tendo hilo.

Baadhi ya marafiki waliokuwa na marehemu kabla hajaelekea kwenye eneo la tukio na ambao wameomba majina yao yahifadhiwe, walidokeza kuwa marehemu alikuwa akinywa, bia lakini alipokaribia kuondoka alichanganya kwa wingi na pombe kali aina ya Konyagi.

Inadaiwa marehemu pamoja na mwanamke huyo wote ni wenyeji wa Machame wilayani Hai na walikuwa wamekuja mkoani Kilimanjaro kwa mapumziko ya mwisho ya mwaka ambao ni utamaduni uliozoeleka kwa wenyeji wa hapa.

Habari hizo zinadai kuwa baada ya marehemu kufanya tendo la ndoa kwa awamu ya pili na kuishiwa nguvu alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ambako baada ya wauguzi kumpima waligundua alishafariki kitambo.

Inadaiwa kuwa baada ya kuarifiwa hivyo, mwanamke huyo alitaka kutimua mbio lakini yeye pamoja na dereva wa taxi waliompeleka MC huyo KCMC walizuiwa hadi polisi walipoitwa na kuwachukua kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Nghoboko alisema polisi hawawezi kuingilia starehe za watu bali walichokuwa wakichunguza ni kama marehemu alinyongwa shingo au la lakini wamegundua hilo halikuwepo.

‘Hayo mambo mengine ni faragha za watu... sisi tulichokuwa tunachunguza ni kama alinyongwa au vipi hayo mengine kwa kweli hatuhusiki nayo na hakuna dalili zozote za kunyongwa’, alisema Kamanda Nghoboko.

Watalaamu wa afya wanahisi kuwa huenda marehemu alikunywa vidonge vya kuongeza nguvu (viagra) ambavyo pamoja na pombe nyingine alizokunywa zilisababisha kiwango cha sukari kushuka hadi chini kabisa.

Mwili wa marehemu ambao umehifadhiwa KCMC mjini Moshi kwa uchunguzi zaidi, utazikwa kesho kijijini kwake Machame.
 
Duh! Haya mambo jamani! Sasa hiyo style nyingine aliyopewa jamaa mpaka anapoteza uhai ni ipi? au alipewa tigo makamuzi mpaka akapoteza muelekeo? Dunia ina mambo ya ajabu kabisa.
 
R.I.P mc

mimi nakupongeza kwa ujasiri wako wa kulala na mke wa mtu.
...kama hukum'baka HAINA MBAYA!
PUMZIKA MC wangu!
 
Nasikiaga kule Nzega wanawekaga pin code kwa wake zao, ukigusa tu unakwenda na maji sijui kama ni kweli nasikiaga tu mie mtoto wa watu
 
isije ikawa alikua anamega sana mabibi harusi huyu MC!!.
 
Daniel Mjema,Moshi

MSHEREHESHAJI maarufu katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, Willy Lema alifariki akiwa anafanya mapenzi na mwanamke ambaye ni mke wa mkazi mmoja wa Nzega mkoani Tabora, Mwananchi imebaini.

Lema, ambaye alifariki akiwa kwenye chumba cha Hoteli ya Newcastle mjini Moshi, ana mke mwenye watoto na familia yao inaishi jijini Arusha.

Uchunguzi wa Mwananchi wa tukio hilo ambalo limekuwa gumzo katika miji hii miwili, umebaini kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano baada ya tukio hilo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinadai kuwa marehemu na mwanamke huyo walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya siri tangu mwaka 2001.

Vyanzo mbalimbali vilivyomkariri mwanamke huyo akitoa maelezo polisi, vimedai kuwa baada ya kufanya awamu ya kwanza ya tendo la ndoa, Lema alimuomba mwanamke huyo wafanye tendo hilo kwa ‘staili’ nyingine, jambo ambalo alilitekeleza.

“Baada ya marehemu kufanya tendo hilo kwa staili na kumaliza aliishiwa nguvu,” amedokeza mpashaji wa Mwananchi ambaye pia alieleza kuwa kabla ya kufika hotelini, mshereheshaji huyo alichanganya pombe kali ili kupata ‘nguvu’ ya kufanya tendo hilo.

Baadhi ya marafiki waliokuwa na marehemu kabla hajaelekea kwenye eneo la tukio na ambao wameomba majina yao yahifadhiwe, walidokeza kuwa marehemu alikuwa akinywa, bia lakini alipokaribia kuondoka alichanganya kwa wingi na pombe kali aina ya Konyagi.

Inadaiwa marehemu pamoja na mwanamke huyo wote ni wenyeji wa Machame wilayani Hai na walikuwa wamekuja mkoani Kilimanjaro kwa mapumziko ya mwisho ya mwaka ambao ni utamaduni uliozoeleka kwa wenyeji wa hapa.

Habari hizo zinadai kuwa baada ya marehemu kufanya tendo la ndoa kwa awamu ya pili na kuishiwa nguvu alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC ambako baada ya wauguzi kumpima waligundua alishafariki kitambo.

