Mbwana Samatta atwaa tuzo ya mchezaji bora mwenye asili ya Afrika katika Ligi ya Ubelgiji

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta nyota yake imezidi kung’aa baada ya kupata mafanikio siku hadi siku akiwa na club yake ya Ligi Kuu Ubelgiji.

IMG_20190507_083206.jpg

Samatta usiku wa May 6 kuingia May 7 2019 amefanikiwa kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2019 anayecheza soka nchini Ubelgiji, tuzo ambayo inajulikana kwa jina maarufu la Ebony Shoe Award, Samatta anakuwa mchezaji wa tatu wa KRC Genk kuwahi kutwaa tuzo hiyo.

Mchezaji wa kwanza wa KRC Genk kuwahi kutwaa tuzo hiyo ni Souleymane Oulare raia wa Guinea ambaye alishinda tuzo hiyo 1999 na Moumouni Dagano raia wa Burkinafaso aliyeshinda tuzo hiyo 2002, pamoja na hayo Samatta hadi sasa anaongoza kwa ufungaji wa magoli ya Ligi Kuu Ubelgiji akiwa amefunga magoli 23 hadi sasa.

Pamoja na tuzo hiyo Samatta kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji wenye mchango mkubwa katika club ya KRC Genk katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2018/2019 wakihitaji point 4 tu kuwa mabingwa pasipo kujali matokeo ya timu yoyote wakiwa wamesalia michezo mitatu na wana point 41.

Hata hivyo tuzo hiyo inayotolewa kwa mchezaji wa kiafrika au yoyote yule mwenye asili ya Afrika imewahi kuchukuliwa na wachezaji mbalimbali akiwemo mbelgiji Vincent Kompany anayeichezea Club ya Man City kwa sasa , Samatta hakuhudhuria utoajiwa tuzo hiyo kwa zile alizotaja kuwa ni sababu zilizo nje ya uwezo wake
 
Hongera zake, aendelee na juhudi kuboresha zaidi kiwango chake.

Mie sio mfuatiliaji wa haya mambo ya michezo lakini ningependa kujua huko kwenye ligi ya Ubelgiji kuna wachezaji wangapi wenye asili ya kiafrika?
 
Ni wachezaji wengi sana, ila idadi yao sina. Tena nadhani hata anayemfuatia kwenye mbio za ufungaji bora ana asili ya Tunisia au Morocco.
 
Najiuliza ti kwanini wasinge 'generalize' tu, kutoa tuzo kwa mujibu wa race si watapata taabu sana hapo bado kuna Asia na America au wanafanya hivyo kwa waafrika pekee?, na pia kwanini?, naombeni mnisaidie hapo...
 
point of correction Genk ana point 50 na michezo mitatu

ili kua bingwa na kubeba uefa Genk anahitaj

1.kushinda game ijayo dhidi ya club brugge since club bruge ni runner n kaachwa point 6 na michezo mitatu n akishinda hio game atamuacha mpinzan wake point 9 na mechi 2 ambaza hazitaweza kufikiwa

2.kama option ya kwanza itashindikana Genk atahitaj ku draw mech mbili tu moja lazima iwe dhid ya club bruge

3.atahitaj point 4 bila kuhitaj matokeo yoyote ya opponents
 
Match ijayo ni dhidi ya clubb bruggy cha msingia wamfunge. Baasi watatangaza ubingwa.
 
huyu Samatta ni level zingine! sijui km Msimu ujao ataendelea kubaki KRC
Hivi ule uzi wa jamaa anamponda Samatta kisa after injuries akapitia kaukame flani ka magoli sijui upo wapi?mkuu msaada tafadhali.
 
Hongera sana ila post yake ya instagram kuelezea wka nini kashidwa kuhudhuria sherehe kanisikitisha sana kuchapia kwa kuuandika EBBEN badala ya EBONY.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom