Mbwa adaiwa kukutwa Kilele cha Mlima K’njaro

Averos

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
993
695

WATALII kutoka Ufaransa waliopanda Mlima Kilimanjaro, wameibuka na kioja cha mwaka jana baada ya kuonyesha picha ya mbwa wanayedai yuko juu ya mlima huo.

Kama tukio hilo litakuwa la kweli, basi litaweza kuwa moja ya maajabu ya dunia kwa mwaka huu ambao mlima huo umewekwa kwenye tovuti kwa ajili ya kupigiwa kura ili kuingizwa kwenye maajabu ya dunia.

Watalii wanne raia wa Ufaransa waliopanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kampuni ya Ahsante Tours ya mjini Moshi, ndiyo waliosema walimwona mbwa huyo akiwa amejikunyata kati ya kilele cha Uhuru na eneo la Stella.
Eneo hilo ni umbali wa urefu wa kati ya mita 5,895 na 5,730 kutoka usawa wa bahari, huku kiwango cha baridi kikiwa kati ya nyuzi joto hasi nne 4 hadi -15.

Mmoja wa watalii hao, Antoine le Galloudec, aliyeongozana na watalii wenzake watatu, Kristina Meese, Irina Manoliv na Monique Indino, ndiye aliyedai kufanikiwa kumpiga picha mbwa huyo kwa kutumia simu ya Iphone.

Katika barua pepe aliyolitumia gazeti hili jana, Galloudec alisema wakati akishuka kutoka Kilele cha Uhuru kuelekea Kituo cha Stella, alihitaji kujisaidia na wakati anafanya hivyo ghafla alimwona mbwa huyo.

“Nilipoanza kujisaidia ghafla macho yangu yakaona kitu umbali wa mita moja hivi kutoka nilipokuwa nimesimama kwenye jabali, sikuamini lakini alikuwa ni mbwa akinitazama machoni huku akitingisha kichwa,” alisema.
Galloudec alisema ilimchukua sekunde kadhaa akili yake kurejea hali ya kawaida, ndipo alipotoa simu yake ya mkononi aina ya Iphone na kumpiga picha na kurejea mahali alipowaacha wenzake.

Ofisa Masoko wa Kampuni ya Ahsante Tours, Abel Edward, alisema mara ya mwisho mbwa aliwahi kuonekana eneo la Kambi ya Baranco, ambalo ni umbali wa urefu wa mita 3,960, miaka 10 iliyopita.

“Waliposhuka na kutuonyesha picha ya mbwa yule hatukuamini na tulijiuliza alifikaje huko na alikuwa anakula nini? Maana eneo la mwisho kuwa na panya ni Barafu ambalo ni urefu wa mita 4,640,” alisema.

Daktari bingwa wa wanyama, Dk Wilfred Marealle, alisema siyo ajabu mbwa kuishi eneo lenye baridi kali na barafu, ila kwenda hadi juu ya Mlima Kilimanjaro siyo jambo la kawaida labda awe na kichaa.

“Mbwa kwenda kule (Mlima Kilimanjaro) siyo kitu cha kawaida, labda awe na kichaa maana akiwa hivyo anaweza kwenda popote bila kujitambua, kwa hiyo watu wakae mbali sana na huyo mbwa,” alionya Dk Marealle.

Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Paschal Shelutete, alisema haamini hadi pale atakapotumiwa picha.

Mkurugenzi wa Ahsante Tours, Cathbert Swai, alisema tukio hilo limefanya kampuni kupata maswali mengi kutoka kwa watalii na waliopiga picha hizo wanakusudia kuzichapisha kwenye majarida ya kimataifa.

Source: Mwananchi

VITUKO KILIMANJARO

Mbuzi mwenye maandishi ya quruwani azaliwa Kilimanjaro.

Je huyo mbwa naye hana maandishi yeyote?

Kama ingekua ni mbongo kamwona huyo mbwa angesema kwenye mlima wa kilimanjaro kuna jini.

VITUKO KILIMANJARO

Mbuzi mwenye maandishi ya quruwani azaliwa Kilimanjaro.

Je huyo mbwa naye hana maandishi yeyote?

Ana maandishi ya biblia.

Back
Top Bottom