Mbwa 3 waliomg'ata Kingunge waponea chupuchupu kupigwa risasi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Capture.PNG

Kingunge aliyezaliwa Mei 30, 1932, alifariki dunia Febrauri 2 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kung'atwa na mbwa wake nyumbani Desemba 22, mwaka jana.

MBWA KINGUNGE 2.jpg

Ilielezwa kuwa mbwa hao ambao walikuwa wakihudumiwa na walinzi hivyo kutowahi kumtambua mwenye nyumba, walimshambulia marehemu alfajiri wakati akienda mazoezini; akidhani wameshafungiwa bandani.

Mtoto mkubwa wa marehemu, Kinjeketile 'Kinje' Mwiru aliiambia Nipashe iliyotaka kufahamu walipo mbwa hao sasa na hatma yao jana kuwa baada ya mkasa huo, familia ilitaka kuwaua kwa kuwapiga risasi kwa kuwa ilikuwa haitaki kuwaona tangu walivyomng'ata baba yao.

Badala yake, alisema Kinje, wamekabidhiwa kwa wataalamu wa mafunzo ya mbwa baada ya familia hiyo ya jijini Dar es Salaam kuwakataa.

Kingunge alifariki dunia Februari 2 mwaka huu majira ya saa 10 alfajiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alipokuwa akitibiwa majeraha yalitokana na shambulizi hilo nyumbani kwake Victoria.

"Wale mbwa tuliwagawa," alisema Kinje na kueleza zaidi:

"Kuna hawa wataalamu wa mafunzo ya mbwa walikuja kuwafuata maana sisi tulitaka kuwapiga risasi (lakini) watu wakasema hapana, watatuletea watu ambao wanawahitaji ndipo walipokuja. Tukaamua kuwapa.

"Tangu wamnga'ate baba tulichukizwa nao sana na hakuna mtu aliyekuwa anapenda kuwaona tena wakiendelea kukaa hapa. Hivyo badala ya kuwaua kwa kuwapiga risasi tukaona tuwape watu wanaowahitaji."

Desemba 22 mwaka jana, wakati akitoka ndani kwenda mazoezi ya kutembea asubuhi, mbwa hao walimshambulia kwa kumng'ata maeneo mbalimbali ya mwili majeraha ambayo hatimaye yalipelekea kifo chake.

Rais John Magufuli aliongoza mamia ya waombolezaji waliomzika Kingunge katika Makaburi ya Kinondoni.

Kabla ya mazishi kufanyika katika makaburi hayo, mwili wa mwanasiasa huyo uliagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, marais mstaafu Jakaya Kikwete, Benjamini Mkapa na Ali Hassan Mwinyi.

Wengine ni Makamu wa Rais mstaafu, Mohamed Gharib Bilal na mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Mizengo Pinda.

Viongozi wengine ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na katibu wake, Maalim Seif Sharif Hamad.

Wengine ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba na Mama Maria Nyerere.

Akizungumza kwa niaba ya serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jaffo alisema serikali inatambua mchango mkubwa uliofanywa na Kingunge katika kipindi chote alichokuwa akishika nafasi mbalimbali serikalini.

Alisema akiwa kiongozi wa umma, Kingunge alikuwa mtumishi aliyekuwa mzalendo wa nchi yake, aliyesimamia kwa dhati majukumu yake na kusimamia kile alichokuwa akikiamini.

Mwezi mmoja kabla ya kifo chake, familia ya Kingune ilimpoteza mama na mke wa mwanasiasa huyo, Peras ambaye alifariki dunia Januari 4 MNH pia baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya kupooza mwili.

Chanzo: Nipashe
 
Looh, kumbe ndivyo ilivyokuwa!! So sad, mzee pumzika kwa amani! Mbwa walitamatisha maisha yake....
 
Muhimbili hawawezi kutibu majeraha ya mbwa? Hao mbwa anina gani? Isijekuwa na ufundi umepita manake alikuwa mtata sana.
 
Bora kufuga mbwakoko, wao ni mahodari wa kubweka na kutoka nduki, halafu wana adabu sana wakikuona wanatikisa mikia tu na kuruka huku na kule, sasa hao wenu sijui wa kijerumani, mh!
Wenyewe huita german shepherd
 
View attachment 694947

Kingunge aliyezaliwa Mei 30, 1932, alifariki dunia Febrauri 2 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kung'atwa na mbwa wake nyumbani Desemba 22, mwaka jana.

View attachment 694946

Ilielezwa kuwa mbwa hao ambao walikuwa wakihudumiwa na walinzi hivyo kutowahi kumtambua mwenye nyumba, walimshambulia marehemu alfajiri wakati akienda mazoezini; akidhani wameshafungiwa bandani.

Mtoto mkubwa wa marehemu, Kinjeketile 'Kinje' Mwiru aliiambia Nipashe iliyotaka kufahamu walipo mbwa hao sasa na hatma yao jana kuwa baada ya mkasa huo, familia ilitaka kuwaua kwa kuwapiga risasi kwa kuwa ilikuwa haitaki kuwaona tangu walivyomng'ata baba yao.

Badala yake, alisema Kinje, wamekabidhiwa kwa wataalamu wa mafunzo ya mbwa baada ya familia hiyo ya jijini Dar es Salaam kuwakataa.

Kingunge alifariki dunia Februari 2 mwaka huu majira ya saa 10 alfajiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alipokuwa akitibiwa majeraha yalitokana na shambulizi hilo nyumbani kwake Victoria.

"Wale mbwa tuliwagawa," alisema Kinje na kueleza zaidi:

"Kuna hawa wataalamu wa mafunzo ya mbwa walikuja kuwafuata maana sisi tulitaka kuwapiga risasi (lakini) watu wakasema hapana, watatuletea watu ambao wanawahitaji ndipo walipokuja. Tukaamua kuwapa.

"Tangu wamnga'ate baba tulichukizwa nao sana na hakuna mtu aliyekuwa anapenda kuwaona tena wakiendelea kukaa hapa. Hivyo badala ya kuwaua kwa kuwapiga risasi tukaona tuwape watu wanaowahitaji."

Desemba 22 mwaka jana, wakati akitoka ndani kwenda mazoezi ya kutembea asubuhi, mbwa hao walimshambulia kwa kumng'ata maeneo mbalimbali ya mwili majeraha ambayo hatimaye yalipelekea kifo chake.

Rais John Magufuli aliongoza mamia ya waombolezaji waliomzika Kingunge katika Makaburi ya Kinondoni.

Kabla ya mazishi kufanyika katika makaburi hayo, mwili wa mwanasiasa huyo uliagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, marais mstaafu Jakaya Kikwete, Benjamini Mkapa na Ali Hassan Mwinyi.

Wengine ni Makamu wa Rais mstaafu, Mohamed Gharib Bilal na mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Mizengo Pinda.

Viongozi wengine ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na katibu wake, Maalim Seif Sharif Hamad.

Wengine ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba na Mama Maria Nyerere.

Akizungumza kwa niaba ya serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jaffo alisema serikali inatambua mchango mkubwa uliofanywa na Kingunge katika kipindi chote alichokuwa akishika nafasi mbalimbali serikalini.

Alisema akiwa kiongozi wa umma, Kingunge alikuwa mtumishi aliyekuwa mzalendo wa nchi yake, aliyesimamia kwa dhati majukumu yake na kusimamia kile alichokuwa akikiamini.

Mwezi mmoja kabla ya kifo chake, familia ya Kingune ilimpoteza mama na mke wa mwanasiasa huyo, Peras ambaye alifariki dunia Januari 4 MNH pia baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya kupooza mwili.

Chanzo: Nipashe
Kosa si la mbwa kwani hivyo ndivyo walivyofunzwa ili wawe na ulinzi wa kiwango cha juu kuliko binadamu, hawahongeki wala hawadanganyiki na chochote, naamini marehemu alikuwa analijua hili ndiyo sababu alikuwa nao, poleni kwa kosa lililotokea.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom