Mbwa wa Ajabu Atishia Amani, Aleta Hofu Kubwa– Goba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbwa wa Ajabu Atishia Amani, Aleta Hofu Kubwa– Goba

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Jul 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  MBWA wa ajabu aliyepachikwa jina la mbwa mtu anatia hofu wakazi wa maeneo ya Goba kutokana na kukimbiza watu hovyo na kutafuna mifugo na hata kutafuna mbwa wenzake Mbwa huyo mithili ya mbwa mwitu ana vitendo mithili ya binadamu anakimbiza watu na kutafuna kuku hovyohovyo na kupelekea watu zaidi ya watano kujeruhiwa na kulazwa hospitalini kutokana na kujeruhiwa na mbwa huyo.

  Jibwa hilo asiyejulikana mmiliki wake halali na amezuka katika maeneo hayo na kupelekea kutishia amani ya wakazi wa maeneo hayo na kufanya wajifungie ndani muda wote kutokana na vitendo vya mbwa huyo.

  Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Goba, Laurent Mtego amesema hofu kubwa imetanda kwa wakazi wake hadi kupelekea wakazi wa maeneo hayo kuogopa kutoka majumbani mwao kwa hofu ya kukimbizwa na jibwa hilo ambalo halijulikani ni la nani na limetokea wapi.

  Amesema inawezekana jibwa hilo ana kichaa cha mbwa na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari sana na mbwa huyo ambaye ni mithili ya Sokwe.

  Pia kuwasihi wakazi kuwahi majumbani kwa kuwa jibwa hilo linaanza kushambulia watu majira ya usiku, na kuwataka wananchi kutohusisha vitendo vya jibwa hilo na imani za kishirikina kwa kuwa watu wanachukulia vitendo vya jibwa hilo na imani za kishirikina.

  Amesema hatua mahususi zinachukuliwa na tayari wameshawasiliana na wataalamu kutoka Manispaa ili kuja kulishughulikia suala hilo.

  Hivyo aliwataka wakazi hao pindi mtu anapojeruhiwa na jibwa hilo kuwahi zahanati haraka akapate chanzo ya kichaa cha mbwa.

  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2579666&&Cat=1
   
Loading...