Mbwa ni wako faza

Nov 13, 2010
91
7
Baada ya kumaliza ibada ya jumapili, padri mmoja alitoka kwa ajili ya kupunga upepo. Akiwa katika matembezi akakutana na watoto watatu wakigombana. Walikuwa wananyang'anyana kitoto cha mbwa. Yule padri akawauliza kisa cha ugomvi ule. Wale watoto wakamwambia kuwa wamemwokota yule mbwa, sasa kwa sababu wako watatu wakaamua kila mmoja aseme uongo na atakayesema uongo mkubwa zaidi ndiye achukue yule mbwa. Wote wanadai kusema uongo mkubwa ndio maana wanagombania.

Yule padri akaanza kuwahubiria kuwa kusema uongo ni dhambi na akawaambia kuwa akiwa katika umri kama wa watoto wale hakuwahi kusema uongo hata siku moja.

Mtoto mdogo kuliko wote akamchukua yule mbwa na kumkabidhi padri, "Faza, huyu mbwa ni wako. Umetushinda kwa uongo!"
 
Tuache msg za kuwakashifu viongozi wa Kiroho kwa vyeo vyao mfano mapadri, mashehe nk. Ungeweza kutumia hata masharubu kwa mfano
 
Hakuna utani kwa viongozi wa dini, bado nasisitiza tumia majina ya utani kama ya humu jamvini lakini acha utani na viongozi wa kiroho Mr. Tanga Nyika
 
Baada ya kumaliza ibada ya jumapili, padri mmoja alitoka kwa ajili ya kupunga upepo. Akiwa katika matembezi akakutana na watoto watatu wakigombana. Walikuwa wananyang'anyana kitoto cha mbwa. Yule padri akawauliza kisa cha ugomvi ule. Wale watoto wakamwambia kuwa wamemwokota yule mbwa, sasa kwa sababu wako watatu wakaamua kila mmoja aseme uongo na atakayesema uongo mkubwa zaidi ndiye achukue yule mbwa. Wote wanadai kusema uongo mkubwa ndio maana wanagombania.

Yule padri akaanza kuwahubiria kuwa kusema uongo ni dhambi na akawaambia kuwa akiwa katika umri kama wa watoto wale hakuwahi kusema uongo hata siku moja.

Mtoto mdogo kuliko wote akamchukua yule mbwa na kumkabidhi padri, "Faza, huyu mbwa ni wako. Umetushinda kwa uongo!"

???????
 
mhh siku hizi naona hakuna utani mwingine zaidi ya maaskofu,masister inatia kichefuchefu kwa kweli:rain:
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom