Mbwana Samatta alivyotua KRC Genk, sababu ya kuchagua kuvaa jezi namba 77

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta January 29 taarifa za yeye kujiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji zilianza kuenea, na baadae kuthibitika baada ya picha za utambulisho wa staa huyo kuanza kuenea mitandaoni.

Huenda ilikupita au ulipata nafasi ya kutazama sehemu ndogo ya utambulisho waMbwana Samatta ambaye wengi tuliona akitambulishwa na kukabidhiwa jezi namba 77 tukiwa hatujui kwa nini kachagua jezi hiyo, Samatta ameeleza sababu ya kuchagua kuvaa jezi hiyo.


Mbwana Samatta alivotambulishwa Genk​


“Nimechagua jezi namba 77 kwa sababu wachezaji niliokuwa nawapenda mimi kama akina Eric Cantona, Cristiano Ronaldo na David Beckham walikuwa wanavaaa jezi namba 7, Mr Dimitri alivyoniuliza napenda kuvaa jezi namba ngapi nilimwambia jezi 77 kwa maana sikutaka kugombania namba ya jezi, kwa kila klabu unayokwenda ni ngumu kukuta jezi namba 7 haina mtu, sasa sikutaka kugombania namba ya jezi lakini mimi pia ni shabiki wa Man United” -Mbwana Samatta.

Chanzo: MillardAyo
 
Hongera sn dogo wapi dogo Yusuph Soka mlikua nae pamoja by then.
 
Back
Top Bottom