Inadaiwa kuwa baada ya kuarifiwa hivyo, mwanamke huyo alitaka kutimua mbio lakini yeye pamoja na dereva wa taxi waliompeleka MC huyo KCMC walizuiwa hadi polisi walipoitwa na kuwachukua kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alisema polisi hawawezi kuingilia starehe za watu bali walichokuwa wakichunguza ni kama marehemu alinyongwa shingo au la lakini wamegundua hilo halikuwepo.

“Hayo mambo mengine ni faragha za watu... sisi tulichokuwa tunachunguza ni kama alinyongwa au vipi hayo mengine kwa kweli hatuhusiki nayo na hakuna dalili zozote za kunyongwa,” alisema Kamanda Ng’hoboko.

Watalaamu wa afya wanahisi kuwa huenda marehemu alikunywa vidonge vya kuongeza nguvu (viagra) ambavyo pamoja na pombe nyingine alizokunywa zilisababisha kiwango cha sukari kushuka hadi chini kabisa.

Mwili wa marehemu ambao umehifadhiwa KCMC mjini Moshi kwa uchunguzi zaidi, utazikwa kesho kijijini kwake Machame.

Hapo kwenye red nadhani mwandishi alimaanisha kiwango cha presha/msukumo wa damu na sio sukari

Dah! What a way to go!!
 
Nasikiaga kule Nzega wanawekaga pin code kwa wake zao, ukigusa tu unakwenda na maji sijui kama ni kweli nasikiaga tu mie mtoto wa watu

Nasikia wamekua pamoja tangu mwaka 2001. Dunia imejaa dhambi, miaka 8 yote unakula tu mke wa mtu. Halafu MC ni mchaga oroginal, krismasi kwa krismasi wanakutana Moshi. Wachaga chungeni sana, ooh, unajua twende Moshi tupeleke watoto, tudumishe mila, kumbe kuna njemba fulani.
 
RIP Mc Willy Lema.
Natoa pole za dhati kwa familia ya Bwana na Bibi Lema kwa kuondokewa na nguzo muhimu katika familia.
Binafsi namfahamu sana Bwana Lema kwani niliwahi kufanya nae kazi General Tyre (ea) Ltd kwa muda mrefu,Bwana Lema alikuwa assuarance Manager mpaka General Tyre ilipochimbiwa kaburi na kuzikwa mwishoni mwa mwaka jana.
Msiba ni msiba hata kama unaaambatana na aibu kiasi gani naitakia heri na baraka familia ya Bwana Lema ambae pia alikuwa mwenyekiti wa MC mkoa wa Arusha.
Bwana Lema ametuachia funzo kubwa sisi tuliobaki,tujaribu kuwa makini sana hasa katika mahusianao nje ya ndoa.

Ma MC washakuwa matapeli... ningependa kujua staili hiyo iliyommaliza... labda "shika kitanzi, kifo chaja"
 
R.I.P mc

mimi nakupongeza kwa ujasiri wako wa kulala na mke wa mtu.
...kama hukum'baka HAINA MBAYA!
PUMZIKA MC wangu!

Je angekuwa wa kwako? Roho inakudunda, pumzi inakuishia, roho inakutoka mwanawane, wewe fikiria mkeo kaliwa Viagra, imepigwa raundi mbili, duh. Mimi nampa pole mume wa huyo mama ingawa labda hatazipata pole zangu.
 
yaani nilish2ka sana, pole sana ma dearest friend Lilian...wish ningekuwa bado nipo moshi nije kukufariji kwa karibu.
 
tangu nimekua hadi leo, sijawahi kusikia mtu anaishiwa pumzi na kufa katika tendo hilo likiwa ndani ya ndoa, hivi inakuwaje? Au labda huwa hayasemwi kama ni katika ndoa?
 
Je angekuwa wa kwako? Roho inakudunda, pumzi inakuishia, roho inakutoka mwanawane, wewe fikiria mkeo kaliwa Viagra, imepigwa raundi mbili, duh. Mimi nampa pole mume wa huyo mama ingawa labda hatazipata pole zangu.
........huyo mwanamke ALIBAKWA!??....
 
Ma MC washakuwa matapeli... ningependa kujua staili hiyo iliyommaliza... labda "shika kitanzi, kifo chaja"

huyu mc alikuwa mstaarabu/heshimu kazi yake kupitiliza, akiwa kwenye shughuli yake utamkubali mwenyewe ni mc mzuri sana, sema mambo ndio kama haya tena, i feel sory kwa ma best frnd.
 
Hata kama hajabakwa, je ni halali kumtendea mwenzio jambo kama hilo? We mwenyewe ungeua mtu yangekukuta
SASA nitamuua nani wakati waifu mwenyewe KWA RIDHAA YAKE AMEAMUA KUVUA!

mbaya zaidi amekutwa kwenye nyumba ya kulala wageni,meaning kwamba angespend hapo hata siku mbili WHICH IMPLIES THE possibilities za kutotumia kondom,WHICH JUSTFIES KWAMBA kuna uwezekano watoto mlionao sio wako,WHICH WILL MEAN TO ME kwamba ni lazima nikachek DNA...

yaani SCIENTIFICALLY kuna so many implications.....!tuwe wakweli tuache siasa
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom