Mbwa Wenye Njaa Waila Maiti ya Mmiliki Wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbwa Wenye Njaa Waila Maiti ya Mmiliki Wao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Mbwa Wenye Njaa Waila Maiti ya Mmiliki Wao
  [​IMG]
  Mbwa Harry na Sally walioila maiti ya mmiliki wao aliyejiua Saturday, December 19, 2009 3:06 PM
  Mbwa wawili ambao walibaki njaa kwa muda mrefu baada ya mmiliki wao kujiua kwa kujipiga risasi, wameila maiti yake. Maiti ya mwanaume mmoja wa nchini Marekani ambaye alijiua mwenyewe kwa kujipiga risasi, imeliwa na mbwa wake wawili ambao walikosa chakula kwa wiki mbili.

  Mbwa hao wawili walibaki na maiti ya mmiliki wao kwa wiki mbili ndani ya nyumba yake bila chakula chochote ndipo walipoanza kuila kidogo kidogo kupooza njaa zao.

  Maiti ya mwanaume huyo iligundulika wiki mbili baada ya kujiua ikiwa imeharibika vibaya baada ya mbwa hao kuila minofu yake.

  Polisi wa Papillion, Nebraska Marekani waliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa uchunguzi wa maiti ya mwanaume huyo ulionyesha kuwa alifariki kutokana na majeraha aliyopata baada ya kujipiga risasi.

  Wataaamu wa wanyama walisema kuwa ni jambo la kawaida kwa wanyama kula maiti iwapo watakaa kwa muda mrefu bila kupata chakula wala maji.

  Taasisi ya kutetea haki za wanyama ya Nebraska ipo kwenye harakati za kuwatafutia mbwa hao mmiliki mwingine.

  Taaisi hiyo ilisema kuwa mbwa hao waliopewa majina ya Harry na Sally hawatasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia kutokana na mkasa huo kwakuwa mbwa hawana kumbukumbu za muda mrefu kama binadamu.

  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3770206&&Cat=2
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,182
  Trophy Points: 280
  Bull dogs sio mchezo...
  Wanaweza hata kuua mtu iwapo utamuudhi
   
Loading...