mbwembwe za ujenzi wa barabara zashindwa kuwabadilisha mawazo wakazi wa daraja mbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mbwembwe za ujenzi wa barabara zashindwa kuwabadilisha mawazo wakazi wa daraja mbili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by meningitis, Oct 29, 2012.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  kwa miezi kadhaa sasa ujenzi wa barabara mjini arusha umekuwa ukiendelea kwa kasi .hii ilikuwa ni mbinu ya kushawishi wapiga kura wa arusha mjini kuipigia kura ccm.

  Matokeo ya jana ya udiwani wa daraja mbili yameonyesha wazi kuwa pamoja na mikakati ya ccm ya kutumia mgongo wa wafadhili kuhadaa wananchi bado wananchi hawa wameonyesha msimamo wao wa kuifuta ccm mjini arusha.wananchi wameelewa kuwa tunaweza kutumia rasilimali zetu kujenga barabara na kuleta maendeleo nchini.wananchi wanajua kuwa kazi ya ccm ni kutuingiza kwenye madeni huku wakiuza rasilimali zetu kwa wawekezaji wa nje.
  Wananchi wa daraja mbili wanatuambia chadema ndio chama pekee kwa sasa kitakachoweza kutumia rasilimali tulizonazo ili kujiletea maendeleo.

  Wananchi wa daraja mbili hawataki kushabikia barabara za lami zitakazotumiwa na mafisadi na maswahiba wao(wawekezaji) huku wao wakiendelea kutembea peku huku mifuko na matumbo yao ikiwa empty!
  Hawataki kudanganyika na magorofa ya vibopa huku wao wakiugua kifua kilichosababishwa na moshi ndani ya nyumba za tembe!

  Hawa ndio wananchi majasiri wa daraja mbili ambao wameamua kujiunga kwenye mapambano ya haki na kweli.hawa ndio wananchi waliokataa usanii wa kimaendeleo ambao unafanywa na ccm kwa miaka takriban 50.

  Wananchi hawa wanaendelea kutuasa kuwa tumeamua kubadilisha mfumo na kamwe tusirudi nyuma na hadaa za ccm inayotapatapa kudumbukia kaburini.

  Pia wanatueleza kwa wale walioendelea kukubali hadaa za ccm tusiwabeze lakini tuendelee kuwapa elimu kwa msisitizo zaidi.
  Mwisho kabisa wanasema kirusi cha mabadiliko kitaendelea kuikumba tanzania kwani wao kama wana arusha watatumia ushawishi wao kuwakomboa wale waliobakia,hapa wanaashiria mapambano yanahamia arumeru magharibi ambapo jana chupuchupu waizike ccm pale bangata.

  M4C ni mchakato utakaokamilika 2015.M4C itafika pasipofikika.tukumbuke 2005 tulikuwa na wabunge watano,leo hii tuko wapi?
  2005 tulikuwa na kata...leo hii tuko wapi?
   
Loading...