Mbwana Samata Kielelezo Tosha Cha Uwepo Wa Vipaji Tanzania,Nini Kifanyike ?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Akiwa mzaliwa mkazi wa Wilaya ya Temeke Mbagala Mbwana amepigana mwenyewe kwa Juhudi zake binafsi mpaka kufika hapo alipo.hii ni changamoto kwetu watanzania na hasa serikali kupitia wizara ya michezo kuibua vipaji ambavyo ni wazi vipo vingi vilivyojificha Tanzania bara na Zanzibar

Ninawaza tu serikali ingepanga bajeti kubwa ya kutosha ingejenga academy ya kukuza vipaji ambapo kijengwe kituo kikubwa sana hata pale Dodoma pawepo na Shule kuanzia Primary hadi Secondary..walimu wa masomo ya kawaida wawepo wengi wakutosha pamoja na wataalam,wakufunzi wa soka wazawa na wageni toka nchi zilizoendelea waje kufundisha michezo mbalimbali tukianza na soka,riadha,kuogelea nk.Viwanja na vifaa viwepo vya kutosha,then nchi nzima Serikali iwe na utaratibu wa Talent search tuwakusanye watoto wa kuanzia miaka mitano wenye vipaji mbalimbali vya michezo na kuwalea kuwafunza na kuwaendeleza ni wazi tukipata wakufunzi toka nje wakikaa na watoto hawa ndani ya miaka 10,15 tayari tutayaona mafanikio yake kuliko ilivyo sasa ambapo mchezaji akiibuka basi iwe bahati tu

Mwisho tumpongeze Samata kwa jinsi ambavyo anatuwakilisha kama nchi,hakika anaweza na jana Lile goli aliwafunga Liverpool japo lilikataliwa pia aliwafunga fc Napoli.....kwa kuweza kuongoza ligi ya belgium kwa ufungaji,kuweza kucheza fainali kubwa kabisa za ulaya na kufunga magoli ni zawadi na kielelezo tosha kuwa Tanzania tuna Vipaji vingi ambavyo vinahitaji kuibuliwa

Hongera Mbwana Samata.
 
Kuna bondia juzi alikwenda kupigana huko ulaya lakini alipokwenda wizarani alijibiwa hakuna fedha,huyo ni mmoja lakini wanamichezo wote wakiomba hata elfu kumi tu utajibiwa hakuna,wenzetu huko Kenya kila weekend unasikia wanavunja rekodi ya riadha,netball,volleyball,rugb,kuruka nk.Leo hii kwa mfano maeneo ambayo yalitakiwa kujengwa viwanja vya michezo wamepewa magabachori wajenge fremu za nguo,hebu nikuambie huko mikoani na mjini vijana wanacheza ngumi au karate lakini ukikutwa unakamatwa na kuwekwa ndani kwamba wewe ni kibaka wa baadae lakini wakisikia unakwenda kupigana marekani wanashangilia kwa mapambio ya chama lakini wamesahau ulikuwa unafanya mazoezi kuanzia tandika,ubungo,hadi mbuzi,samata anatamani vijana wengi waende mbele lakini je serikali imeweka mazingira?Hayo ndio mafigisu ya nchi hii yaani inasema vijana mjiajiri lakini hakuna mazingira ya kujiajiri.Mchana mwema
 
Ni kweli usemayo mfano ni Bondia Mwakinyo amehangaika mwenyewe

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom