Mbwembwe nyingi za elimu haziendani na tija ya Taifa

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Ni mara nyingi sana ninawasoma watu kwenye mitandao ya habari, wakiziponda elimu za wabunge, elimu za maafisa wa serikali pamoja na mashirika ya umma. Watu wengi wanawekwa kitimoto kwenye mijadala, na kinachohojiwa ni elimu zao kuwa ndogo.

Kwa watanzania wengi vizazi vyenye elimu havizidi vitatu kurudi nyuma. Maana yangu ni kwamba usomi tunaojivunia unawahusu watu wa umri wa Mwalimu Nyerere na kufuatia, yaani watu waliozaliwa miaka ile ya 1920 kuja miaka ya hii ya sasa. Kwenye familia moja ya kawaida ya kitanzania walioelimika ni kuanzia Babu kuja kizazi cha Baba na watoto, lakini Baba yake Babu alikuwa mtupu asiyejua A inaandikwaje. Elimu yetu inawahusu watu ambao wamekuwepo duniani kuanzia mwanzoni mwa karne iliyopita na sio zaidi ya hapo.

Ukitazama wazungu waliotutawala, unakuta kuwa karne tano au sita zilizopita kulikuwa na vyuo vikuu vyenye kuzalisha watu wenye elimu kubwa. Lakini hawa waliotutawala hawaitambii elimu kama sisi tuliotawaliwa tunavyojaribu kujifanya tumeelimika sana. Wanaovumbua injini za ndege, wanaovumbua meli na kompyuta za kila aina hawaiongelei elimu kwa mbwembwe kama sisi tunaoshindwa kuvumbua hata vitu vidogo, tunavyoiongelea kwa kejeli a dharau nyingi.

Binafsi sifurahishwa na ulimbukeni wetu kwenye suala zima la elimu. Zipo kauli nyingi zenye kulenga kuwakejeli watu ambao hawana elimu lakini ukweli ni kwamba vizazi vitano nyuma, hapa Tanganyika (wakati huo ikiitwa hivyo), hapakuwa na mzalendo mwenye kujua kusoma wala kuandika. Leo hii sisi tulioletewa elimu na wale waliokuja kututawala tunaona ufahari sana kuitumia katika kunyanyasia wale wasiokuwa nayo. Tuko nyuma kwenye viwango vya daktari mmoja na idadi ya wagonjwa anaowatibu. Tuko nyuma katika idadi ya wafanya tafiti nzito zenye kueleweka lakini eti tunakuwa wepesi sana katika kuwakejeli wale wasio na elimu!. Hiyo elimu kwanza ioneshe faida zake kwetu binafsi katika uvumbuzi wa mambo yatakayotuweka katika daraja la juu duniani.

Watanzania tubadilike, hizi dharau za kijinga tunazozionyesha wakati elimu kwetu sisi haina zaidi ya karne moja tangu iletwe na wazungu, haziwezi kutujengea heshima zaidi ya kuwa kielelezo cha aina fulani ya ushamba, tunaopaswa kuachana nao.
 
Kuponda watu na kusengenya watu ndio kazi rahisi kuliko zote, na watanzania wengi sana wanaipenda kazi hiyo. Ndio maana nchi yetu itabaki kuwa maskini kwa vizazi vingi vijavyo.
Hata watawala wameshagundua wakisigina demokrasia kwa manufaa yao kikubwa tunachofanya ni kulumbana baadae tunanyamaza.
 
Nimeanza kukudharau sababu ya elimu yako! Ukinijibu swali hili nitakuheshimu. Elimu ni nini?
 
decade<age<generation<century.am not sure kama kuna generation 3 since 1922
 
Umeongea point mkuu,mm mwenyewe naitafakari saana hii elimu yetu.ina tija gan hasa,maana hatuvumbui hata chochote...nikilinganisha na wenzetu wa mbele.lakini kutwa tunajasifu kuwa,tuna Degrees nk.
 
Kwa kweli mm binafsi najiuliza mara nyingi kuhusu hii tunayoita elimu.

Watoto wanapelekwa shule kufundishwa maandishi tu baada ya hapo wanabakia kuzungumzia Degree na Masters ila tija ya hivi vitu kwa taifa na kwa maisha binafsi bado ni kitendawili.
Maprof wangu zaidi ya watatu walikua wanaonyesha kutokuridhika na maisha yao ya kila siku pamoja na elimu na kazi zao.

Wengi wa hawa wasomi wanakimbilia kwenye siasa tumewekeza zaidi kwenye siasa kuliko kitu kingine, hakuna tafiti zinazogaramiwa kwa ajili ya kuboresha maisha yetu.

Wakati fulani nafedheheka sana wanasiasa wanapowatumia wasomi wetu au mtu anapewa nafasi fulani ambayo ni kama msaada ila ukiangalia haitasaidia jamii kulinganisha na shughili ya kitaaluma ya mtu Huyo.
 
Angalia huyu nae ameanza kujisifu na kuponda. Kwa mtazamo wake hiyo ndio faida ya elimu.
Elimu ni nini? Kama hujui elimu ni nini usi-quote kitu ambacho hujaelewa hilo swali rahisi sana na pia ni gumu kuliko unavyofikiria .THINK!
 
Sasa hivi wengi wanakimbilia kupata Masters! Kila msomi sasa hivi utasikia nachukua masters au nipo mbioni kuchukua masters.
 
Nimeanza kukudharau sababu ya elimu yako! Ukinijibu swali hili nitakuheshimu. Elimu ni nini?
Na waitwe dokta, profesa, injinia, wakili msomi, na kadhalika.

Zaidi ya hapo hamna jingine la maana.
Sasa hivi wengi wanakimbilia kupata Masters! Kila msomi sasa hivi utasikia nachukua masters au nipo mbioni kuchukua masters.

Naamini Nyani Ngabu na Sometimes: mna elimu (ya darasani) na siamini mnaweza kuandika hivyo. xaracter: kauliza swali la msingi kwa mleta mada, elimu anayoizungumzia ni nini! Kabla ya kushutumu walio na elimu ya darasani wanafanya nini nchini, jiulize wewe na mimi elimu ya darasani tuliyonayo inasaidia nini!

Wahenga wamenena "Kama unaona elimu ni ghari jaribu ujinga". Mnaoshadidia mleta mada mnajidharirisha.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Na waitwe dokta, profesa, injinia, wakili msomi, na kadhalika.

Zaidi ya hapo hamna jingine la maana.
Tanzania hakuna mwenye elimu bali kuna wenye kukariri masomo na kupata vyeti, maana ya elimu ni kuelewa kitu kikakusaidia kutatua matatizo na kujisaidia mwenyewe na taifa lako, hapa tz mu akimaliza masters na PHD anawaza aingie TANAPA, TPA, TRA, HAZINA,ANESCO akafanye wizi na kujilimbikizia magari na nyumba. Kifuatacho ni kuwa na vimada watano kila kimada na nyumba, kutengeneza migogoro katika family kwani kila siku mama hana amani na kukamata mesagi za kuitwa kutimiza wajibu kwa vimada
 
Tanzania hakuna mwenye elimu bali kuna wenye kukariri masomo na kupata vyeti, maana ya elimu ni kuelewa kitu kikakusaidia kutatua matatizo na kujisaidia mwenyewe na taifa lako, hapa tz mu akimaliza masters na PHD anawaza aingie TANAPA, TPA, TRA, HAZINA,ANESCO akafanye wizi na kujilimbikizia magari na nyumba. Kifuatacho ni kuwa na vimada watano kila kimada na nyumba, kutengeneza migogoro katika family kwani kila siku mama hana amani na kukamata mesagi za kuitwa kutimiza wajibu kwa vimada

mgt software: ati Tanzania hakuna mwenye elimu!!!!!! Toa takwimu ni wasomi wangapi waliokariri masomo na kupata vyeti, la ni wewe mwenyewe. Usisukumwe na hisia na kujumuisha kwa kuwa wewe umeshindwa kutafsiri elimu yako kwa vitendo. Kuna wenye elimu unayoibeza wengi sana km Waalimu, Wahandisi, Madaktari wa afya, Wakadiria majengo, Wahasibu, na wenye taaluma nyinginezo tu wanaondesha shughuli za kila siku za kiuchumi, kisiasa, kijamii nk. Bado huwatambui wakati unapata huduma kutoka kwao!

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Nchini kwetu tunasoma ili tupate kazi za ofisini Kisha tupate mapesa chap chap. Ndiyo maana watu wanakimbilia masters ili iwe kama added advantage kwenye kusaka hizo kazi. Ukizingatia Jamii imeaminishwa kwamba anayefaulu mitihani ndiye Ana akili sana...
kumbe wapi..kibongo bongo anayefaulu ni mtaalamu wa kukariri..(Ndiyo maana wanafunzi toka primary mpaka Elimu ya Juu wanathamini past papers na Reviews kuliko kusoma ripoti za tafiti na vitabu)

Hii misifa haina tija yoyote...

Mfano, kwa mtazamo wangu, tofauti kati ya mtu mwenye bachelor degree na Darasa la 7 hapa nchini kwetu ni kwamba wa degree anajua (si kwamba anaelewa) mengi
Kuliko wa la 7.

Hivi majuzi nimeuliza wanafunzi kadhaa wa UDSM swali hili.

"Kwanini hasi mara hasi ni chanya...?"
Hakuna hata mmoja aliyeweza kunieleza kwa usahihi... (bado nafuatilia)
Lesson: hii inamaanisha mfumo wetu wa kujifunza ni ule wa kutufanya tukariri bila kujua maana halisi ya tunayoyakariri.

Yaani "kariri ufaulu mitihani" Si "elewa ukatumie uelewa kutatua changamoto za mazingira yako"
 
Nimeanza kukudharau sababu ya elimu yako! Ukinijibu swali hili nitakuheshimu. Elimu ni nini?
Akili zile zile za vijiweni, mwenye elimu ya kweli ambayo inatoa msaada kwa waliomzunguka hawezi kujisifia. Matunda ya elimu yake ndio yatakayomtangaza.
 
Huku kwetu kanda ya ziwa maeneo ya sukuma land tuulikuwa tukiambiwa jaga kushule tunasema bhakumara numbu yaani watamaliza samaki
 
Uwe na elimu ya darasani au ya kipaji hutakiwi kudharau wasio na elimu. Aliyeelimika vizuri hawezi kudharau watu. Mafanikio ya mtu yanatokana na watu wanaomzunguka au anaokutana nao, sababu atawategemea wamfanyie kazi zake au wampe taarifa au kwa mambo ya kijamii. Kudharau wasio na elimu kama yako kwa namna moja au nyingine unajikwamisha mwenyewe na taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom