Mbwana Samatta uwezo wake wa kawaida Mno, Anabebwa na bahati tu!

Ni heri mshambuliaji asiyejua lakini ana bahati kuliko anayejua lakini hana bahati.. (kwa strikers ni stat moja tu muhimu... Kufunga Magoli..)
 
But remember one thing though,you have to be good to be lucky.
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Mbwana Samatta Tangu alivyotua katika Club ya KRC Genk ya Belgium akitokea TP Mazembe ya DRC.

Kiukweli jamaa kiwango chake ni cha kawaida sana na anabebwa sana na bahati kubwa aliyonayo kwani performance yake haitishi sana.

Ukiangalia magoli anayofunga asilimia kubwa ni ya kawaida sana yasiyo na ufundi (hufunga zaidi kwa kichwa na asilimia kidogo kwa mguu na setpieces).

Kwa namna soka la Ulaya lilivyokuwa na ushindani hasa kwa mabeki wakatili (kama akina Pepe) sioni Samatta akifanya lolote mbele yao, kwani mbinu zake mguuni hazitishi mabeki na ni za kawaida sana.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.....Jamaa some how Anajitahidi na anaendelea kujitahidi kwani ameonesha ujasiri na amekuwa Idol kwa Vijana wengi wenye ndoto za mafanikio kwenye soka kama ya Samatta.

Kama ataweza kuuona uzi huu au aambiwe na mtu wake wa karibu aliyeko humu basi nimwombe ndugu yangu Samatta, aongeze zaidi juhudi na ajifunze mbinu nyingi za kufunga kwani yeye kama forward kazi yake uwanjani ni magoli tu na si vinginevyo. Bila kisahau Kujisahau na Kuvimba kichwa akuepuke sana kwani magazeti ya bongo yanapamba wachezaji hadi wanakuwa under pressure na mwishowe huharibu carrier yao.

NB: Kama itaonekana sina haki ya kumkosoa Huyu dogo Basi no one has the right to critisize my opinions too.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom