Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Keshatupia huko katika mechi ya kirafiki.
Screenshot_2019-01-10-17-55-47.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kauli yako inachekesha, kazi ya striker ni nini? Ulitaka akiwa kwenye nafasi ya kufunga akipewa pasi aanze kuwalamba chenga huku akirudi golini kwakwe? Alafu ageuke aanze kuwalamba chenga tena ndio afunge? Tatizo la shabiki wa netball mkivamia football ndio hili.

Sent using Jamii Forums mobile app

Dah Safi sana mkuu
 
:D:D:D:D hivi mtoa mada bado yupo kwelii.. naona unayemuita mviziaji anaongoza wazungu huko kwa kutupia magoli
 
Mtoa mada ulikuwa unamuongelea sammata junior au Huyo aliyechini apo kwenye list
 
Attachments

  • Screenshot_2019-02-09-11-15-30.png
    Screenshot_2019-02-09-11-15-30.png
    147.5 KB · Views: 44
Mtoa mada ulikuwa unamuongelea sammata junior au Huyo aliyechini apo kwenye list
Bendera yetu inapeperushwa vizuri, Samata anafungua njia kwa nchi yetu kuangaliwa zaidi hasa katika mashindano yetu ya mpira wa miguu. Tutegemee vijana wengi zaidi kupata nafasi za nje kwakua sasa tutaanza kufuatiliwa zaidi katika league zetu

Mkorintho wa 6
 
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.

Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.

Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).

Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.

Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.

NB: Kama itaonekana sina haki ya kumkosoa Huyu dogo Basi no one has the right to critisize my opinions too.
Ndiyo ni kweli kiwango chake tunatamani kiwe juu zaidi na awe kwenye timu kubwa zaidi LAKINI kwamba kinachombeba hadi kufikia hapo alipo ni bahati, SIYO KWELI. Amepita TP Mazembe na aliiwezesha kuwa bingwa wa DRC na AFRICA wakati huo akiwa mfungaji bora wa klabu bingwa Africa. Na pia alichaguliwa mchezaji bora wa Africa Ligi ya ndani. Sasa hivi anaelekea kuwapa Genk ubingwa wa beligium kwa kuwapa points 3 karibu kila wiki. Kote huko ni kubahatisha?
 
H
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.

Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.

Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).

Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.

Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.

NB: Kama itaonekana sina haki ya kumkosoa Huyu dogo Basi no one has the right to critisize my opinions too.
Na wewe pia uwezo wako was kujieleza ni wakawaida mno, point zako hazieleweki unaongelea ukawaida UPI. Na we we pia uwezo wako was kutoa maoni ni was kawaida sana hats Haumtishi Mbwana Samatta
 
Back
Top Bottom