Mbwa wala mahindi mashambani

Freetown

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
883
73
2008-08-21 09:13:51
SOURCE: Nipashe


Mbwa wanaofugwa na wakazi wa kata ya Kitembe wilayani Rorya wamegeuka wanyama waharibifu kwa kula mahindi mabichi mashambani.

Uharibifu huo wa mazao umesababisha kushuka kwa kiwango cha uvunaji msimu huu na hivyo kuongeza wasiwasi wa upungufu wa chakula, kwa mujibu wa wanavijiji.

Wakazi wa kata ya Kitembe waliozungumza na gazeti hili walisema tatizo la mbwa kuvamia na kushambulia mahindi mabichi mashambani kama nyani na nungunungu, lilianza tangu mwezi Mei.

Kwa mujibu wa wanavijiji, baada ya kuona mahindi yanazidi kushambuliwa waliweka mitego ya sumu wakitarajia kuwaangamiza wanyamapori lakini matokeo yake waliwanasa mbwa wafugwao.

``Mbali ya kula mahindi mabichi mashambani wanasaka na kutafuna magunzi ya mahindi yaliyochemshwa,`` alisema Bw. Jared Nyakira.

Wanavijiji hao walisema wamewasilisha taarifa hizo katika ofisi za mifugo na kilimo wilayani hapa wakiomba uchunguzi wa kitaalamu kufanyika na pia kutafuta ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom